Serikali yapiga marufuku masomo ya ziada

Serikali yapiga marufuku masomo ya ziada

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
13,149
Reaction score
6,994
Serikali umepiga marufuku masomo ya ziada kwa shule za Serikali na hasa wakati wa likizo, kwa kubainisha kuwa yanaongeza gharama zisizo za lazima kwa wazazi na ni kinyume na waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016,ambao unataka wanafunzi wapate likizo ama muda wa kupumzika.

Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa Mbuge wa Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza aliyetaka ufafanuzi wa waraka uliotolewa na kamishina kutoka wizara ya Elimu uliotaka shule zote zifungwe wakati wa likizo.

Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya shule za Serikali zinazalazimisha wanafunzi na wazazi kuchangia gharama kwa kipindi chote cha likizo ambacho wao wanatumia kufundishwa.
 
Tatizo ni likizo, gharama, waraka wa kamishna, au vyote kwa pamoja? Kama ni suala la likizo, mbona private schools hawahusiki? Kama ni suala la gharama, linawahusuje serikali, maana pesa hutoka kwa wazazi na walezi na wahisani na wafadhili wa wanafunzi? Kama ni suala la waraka wa kamishna, mbona itakuwa haina tija na usawa? Kama ni vyote hivi vitatu kwa pamoja mbona hakuna uwiano wa kimantiki?
 
Hii itumike hata private school, zifungweee maana ni kukaririsha tu wanafunzi na pesa tu.

Haya mambo yapo scientifically, ajabu watu wanapiga mwisho matoto yanakua mazezeta mbele.

Watoto waachwewa relax na kutumia kile halisi kilichobaki kichwani na wawapime KWA hilo.

Afu private school wanawachimba mabiti sana wazazi KWA hili.

Waziri kazia hapo watoto wapumzike
 
Tatizo ni likizo, gharama, waraka wa kamishna, au vyote kwa pamoja!??? Kama ni suala la likizo, mbona private schools hawahusiki!???
Wazazi wanapata gharama kubwa ya kulipia,bado hela ya usafiri,dalala,bodaboda,na wazazi wengine wanakuwa na watoto zaidi ya mmoja, kwa mfano anakuwa na mtoto wa darasa la nne,mtoto wa darasa la saba, mtoto wa kulea, aliyefiwa na mzazi wake, ambaye ni ndugu, wa kidato cha pili na wa kidato cha nne, wote hao,wanatakiwa walipiwe.Kuna shule zinatoza mpaka elfu kumi kwa mwezi,huo ni mzigo mkubwa kwa mlezi au mzazi.

Waalimu wanalazimisha, kwa hiyo kwa wasio na uwezo, wa kulipiwa, wanapitwa kimasomo na wenzao wenye uwezo wa kulipiwa,hii inakuwa kama kuna ubaguzi kimasomo.
 
Hii itumike hata private school, zifungweee maana ni kukaririsha tu wanafunzi na pesa tu.

Haya mambo yapo scientifically, ajabu watu wanapiga mwisho matoto yanakua mazezeta mbele.

Watoto waachwewa relax na kutumia kile halisi kilichobaki kichwani na wawapime KWA hilo.

Afu private school wanawachimba mabiti sana wazazi KWA hili.

Waziri kazia hapo watoto wapumzike
Hakika uliyosema.
 
Wazazi wanapata gharama kubwa ya kulipia,bado hela ya usafiri,dalala,bodaboda,na wazazi wengine wanakuwa na watoto zaidi ya mmoja, kwa mfano anakuwa na mtoto wa darasa la nne,mtoto wa darasa la saba, mtoto wa kulea, aliyefiwa na mzazi wake, ambaye ni ndugu, wa kidato cha pili na wa kidato cha nne, wote hao,wanatakiwa walipiwe.Kuna shule zinatoza mpaka elfu kumi kwa mwezi,huo ni mzigo mkubwa kwa mlezi au mzazi.

Waalimu wanalazimisha, kwa hiyo kwa wasio na uwezo, wa kulipiwa, wanapitwa kimasomo na wenzao wenye uwezo wa kulipiwa,hii inakuwa kama kuna ubaguzi kimasomo.
Elimu ni gharama; wazazi washauriwe wazae watoto wanaoweza kumudu kuwalisha, kuwalea na kuwasomesha. Lazima tujiulize kama taifa, hivi tunataka watoto wetu wapate elimu au mwanga? Ukweli ni kwamba suala la elimu lisingepaswa kufanyiwa negotiations.

