Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUINGIZA MALIGHAFI YA CHUMVI KUTOKA NJE KWA VIWANDA VYA NDANI
"Mkakati wa Serikali kuvutia wawekezaji katika sekta ya Chumvi unaendelea ikiwa ni pamoja na kutenga eneo lenye ukubwa wa Hekari 168 katika Wilaya ya Kilwa kwaajili ya wawekezaji Wenye nia ya kuchakata Madini ya Chumvi. Serikali imeendelea kutoa vivutio mbalimbali vya kikodi na visivyo vya kikodi kwa Uratibu wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na taasisi husika ili kufanikisha adhma ya kuwekeza katika Sekta ya Madini" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara
"Biashara ya wazalishaji wa Chumvi katika Mkoa wa Lindi imekuwa ikiathiriwa na waagizaji wa Chumvi kutoka nje ya nchi. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo waweze kufanya biashara ya Chumvi kwa ufanisi?" - Mhe. Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini
"Je, Serikali haioni sasa wakati umefika wa kuweza kuwa na bei elekezi kwa zao la Madini ya Chumvi kwa Mkoa wa Lindi ili kuhakikisha wafanyabiashara wa Chumvi katika Mkoa wa Lindi wananufaika na Biashara" - Mhe. Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini
"Ni kweli kumekuwa na changamoto katika sekta ya Chumvi kwa maana baadhi ya viwanda kuagiza Malighafi ya Chumvi kutoka Nje ya nchi badala ya kuchukua Chumvi inayozalishwa hapa nchini. Tumeshatoa maagizo na ni agizo la Serikali kuwa Wenye viwanda wote wanaozalisha Chumvi watumie Chumvi inayozalishwa nchini. Tulishatoa marufuku kuagiza Chumvi kutoka Nje ya nchi kwaajili ya viwanda vya ndani" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara
"Biashara zinatakiwa ziende kwa Uhuru (Supply and Demand) lakini inapotokea hoja mahususi kwenye Sekta muhimu tutaangalia ikiwa kuna ulazima wa kuweka bei elekezi kwaajili ya kuona watanzania na wanaozalisha Chumvi waweze kupata bei nzuri inayouzwa kwenye viwanda vya Tanzania" - Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.