Serikali yapiga marufuku kushikilia ID za watu.....Murkomen asema ni kosa la jinai

Serikali yapiga marufuku kushikilia ID za watu.....Murkomen asema ni kosa la jinai

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Interior CS Kipchumba Murkomen ameibuka na agizo kali: hakuna mtu au taasisi inaruhusiwa kushikilia kitambulisho cha mwingine.

Amesema wazi ID si dhamana. Si collateral. Si kitu ya kushikilia mtu mpaka alipe deni.

KILE KINAENDEA GROUND
Kwa muda sasa, hii tabia imekuwa kawaida sana Kenya:
  • Shylocks wanachukua ID kama security ya loan
  • Hospitali zinashikilia ID ukikosa kulipa bill
  • Clubs na biashara zingine zinadai ID kama deposit
Murkomen anasema hii yote ni illegal na inakiuka haki za wananchi.

SHERIA INASEMAJE?
Chini ya Registration of Persons Act:Kila Mkenya lazima awe na ID kuanzia miaka 18
  • Ni kosa kushikilia au kutumia ID ya mtu mwingine vibaya
  • Ukipatikana na hatia – fines au hata kifungo
Kwa kifupi: Hakuna excuse ya kushikilia ID ya mtu.

ATHARI KWA MWANACHI
Watu wengi wamekuwa stranded juu ya hii mambo ya ID kushikiliwa:
  • Huwezi apply kazi bila ID
  • Huwezi access huduma za serikali
  • Huwezi register kama voter
Na sasa tukielekea uchaguzi wa 2027, hii issue imekuwa big deal sana.

Serikali Inasema nini next?
Murkomen ameagiza:
  • IDs zote ziachiliwe mara moja
  • Wenye wanakataa waripotiwe polisi
  • Wananchi wajue haki zao
Pia kuna push ya kuboresha mfumo wa usajili ili IDs zipatikane kwa urahisi zaidi.
PRINTED-NATIONAL-ids.jpg

================= For English Audience =================
​
Interior CS Kipchumba Murkomen says that national ID cards are not legal tender and cannot be used in exchange for goods and services. He has directed extortionist moneylenders and others holding another person's ID as security for payment to return the documents immediately or face prosecution.​

SOURCE: KENYAN TIMES​
 
Back
Top Bottom