Serikali yanywea

Serikali yanywea

Unajua kinachogomba hapa ni sababu ya kufuta hiyo misamaha...
Na nini kimetokea ghafla hadi kugeuza sababu hizo na kuifanya serikali kubatilisha uamuzi wake?
Pinda anasema alikutana na viongozi wa dini (jana) na kisha akaenda kuonana na muungwana (leo) na kukubaliana kuwa uamuzi huo ubatilishwe.
 
iam getting old once i start thinking madudu ya hii serikali ya Kikwete.Ni upuuzi mtupu mawaziri wanakurupuka tu ..yaleyale ya kuanza kulia mbele ya bunge...
 
Kwa kweli msimamo wangu unabaki kuwa dini ni kitu personal ambacho hakiwahusu watu wengine ambao si members wa dini hiyo. Kuendelea kutoa misamaha ya kodi kwa dini ni kutoa preference kwa wenye dini. Wasio na dini nao wanavyo vitu personal wanavyovipenda lakini havisamehewi kodi. Dini ni personal sawa na unywaji wa pombe au uvutaji wa sigara. Wenye dini wanastahili kulipia vifaa vyao vya ibada kama wanavyolipa sadaka na zaka makanisani bila kuhoji matumizi yake.
Ni kweli kuwa dini ni kitu personal. Ila kinapokuwa haki-generate profit sioni sababu ya kukitoza ushuru. Vile vile taasisi za dini zina mchango mkubwa kwa amani na utulivu wa jamii yetu. Mafundisho yanayotolewa na dini mbalimbali huisaidia sana serikali kupata nafasi ya kuongoza. Kwa maana nyingine, dini ni silaha mojawapo ya serikali. Hili pia linajitokeza katika ushiriki wa dini mbalimbali katika utoaji wa huduma za jamii kama mashule, hospitali n.k.

Ukizitoza ushuru si tu kwamba zitadhoofika kiutendaji, bali pia hazitakuwa na sababu ya kuendelea kushirikia na serikali inayoviumiza kwa kodi.

Mkuu, si kweli kuwa u-personal wa dini ni sawa na u-personal wa sigara na/au bia. Bia na sigara ni profit generators wa wanaozizalisha, kuzisambaza na kuziuza. Hivyo hao ndio wanaokatwa kodi na ni wajibu wa serikali kufanya hivyo.

Kazi za dini zote zinatakiwa ziendelee kubaki za kukuza waumini wake kiroho. Baadhi hujitafutia uwezo kwa kuanzisha mashirika yanayoweza kuwapa kipato. Labda katika hayo ndio serikali ingeweza kutoza ushuru kidogo. Lakini pia, Dini hizi zinahitaji kuwa na uwezo wa kufanya shughuli zake. Na kila shughuli inahitaji pesa.


Hata hivyo, logic ya kumsamehe kodi Barick gold na kumtoza kodi mwenye kanisa ndo inayofanya ni withdral support yangu kwa suala hilo.

Mikataba ya madini iliyosainiwa iko juu ya sheria zote zitakazotungwa mpaka muda wa mikataba ile utakapoisha. Nilishangaa nilipogundua kuwa misamaha iliyofutwa kwenye madini ni kwa makampuni ambayo hayajaingia nchini yaani makampuni ambayo hayapo. Yale yaliyopo misamaha kama kawaida.
Kama hii ni kweli, basi ni dalili ya serikali kutokuwa makini. Maana ni kwamba, kuna sheria kwa makampuni yasiyokuwepo na yale yaliyopo. Ni kweli hii?

Sasa ikiwa hawa wanaozalisha faida kubwa huko kwao wanaachiwa halafu tunatozana sisi hata kwenye vifaa vya ibada, huu ungekuwa utaahira. Kwanza kodi yenyewe ingekuwa only symbolic.

