Serikali yapiga imesitisha usajili mpya wa Bajaji mbeya yadai zipo nyingi sana

Serikali yapiga imesitisha usajili mpya wa Bajaji mbeya yadai zipo nyingi sana

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Serikali imesitisha usajili wa bajaji mpya katika Jiji la Mbeya, huku bajaji zaidi ya 6,000 zilizopo zikiruhusiwa kuendelea kutumia barabara kuu kwa siku 14 wakati tathmini ya changamoto za miundombinu ikiendelea.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, amesema ameunda timu maalumu yenye wawakilishi wa wadau mbalimbali wa usafiri na usafirishaji ili kuchunguza hali ya barabara na kubaini maeneo yanayohitaji ukarabati.

Amesema timu hiyo itakuwa na siku 14 za kutathmini miundombinu na kupendekeza maboresho yatakayowezesha barabara kuwa rafiki kwa bajaji zinazofanya shughuli za usafiri jijini humo.Kutokana na hatua hiyo, Profesa Shemdoe amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Justice Kijazi, kusitisha mara moja usajili wa bajaji mpya, akieleza kuwa idadi iliyopo imezidi 6,000 na miundombinu ya sasa imezidiwa.

Ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Mkoa wa Mbeya na viongozi wa vyama vya siasa, ikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili waendesha bajaji.

Chanzo : Jambo tv


 
Back
Top Bottom