Kesi ya kupinga tozo kwa watumiaji wa Daraja la Julius Kambarage Nyerere lililoko Kigamboni imetajwa leo kwa ajili ya maelekezo ya mahakama, huku Serikali ikiomba kuongezewa muda zaidi wa kuwasilisha maelezo ya utetezi wake wa maandishi dhidi ya kesi hiyo.
Kesi hiyo ya Kikatiba namba 20632 ya mwaka 2026, imefunguliwa na wakili wa kujitegemea, Mohamed Majaliwa, katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na wenzake.
Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo ni Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), ambao ndio wamiliki wa barabara nchini; Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Kesi hiyo, inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, Amir Mruma (kiongozi wa jopo), Biswalo Muganga na Suleiman Hassan, ilipotajwa leo Jumatano, Agosti 19, 2026, walalamikiwa wote waliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Edwin Webiro, akisaidiwa na mawakili wa Serikali, Happy Mwakanyamale na Victoria Rugendo.
Webiro ameeleza mahakama hiyo kuwa walipewa nyaraka za kesi hiyo Agosti 12, hivyo tarehe yao ya mwisho ya kuwasilisha maelezo yao ya maandishi kujibu madai hayo ni Agosti 26, 2026.
Hata hivyo, amesema kuwa kwa kuwa shauri hilo linahusisha taasisi nne za Serikali, wanahitaji kupata maelezo yake kabla ya kuwasilisha majibu ya madai hayo.
Soma pia: Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?
Hivyo, amesema wanaomba nyongeza ya muda wa siku tano zaidi, hadi Agosti 31, 2026, chini ya Kanuni ya 19 ya Kanuni za Mashauri ya Kikatiba, sambamba na Kifungu cha 105 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai (CPC).
Wakili Majaliwa, ambaye anajiwakilisha mwenyewe katika kesi hiyo, amesema kuwa kulingana na sababu zilizotolewa na Wakili wa Serikali, hana pingamizi kuongezewa muda huo, na mahakama katika uamuzi wake imeikubalia Serikali.
“Tunakubaliana na maombi yenu na muda unaongezwa kama mlivyoomba. Shauri hili litasikilizwa Septemba 9, 2026 na majibu ya upande wa walalamikiwa yawasilishwe kabla au Agosti 31, 2026,” amesema Jaji Muganga kwa niaba ya jopo la majaji hao.
Katika kesi hiyo, Wakili Majaliwa anaiomba mahakama hiyo itoe amri mbalimbali. Kwanza, itoe tamko kwamba tozo zinazolipwa katika daraja hilo ni batili kwa kuwa ni kinyume cha Katiba, kwa kuwa zinakiuka Ibara za 13(1) na (4), 29(2), 138(1), 143(2)(c) na 26(1).
Pili, mahakama itoe amri ya kusitishwa haraka kwa tozo hizo katika daraja hilo. Tatu, itoe amri ya zuio dhidi ya walalamikiwa wasiendelee kukiuka Katiba kwa kuendelea kutoza tozo hizo. Nne, imuamuru mdaiwa wa nne (CAG) kufanya ukaguzi wa mapato tangu tozo hizo zilipoanza kukusanywa.
Kwa mujibu wa wakili, daraja hilo lililojengwa kuvuka Bahari ya Hindi, katika Manispaa ya Kigamboni, ni mradi wa ubia kati ya NSSF na Serikali kwa uwiano wa asilimia 60 kwa 40.
Ingawa inaelezwa kuwa daraja hilo linamilikiwa kwa ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa muda usiojulikana, watumiaji wamekuwa wakitozwa ada ya matumizi iliyowekwa na wadaiwa, ambayo imekuwa ikikusanywa na NSSF.
Kwa mujibu wa hati ya maombi na kiapo chake, Wakili Majaliwa anadai kuwa NSSF haistahili kuitwa taasisi ya sekta binafsi, kwa kuzingatia uanzishwaji wake na uendeshwaji wake.
Anabainisha kuwa shirika hilo limeanzishwa kwa Sheria ya Bunge na kwamba mwenyekiti wa bodi na mkurugenzi wake mkuu huteuliwa na Rais, huku wajumbe wa bodi wakiteuliwa na waziri.
Anadai kuwa tozo ya daraja hilo inasimamiwa na Sheria ya Tozo za Barabara na Mafuta na kwamba, hivyo, watu wanaotumia daraja hilo, hususan madereva na wamiliki wa magari, hulipa tozo hizo wanaponunua mafuta, hivyo si sahihi kulipa tena tozo hizo darajani hapo.
Hivyo, anadai kuwa walalamikiwa (Serikali) walifanya uamuzi wa kuanzisha na kutoza tozo hizo katika Daraja la Nyerere bila kuwa na mamlaka hayo na kwa kukiuka masharti ya Katiba na sheria husika za nchi.
Anabainisha kuwa kuna madaraja mengi kama hilo, yakiwemo linalounganisha Barabara za Aga Khan na Coco Beach, Dar es Salaam (Daraja la Tanzanite), na Kigongo-Busisi (Daraja la Magufuli), yaliyojengwa kwa fedha za umma.
Analalamika kuwa watumiaji wa Daraja la Nyerere wanatendewa tofauti na watumiaji wa madaraja hayo mengine, kwani watumiaji wa madaraja hayo hawatozwi tozo yoyote, hali ambayo inaweka ubaguzi, kinyume na Katiba na sheria.
Pia anadai kuwa TRA, kupitia Kamishna Mkuu, inawajibika kwa ukusanyaji wa tozo za barabara na mafuta zinazolipwa chini ya sheria hiyo ya Tozo za Barabara na Mafuta na kwamba ndiye anayewajibika kuwateua wakusanya tozo na kuwasimamia.
Hata hivyo, anadai kuwa Kamishna Mkuu wa TRA ameteua maofisa wa NSSF kukusanya tozo katika daraja hilo, wakati akijua au alikuwa na sababu ya kujua kuwa tozo hiyo imeanzishwa bila kuwa na mamlaka na kwa ukiukwaji wa Katiba na sheria husika.
Vilevile, anadai kuwa licha ya kutozwa tozo hizo, CAG ana wajibu wa kikatiba na kisheria kufanya ukaguzi wa malipo hayo, lakini ameshindwa kutekeleza wajibu huo, kwani malipo hayo hayajawahi kukaguliwa.
Via: Mwananchi