Serikali yaongeza siku 14 za kukamilisha Usajili wa Laini za Simu

Serikali yaongeza siku 14 za kukamilisha Usajili wa Laini za Simu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeongeza Siku 14 kutoka Januari 31, 2023 iliyopangwa kufungia Mawasiliano ya Laini za Simu mbazo hazijakamilisha usajili wa alama za Vidole na Kitambulisho cha Taifa.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, #NapeNnauye amesema “Ikifika Februari 13, 2023, siku moja kabla ya Siku ya Wapendanao, anga la Mawasiliano liwe Salama, hatutaki zile meseji za 'ile hela tuma kwenye namba hii’, saa 10 jioni kama kuna laini itakuwa haijahakikiwa itakuwa mwisho wa kutumika kwake,".

Waziri Nape ameongeza kuwa hadi sasa kuna jumla ya Laini za Simu 60,739,790 zinazotumika Nchini kote

===============

Serikali imetangaza kuzifungia laini za simu ambazo hazijahakikiwa ifikapo Februari 13, 2023.

Akizungumza leo Januari 24, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mpaka Januari 19, 2023 kuna watumiaji wa simu 60,739, 790 kati ya Watanzania milioni 61.

Amesema :“Utapeli mwingi unaendelea na jambo hili linaongezeka, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) tulichukua hatua za kufanya usajili kwa kutumia alama za vidole na vitambulisho, zoezi hili lilianza Januari 5, 2019 na kufungwa Desemba 2021,”amesema Nape na kuongeza:

“Kila laini iliyokuwa imelengwa kwa wakati ule ilisajiliwa.”

Amesema Februari 13, 2023 kama namba haijahakikiwa basi namba hiyo itazimwa, na kama kuna mtu alisajili namba kwa jina la mtu mwingine basi ajisalimishe kimaandishi iwapo namba hiyo itafanya uhalifu basi atachukuliwa hatua.

“Kama namba haijahakikiwa hiyo namba itazimwa, laini nyingi mtaani watu wametumia vitambulisho vya watu wengine kusajili na zinatumika kufanya utapeli. Laini tunazoenda kuzifungia ni zile zilizosajiliwa kwa uongo, tumelenga kuwaondoa matapeli kwenye mfumo.

“Tumeongeza siku nyingine 14 hivyo ikifika Januari 13, 2023 siku moja kabla ya siku yawapendao, anga la mawasiliano liwe salama, hatutaki zile meseji ‘ile nauli tuma kwenye namba hii’, saa 10 jioni kama kuna laini itakuwa haijahakikiwa itakuwa mwisho wa kutumika kwake,”amesisitiza.

Nape amewataka wananchi ambao hawajahakiki namba zao kufanya hivyo kabla ya Januari 13 kwa kupiga *106# ili kuhakiki namba yako kama imesajiliwa au la!

HABARI LEO
 
Pongezi Kwa serikali ya nani sijui nikikumbuka nitarudi
 
Line 60,739,790, kama nawaona wanaharamu wakihesabu 1,000/- Kwa mwezi kwa line Kwa jina la uzalendo.

Majibu hapo 6tr/- kwa mwezi mjomba!

Kuanzia Jan 25 tusipofanya kweli ajuaye mola.
 
Kwani line zinazotumika kutapeli zinakuwa hazina usajir wa alama za vidole?
Ugumu ni kumpata hata huyo aliyejisajiri kila kitu maana serkali haina resources kihivyo kuwapa polis kuhangaikia kila jambo.
Muhim iwekeze katika ufaham kwa raia kupambana na madhara ya matumizi ya teknolojia.
Ushamba na kutojari vinawaponza wengi. Wengine wanagawa password kama no za simu.
mf. unaibiwaje kwa sms ya tuma humu alafu unataka serkali ikupe majibu! Yan ni kusema serkali igharamikie kutojari
kwako ilihali kuna madawa muhim hata haijapata pesa kuagiza!
Unakuwa tu jinga flan. Bas serkali haiwez adhibu toto lake jinga maana pesa inakuwa humu humu inazunguka kwenye kaya yake.
Tusipoambizana ukweli tutailaumu serkali miaka yote maana aina ya utapeli inabadirika kil siku.
Tupende kujiridhisha kwa kila jambo. Na tuache tamaa za kijinga.
Wizi wa mtandao wa kujadiri ni kama hackers wanaoingilia mifumo ya kipesa!
MLINZI NO 1 WA MALI YAKO NI WEWE!
LIVE RESPONSIBLY!
 
Uhakiki gn tena unatakiwa?

Kwann kila siku Jambo hili haliishi?.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Hawa jamaa hawaeleweki

Kila siku mwisho mwisho

Kikomo kikomo ....

Kila siku watu wanafikishia umri wa kumiliki line za sim sasa wanapos3ma sijui kuna mwisho hawa siwaelewi

Matamko yao yana mikwala mingiii
Tu

Ova
 
Yaani hadi leo bado kuna laini hazijasajiliwa kwa NIDA na zinafanya kazi?!!! , ndio maana utapeli unaendelea
 
Hawa jamaa hawaeleweki

Kila siku mwisho mwisho

Kikomo kikomo ....

Kila siku watu wanafikishia umri wa kumiliki line za sim sasa wanapos3ma sijui kuna mwisho hawa siwaelewi

Matamko yao yana mikwala mingiii
Tu

Ova
Kabisa mkuu,,
Kila siku line zinahakikiwa halafu mbaya Zaidi uhakiki sio bure unalipa pesa..

Sasa mtu yupo nje ya inchi umwambiye aje ahakiki line.
Hivi ni utaratibu wa wapi?
Usajili na uhakiki tofauti yake nn?

Wao wanapaswa wawe active ktk uhalifu wa mitandaoni,,

Yote hayo ni sababu wanashindwa kuwadhibiti wezi wa mitandaoni.,
Wanatuletea usumbufu raia wema.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom