Serikali yaondoa tozo 42 kwenye zao la Kahawa

Serikali yaondoa tozo 42 kwenye zao la Kahawa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuondoa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera hadi kufikia tozo 5 ambazo zitakuwa ni jumla ya Sh267 kwa kilo kutoka Sh830 za awali.

Waziri Mkuu ametoa maamuzi hayo kufuatia tume maalum aliyoiunda ili kupitia utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika wa zao hilo mkoani Kagera.

Majaliwa amewaagiza viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia vyama vyao kwa uaminifu na weledi ili view na tija kwa wakulima. Pia, Majaliwa amewata viongozi wa vyama hivyo kuacha tabia ya kukopa pesa benki kwa ajili ya kununua kahawa kwa wakulima.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Jumanne Machi 29, 2022 wakati akiendesha mkutano maalum wa wadau wa zao hilo uliofanyika mkoani Kagera.

Amesema kuanzia sasa mauzo ya kahawa katika mkoa huo yatafanyika kwa njia ya mnada, utakaofanyika katika ngazi ya vyama vya msingi.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema baadhi ya vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaumiza wakulima wa kahawa kwa kuwaongezea tozo zisizokuwa na tija.

Amesema jambo hilo linafanyiwa kazi kwani wakulima wa kahawa mkoani humo wamekuwa wakilia na tozo kubwa zaidi ya 47 na bado wamekuwa wakicheleweshewa malipo.

Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa kugawa miche ya kutosha ya kahawa kwa wakulima ili ilete tija na kuwaongezea kipato.
 
aliwapic

===
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuondoa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera hadi kufikia tozo 5 ambazo zitakuwa ni jumla ya Sh267 kwa kilo kutoka Sh830 za awali.

Waziri Mkuu ametoa maamuzi hayo kufuatia tume maalum aliyoiunda ili kupitia utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika wa zao hilo mkoani Kagera.

Majaliwa amewaagiza viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia vyama vyao kwa uaminifu na weledi ili view na tija kwa wakulima.

Pia, Majaliwa amewata viongozi wa vyama hivyo kuacha tabia ya kukopa pesa benki kwa ajili ya kununua kahawa kwa wakulima.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Jumanne Machi 29, 2022 wakati akiendesha mkutano maalum wa wadau wa zao hilo uliofanyika mkoani Kagera.

Amesema kuanzia sasa mauzo ya kahawa katika mkoa huo yatafanyika kwa njia ya mnada, utakaofanyika katika ngazi ya vyama vya msingi.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema baadhi ya vyama vya ushirika vimekuwa vikiwaumiza wakulima wa kahawa kwa kuwaongezea tozo zisizokuwa na tija.

Amesema jambo hilo linafanyiwa kazi kwani wakulima wa kahawa mkoani humo wamekuwa wakilia na tozo kubwa zaidi ya 47 na bado wamekuwa wakicheleweshewa malipo.

Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa kugawa miche ya kutosha ya kahawa kwa wakulima ili ilete tija na kuwaongezea kipato.

#365Mama anachanja mbuga kuwaletea maendeleo walalahoi wa nchi walio wengi ambao ni wakulima,,
 
Waweke wazi tozo gani zilizobaki kwenye mkulima ili pale anapofanya biashara yake ajue analipa kipi na kipi.

Ndio yale unasikia sasa boda na bajaji kulipa faini 10000, kumbe maneno tuu utekelezaji ndio hafifu
 
Nina mashaka kama zote hizo zilikuwa ni tozo au ni gharama.
Kwa mfano kahawa ikinunuliwa au ikikusanywa kwenye ngazi ya chama cha msingi si lazima yawepo magunia - gharama ya magunia ikaitwa Tozo. Kahawa itasafirishwa kwenda kiwandani kukobolewa- gharama hiyo ikaitwa tozo; mishahara ikaitwa tozo, sdl nayo nadhani iliitwa tozo!
Nakubali kuwa kuna ubadhirifu mkubwa katika vyama vikuu, ila kuita gharama hizo ni tozo sidhani kama ni sahihi
Kitu kingine ambacho Waziru mkuu amesema hakielewi na labda hakubaliani nacho ni out turn ratio. Katika any raw material processing industry hiyo lazima iwepo, Huwezi kuingiza kilo 100 za korosho za maganda kwenye kiwanda cha kukoboa ukategemea kupata kilo 100 korosho safi. labda utategemea kupata kilo 60, Maana yake ndiyo ratio ya 60%. Kwa hiyo unapofikiria bei ya kununulia maganda, wakati wewe unauza iliyokobolewa, lazima hayo uyatilie maanani.
Kwa maoni yangu, gharama hizo hazijaondolewa kwa mkulima, lakini kwa kuwa atauzia kahawa yake kwenye ngazi ya chini kabisa, yule mnunuzi lazima afikirie hayo yote ndipo atoe bei. Gharama zinaweza kupungua kwani mtu binafsi na chombo cha watu wengi, havilingani kwenye gharama.
 
Kabla ya kuondolewa haikutakiwa kupitia kwanza Bungeni kupata kubali?
 
Back
Top Bottom