Kwa hiyo aliyeileta kodi hiyo aliazimia kuzikomoa taasisi za kidini ambazo anadhani hazimhusu.
Nina uhakika kuwa kesho Mkullo atakapotangaza mabadiliko ya Bajeti yake, atarudisha misamaha/mapunguzo ya kodi yaliyotolewa na serikali kwenye ile ya kwanza. Mapunguzo ya VAT hadi 18% sasa yatarudi kama yalivyokuwa. Sina uhakika kama anaweza kurudisha ushuru wa meli ambao ulikuwa umefutwa hapo awali.

Kimsingi, Bajeti yake ya awali ilitoa unafuu kiasi kwa walaji (wananchi). Ila kwa kuwa hili limejitokeza, basi unafuu ule ama utaondolewa, au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa.
 
Recta,

Ni kweli kufutwa kwa misamaha ya kodi kwenye mafuta mazito yanayoagizwa na makampuni ya mafuta hakuwahusu wale wenye mikataba tayari. Kuna wahusu wale watakaoingia baada ya sheria hii.
 
Clever men know how to solve their problems, but wise ones know how to avoid them

Mkuu Mpita Njia signature yako inaleta maana kubwa hasa ktk U-Turn kama hizi. Binafsi nilijua hawataweza kustahimili moto wake. ... wenye busara wanajua namna ya kuzuia matatizo...
 
Kweli hawa viongozi wetu ni wazembe na wavivu wa kufikiria.

Kwa Mkulo tu kusema kuwa ushuru unafutwa kwa NGO na Taasisi za dini eti sababu kuna baadhi ya taasisi na NGO zinailetea hasara serikali kutokana na bidhaa zao nyingine kuwa za biashara, haikuleta maana kabisa.

Swali lililonijia haraka haraka ni kwamba, kama wanafahamu hizo taasisi na NGO, kwa nini hazikuchukuliwa hatua? Nini kilikuwa kikwazo kikubwa?

Kama kikwazo ni uwajibikaji wa idara ya serikali kama TRA, tafuta chanzo ni nini?

Either uongozi wao ni OVYO, kwa hiyo fukuza kazi wote! OR
Wanahitaji more manpower and resources, ajiri watanzania (more employment to meet JK goal of 1M).

That's my short conclusion on little info I got from this saga. Our so called leaders need to use your heads to think a little bit.
 
Hiyo ni weakness kubwa sana, mpaka sasa sijaona sababu kwa nini wasitozwe kodi kwenye non-spiritial services.

Nitawaunga mkono tu kama watapunguza matumizi ya serikali, kutangaza kuuza VX zote... na waziri apewe SUV [RAV 4, Honda, Suzuki Vitara]!!!

Jana na juzi nimekuwa nikipita pale KCB Posta opposite na Wizara ya Ujenzi. Kila niki-check parking lot kichwa inagonga "You are now walking in the City of Danganyika Republic"

Macho yangu huziona STK mpya kabisa na nyingine bado zina makaratasi. Ziko kama saba hivi zote nyeupe pee. Labda hizi sio VX ambazo serikali imetangaza kusitisha uagizaji wake. Kwa sababu hazina sticker na rangi za ki-heshimiwa. labda tuziite land Cruiser-Mapalachichi. Na ghalama yake itakuwa ya Ki-palachichi.
 
Uamuzi mzuri sana huu maana mantiki ya misamaha hii ililenga zaidi kuudidimiza ukristo. Angalia mifano aliyoitoa Mkulo inahusu Makanisa tu. Pia hakukuwa na mantiki kuwaadhibu Wakristo wote kwa makosa ya wachache. Sheria ziko wazi. Atakayekiuka ndiye aadhibiwe. Kwa mfano dhehebu au shirika la dini lilitakiwa liagize magari kwa ajili ya shughuli za kiroho halafu lenyewe likayaingiza kwa ajili ya biashara. Kinachofuata ni kulichukulia hatua shirika au dhehebu husika. Sio kuyachukulia na madhehebu mengine ambayo hayajakiuka taratibu na kuyafutia misamaha kwa kosa la wachache! Ile kauli ya Mkulo kwamba "uamuzi huu wa kufuta baadhi ya misamaha haukufanywa kwa sababu yeye na Rais Kikwete ni waislamu bali uamuzi ulifanywa wakati wakristo ni wengi waliohusika na uamuzi huo". Hivi hapa anataka kueleza nini? Wakristo walio wengi wanaangalia kwa makini mwenendo wa Serikali hii ya Awamu ya Nne!

