Serikali yaongeza ushuru kwenye magari ili kuongeza mapato na kupunguza uchafuzi wa mazingira

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Waziri wa fedha, Balozi Khamis Mussa Omar akiwasilisha hotuba ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027 amesema .....

Your browser is not able to display this video.
Kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini kutoka asilimia 15 hadi asilimia 20 kwa magari yenye umri wa miaka nane lakini hayazidi miaka 10 na kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40 kwa magari yenye umri wa zaidi ya miaka kumi lakini hayazidi miaka 20.

Aidha, magari yenye miaka inayozidi 20 na kuendelea yatatozwa ushuru wa bidha kwa kiwango cha asilimia 50. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali pamoja na kupunguza uingizaji wa magari husika ambayo kwakiasi kikubwa yanasababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na uwepo wa taka ngumu ambazo hutumia gharama kubwa katika kuziteketeza.

Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 106.70.
 
Hongera sana Serikali na TRA kwa maamuzi haya ya kimkakati. Kwanza kabisa, wananchi hatutaki magari. Hayo ni mambo madogo sana. Kipaumbele chetu kikubwa ni kulipa kodi nyingi zaidi kadri inavyowezekana ili watu muhimu kama Abdul na Kizigha waweze kununua Bugatti mpya, kuongeza magari ya kifahari kwenye misafara yao na kujenga majumba makubwa zaidi. Huo ndio uzalendo wa kweli unaotakiwa katika taifa letu.


Kwa kweli hatua ya kuongeza ushuru wa magari yaliyotumika ni ya kupongezwa sana. Kwa nini mtu aagize gari la miaka 8 au 10 kwa bei nafuu wakati anaweza kununua gari hilohilo hapa nchini kwa bei iliyopandishwa mara mbili au tatu? Hapo fedha zitabaki ndani ya nchi, zizunguke kwa walewale, na sisi wengine tuendelee kushangilia ukuaji wa uchumi kupitia taarifa za takwimu. Maisha ya kumiliki gari binafsi yamekuwa mepesi sana kwa wananchi, hivyo ni sahihi sasa yawe magumu kidogo ili tujifunze nidhamu ya kiuchumi.
 
TRA nawashauri wasisimame hapo. Wakaze zaidi. Bado kuna watu wanafanikiwa kuagiza magari, jambo linaloonyesha wazi kuwa ushuru bado ni mdogo. Ikiwezekana magari ya zaidi ya miaka 10 yatozwe ushuru unaozidi thamani ya gari lenyewe mara kadhaa. Mwananchi akifikia hatua ya kuona ni bora aende kwa daladala kuliko kufikiria kuagiza gari, hapo tutajua sera zimefanikiwa kikamilifu.


Na wale wanaolalamika kuhusu gharama kubwa za magari waache kulia. Kazi ya mwananchi si kumiliki mali; kazi ya mwananchi ni kuchangia mapato ya Serikali. Mambo ya magari, Bugatti, majumba ya kifahari na starehe nyingine kubwa tuwaachie kina Mafwele, Kizigha na kina Lugum, sisi wengine tuendelee kulipa kodi kwa furaha na upendo huku tukishukuru kwa kila ongezeko jipya, maana inaonekana bado akili zetu hazijakaa sawa vya kutosha.
 
KODI+MIKOPO+MISAADA ...
 
Yaan bongo kumiliki gar ni kama jinai kbs! Ni kama viongozi hawataki hata raia wa kawaida wamiliki magari 😥😥😥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…