Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Awali, Mwanachama huyo alisema kulikuwa na Kampeni ya Ng’arisha Katavi Tunza Mazingira iliyolenga kupanda miti Milioni 10 ambapo ilizinduliwa 24/01/2023 hadi 26/10/2023 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko kwa lengo kuhamasisha utunzaji wa mazingira, lakini miti yote iliyopandwa Milala ilikufa na hakukuwa na ufuatiliaji.
Zoezi likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph limefanyika Desemba 28, 2024 kwa kupandwa miti zaidi ya 1,500 katika eneo la Bwawa la Milala Manispaa ya Mpanda ili kufikia lengo la kupandwa miti Milioni 1.
MKUU WA WILAYA AZUNGUMZA
Akizungumza na JamiiForums na kuelezea kilichofanyika, Mkuu wa Wilaya, Jamila Yusuph anasema:
Upandaji miti ni zoezi endelevu, pia kupanda miti na kisha kunayuka au kufa ni jambo la kawaida lakini safari hii kuna utofauti na ilivyokuwa awali.
Zoezi la sasa limefanyika Desemba 27, 2024, tumepanda miti zaidi ya 1,500.
Kipindi kile wakati miti ilivyopandwa kulikuwa na shughuli za Watu zinaendelea kutokana na baadhi yao kuwa wanaishi maeneo hayo ya karibu na Bwawa, walikuwa hawajalipwa fidia lakini safari hii hawapo na kuna mikakati tumeweka ya kusimamia kuanzia ngazi ya Serikali za Mitaa.
Zoezi lilishirikisha pia Timu ya Usalama, Wanahabari na Viongozi wa Mitaa.”
Pia soma ~ Kampeni ya 'Ng’arisha Katavi Tunza Mazingira' iliyoanzia katika Bwawa la Milala, imeishia wapi?