Hivi watu wengine msipoandika pumba huwa hamjisikii raha??

Serikali kama itabadilisha uamuzi huo itakuwa imechemsha sana, hii misamaha ya kodi ndio chanzo kikubwa cha rushwa.
 
Hivi watu wengine msipoandika pumba huwa hamjisikii raha??

Serikali kama itabadilisha uamuzi huo itakuwa imechemsha sana, hii misamaha ya kodi ndio chanzo kikubwa cha rushwa.

Huna habari kwamba wamegundua kwamba wamechemsha na sasa wamesharudi to their senses? Hongera sana Mkulo, nilishaanza kupoteza imani na wewe.
 
Naipongeza serikali kwa kuona mantiki katika udhaifu wa proposal yake ya kodi kwa huduma za kidini.
Pengine la kupongezwa zaidi ni nguvu ya demokrasia.
Hii si dalili ya udhaifu wa serikali bali uwezo wake wa kujisahihisaha ili kuondoa dalili zote za mparaganyiko kati yake na wadau wake wa karibu katika kuendesha huduma za kijamii.
Ni wazi kuwa serikali imeona umuhimu wa kutowatenga wadau wake katika shughuli za kijamii na maendeleo lakini vile vile serikali inashauriwa kuziba kabisa mianya ya matumizi mabaya ya misamaha ya kodi kwa mashirika ya kidini ili kuondoa mtafaruku uliojitokeza.
Kuna "Maaskofu na Mashekhe" bandia ambao kihalisi ni wafanyabiashar.Hawa watu wabanwe ili kama wanafanya biashar ya kujinufaisha walipe kodi halali ya serikali.
Cha muhimu zaidi ni serikali kuongeza wigo wa maendeleo kwa wa Tz wazalendo ili kodi zaidi iweze kukusanywa.
 
Msingi sio dini. Msingi ni kwamba charitable activities should not be taxed.

Kama Bill Gates akinunua dawa za kuwasaidia waathirika wa ukimwi, basi si akili kumtoza kodi. Kama nikijitolea kujenga makazi ya watoto yatima, hata kama mimi ni Atheist basi si vizuri kutoza gharama zangu kodi.

Ni serikali ndiyo inaandikisha ni kikundi gani ni charitable organization na kipi sio. Kama kuna kikundi kilitumia vibaya msamaha wa kodi, basi hicho ndio kishughulikiwe.

Haingii akililini kwamba serikali haikuzungumza na viongozi wa dini kabla ya kuwabandika kodi. Ni serikali isiyofahamu namna ya kutekeleza azma yake. See, they are now eating their words. Shame on them!
 
Viongozi wa Nchi za Kiafrika baadhi yao si waaminifu na wanapotoka madarakani ndipo wanayaona mabaya. Kwa Tanznaia watazame walio kuwa mawaziri au wabunge zamani kwa sasa ndipo wanayaona makosa! walaaniwe!
 
Next Level,

Hata ikiwa wanatumia vizuri, lakini wajameni taasisi za dini kazi yao ni kueneza neno la Mungu!

Unaweza kusimama mahali na ukahubiri neno la Mungu wakati wahumini wanaumwa na hawana huduma ya matibabu, hata kama ipo hawawezi kuchangia au zipo mbali. Viongozi wa dini wanaelekezwa kuponyesha wahuni kiroho na kimwli, ndiyo maana miskiti inachimba visima, shule nk.. ili wahumini wao wasipate shida mahali walipo.

