Serikali yapiga hatua kubwa kutatua migogoro ya Ardhi na kuboresha Huduma

Serikali yapiga hatua kubwa kutatua migogoro ya Ardhi na kuboresha Huduma

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
IMG-20260428-WA0103.jpg

Dodoma, Tanzania

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuandika historia mpya katika sekta ya ardhi kwa kuhakikisha migogoro ya muda mrefu inapatiwa suluhu ya kudumu na huduma kwa wananchi zinaboreshwa kupitia teknolojia ya kisasa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya katika mahojiano na Clouds FM jijini Dodoma,

Mhe. Mmuya alibainisha kuwa serikali inafanya kazi kwa karibu na wananchi ili kuleta tabasamu na kuimarisha uchumi wa taifa kupitia matumizi bora ya ardhi kwa kuhakikisha ardhi yote nchini inaendelea Kupimwa, Kupangwa na Kumilikisha

Aidha, Naibu Waziri huyo amesisitiza dhamira ya serikali ya kutatua migogoro ya ardhi na kuboresha huduma kupitia mfumo wa e-Ardhi.

Katika hatua nyingine Mhe. Mmuya amemshukuru Rais Samia kwa kumteua Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye amekuwa akisisitiza viongozi kuwafikia wananchi moja kwa moja akitolea mfano wa ziara za kikazi ambapo viongozi husikiliza kero za wananchi kuanzia asubuhi hadi usiku ili kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake.

Kwa Upande Mwingine Mhe. Mmuya amesema kuwa Ili kuondoa urasimu na migogoro ya hati miliki, serikali imeimarisha matumizi ya mfumo wa e-Ardhi. Mfumo huu unasaidia wananchi kupata huduma za ardhi kwa haraka na kupunguza uwezekano wa kiwanja kimoja kuwa na hati mbili.l (Double allocation).

Hatua hizi za Wizara ya Ardhi ni kielelezo tosha cha Uongozi Bora unaolenga kumsaidia mwananchi wa kawaida. Kwa kuboresha mipango ya matumizi ya ardhi katika sekta za viwanda, maji, kilimo, na nishati, serikali inatengeneza mazingira rafiki kwa maendeleo ya taifa zima
IMG-20260428-WA0097.jpg
 
Nna taarifa nyingi za watu kudhulumiwa maeneo kibabe watu wenu huku chini ni wajeuri kutendea kazi na wanazidi kuleta migogoro kila uchao.

Haki za watu maskini zimegeuzwa dili.

Ipo siku hawa Wenye viti sijui watendaji mtakuta watu wamewagawana.
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Inakuwaje unaweka hapa taarifa rasmi za mamlaka na serikali wakati huu mtanda umefungiwa na mamlaka kama hii kwa baraka za serikali...!!??
 
Wakati wa uwaziri wa Lukuvi nilijua kaimaliza migpgoro yote nchini maana si kwa headlines zile kila siku.

Alipoingia Jerry Silaa ikawa kama hiyo wizara haijawahi kuwa na waziri maana na yeye kila siku anazungumzia kutatua migogoro iliyodumu miaka 30,20,40 na clinic zisizoisha!!

NB:Wanasiasa wanashughulika na matokea badala ya vyanzo vya hiyo migogoro hivyo haiwezi kuisha.
 
Hivi yule Tapeli wa viwanja na Boss wa Tamasha la Pasaka mliishia wapi pamoja na kumuwekea dau?
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuandika historia mpya katika sekta ya ardhi kwa kuhakikisha migogoro ya muda mrefu inapatiwa suluhu ya kudumu na huduma kwa wananchi zinaboreshwa kupitia teknolojia ya kisasa.
Ukienda kufuatilia ndo utajua kama hii ni kweli au propaganda as usual
 
Back
Top Bottom