Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,149
- 6,994
Serikali umepiga marufuku masomo ya ziada kwa shule za Serikali na hasa wakati wa likizo, kwa kubainisha kuwa yanaongeza gharama zisizo za lazima kwa wazazi na ni kinyume na waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016,ambao unataka wanafunzi wapate likizo ama muda wa kupumzika.
Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa Mbuge wa Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza aliyetaka ufafanuzi wa waraka uliotolewa na kamishina kutoka wizara ya Elimu uliotaka shule zote zifungwe wakati wa likizo.
Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya shule za Serikali zinazalazimisha wanafunzi na wazazi kuchangia gharama kwa kipindi chote cha likizo ambacho wao wanatumia kufundishwa.