Hata wamisionari walipokuja walijenga makanisa, shule, hospitali nk.


Kazi zao sio ku-run government parallel to government ya kaisari, haya mambo ya shule na hospital za taasisi za dini in reality ni services za kutolewa na serikali ikiruhusiwa kupokea kodi.

Ndugu yangu nakushangaa wewe umeshazunguka mikoa mingapi ukaangalia hali halisi au ndiyo wale mliozaliwa masaki. shule olimpio, kazi dar...

Ni vigumu kwa serikali ku-run hizi huduma peke yake hata kama hiyo kodi ingerudishwa kwa taasisi hizi. Nchi kubwa hii huduma kwa jamii bado haijafikia kila mtu. Sasa hivi tupo level ya wilaya kuwa na hospitali. Je tutafika lini kuwa hospitali katika level ya tarafa au kijiji??? Huko tarafini au kwenye kata nani tutafikisha lini hospitali? Tujaribu kuangalia hali halisi na sio kulingalisha huduma zipatkanazo wilaya za dar basi na huko mikoani ni hivyo hivyo
 
Hongera kwa serikali kuondoa hofu ya Makanisa na dini, Maana miskiti na makanisa yote yanategemea misaada ya wahisani kutoka nje, Ukiangalia mikoa yote TZ hospitali zote ni za TAASISI ZA DINI , Mfano Kagera kuna hospitali 2 tu za Serikali, Hii serikali inajichanganya yenyewe.

SERIKALI MWENDAWAZIMU chai na vitafunwa bil 19, Safari za nje bil 34.

Je tutafika???

MKULLO AJIHUZULU AMEMDANGANYA RAIS KUFUTA MSAMAHA WA KODI, PINDA AMUONDOE ametuboa.
 
Mimi nasema haikunywea ime FYATA MKIA!

Very shame! Jana nilikuwa nikiangalia kipindi cha Mchungaji Lusekelo chanel 10..ameonesha kusikitishwa mno na kauli za viongozi wa Kanisa aliwaita wachungaji na maaskofu za kuitisha serikali.

In short..serikali yetu iko rehani...Kanisa limeonyesha kwa mara nyingine is big than the Government!

Recalll! when the GOVT said kama limefanya utafiti wa kutosha na kuona kama Tanzania kujiunga na OIC hakuna shida.... Kanisa lilisimama kidete likasema kama litaangalia upya uhusiano wake na CCM! unless li withidraw maamuzi haya. Membe allitwa na Pengo..guess what next! waislamu walisema wee! wakaomba wee hata waonane na Membe lakini..thubutu!

Baada ya Kadhia hii ya misamaha ya Kodi..wakarudia tena karipio lile lile..serikali kwa mara nyingine ikanywea na jana Mh Pinda akatangaza kutengulia uamuzi ule wa misamaha ya kodi.

In short kweli imedhihiri kama Kanisa ni extremely powerful than any one can even dare to imagine.

Kwa faida rejeeni kitabu cha kanisa katoliki na siasa ya Tanganyika cha Padire Sivalon..
Padre akimnukuu Father Robinson
, (the church) is now totally dependent on state aid for the administration of these school. If this aid were withdrwan, the the church will be forced to close its schools'

Leo tunaambiwa kama serikali itatangaza itatoa wapi pesa zitakazo fidia misamaha hii ya kodi kwenye miradi ya Kanisa.

Haya bwana tumenyoosha mikono.
You are indeed powerful na una uwezo wa kuindoa serikali iliyopo madarakani hasa kwa elimu hiyo ya uraia kwa waumini.
 
Uamuzi huu umechukuliwa kisiasa zaidi kuliko kitaalam na kizalendo
 
Back
Top Bottom