Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Waziri wa fedha, Balozi Khamis Mussa Omar akiwasilisha hotuba ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027 amesema .....
Kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini kutoka asilimia 15 hadi asilimia 20 kwa magari yenye umri wa miaka nane lakini hayazidi miaka 10 na kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40 kwa magari yenye umri wa zaidi ya miaka kumi lakini hayazidi miaka 20.
Aidha, magari yenye miaka inayozidi 20 na kuendelea yatatozwa ushuru wa bidha kwa kiwango cha asilimia 50. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali pamoja na kupunguza uingizaji wa magari husika ambayo kwakiasi kikubwa yanasababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na uwepo wa taka ngumu ambazo hutumia gharama kubwa katika kuziteketeza.
Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 106.70.