Vinginevyo, shule za serikali ziboreshwe kuanzia miundombinu, mazingira, walimu, mitaala, nk ili kuhakikisha kwamba mwanafunzi anapokuwa shule, kweli anapata masomo makini na ya kutosha yanayowiana na muda anaokaa ama kwenda shule, kiasi kwamba hatahitaji tena masomo ya ziada.
 
Elimu ni gharama; wazazi washauriwe wazae watoto wanaoweza kumudu kuwalisha, kuwalea na kuwasomesha. Lazima tujiulize kama taifa, hivi tunataka watoto wetu wapate elimu au mwanga!??? Ukweli ni kwamba suala la elimu lisingepaswa kufanyiwa negotiations. Vinginevyo, shule za serikali ziboreshwe kuanzia miundombinu, mazingira, walimu, mitaala, nk ili kuhakikisha kwamba mwanafunzi anapokuwa shule, kweli anapata masomo makini na ya kutosha yanayowiana na muda anaokaa ama kwenda shule, kiasi kwamba hatahitaji tena masomo ya ziada.
Hili Neno!
 
Waje vijijini huku. Graduates wa DIPLOMA na DEGREE za EDUCATION ni wengi sana waalimu walioajiriwa wengi wamejiajiri kwenye TUITION hadi la kwanza wapo shuleni wanasoma TUITION wakati wa likizo. Form one hadi form 4 ada ya tuition hadi buku jero wanasoma hadi usiku aseeeee.
 
Mimi naunga mkono hoja na sio shule za serikali tu wanafunzi wakipata likizo basi iwe likizo kwa maana wapate muda wa enjoy sio likizo baado homework utasema nyumba ndio imekuwa shule hata watoto kufurahia likizo hakuna unaona bora hata shule.

Kuna nchi ambazo ziko number one kielimu duniani kama Finland ni marufuku kitu kinaitwa homework wanataka watoto wasome lakini pia wanataka watoto waishi kama watoto kwa kuamini muda wa utotoni ni gift na wanahitaji enjoyment sababu muda unapita lakini mashuleni Finland ni top. Waziri angepiga marufuku aina yoyote ya homework wakati wa likizo.
 
Private schools watoto wanaenda kufanya revision na kucheza tu. Hakuna kipya cha maana isipokuwa Shule kukamua pesa kwa wazazi. Je ni mwanafunzi gani anaweza kusoma mwaka mzima bila kupumzika
 
Tatzo serikali inasema tu ila haifatilii ilichokiagiza.Kwa sasa DEOs ndo wanaamua shule zifungwe au zisifungwe hasa kwa madarasa ya mitihani.
 
Mimi naunga mkono hoja na sio shule za serikali tu wanafunzi wakipata likizo basi iwe likizo kwa maana wapate muda wa enjoy sio likizo baado homework utasema nyumba ndio imekuwa shule hata watoto kufurahia likizo hakuna unaona bora hata shule. Kuna nchi ambazo ziko number one kielimu duniani kama Finland ni marufuku kitu kinaitwa homework wanataka watoto wasome lakini pia wanataka watoto waishi kama watoto kwa kuamini muda wa utotoni ni gift na wanahitaji enjoyment sababu muda unapita lakini mashuleni Finland ni top. Waziri angepiga marufuku aina yoyote ya homework wakati wa likizo.
Huko Finland (Nchi ya Mapezi), ukifundishwa na mwalimu mmoja kwa nusu saa, ubora unazidi hapa kwetu ukifundishwa na walimu ^war-tar-know^ kutwa nzima au hata ^we-key^ moja. Nachelea kusema kwamba mshabihiano huu ni almost sawa na kulinganisha Ferdausi na Jehanamu. Tofauti kabisa!!!
 
Likizo ni muhimu mazee! Hasa kumfanya wanafunzi apate kujifunza maisha halisi ya mtaani, kama kufanya kazi ndogondogo zinazompatia kipato(wanafunzi wengi wameweza kujihudumia kwa njia hii), kucheza, kuwatembelea ndugu, n.k
Wanafunzi si roboti, na shule sio programming lab pekee.
Mnaotetea haki za watoto mpo?
 
Serikali umepiga marufuku masomo ya ziada kwa shule za Serikali na hasa wakati wa likizo,kwa kubainisha kuwa yanaongeza gharama zisizo za lazima kwa wazazi na ni kinyume na waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016,ambao unataka wanafunzi wapate likizo ama muda wa kupumzika.

Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa Mbuge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza aliyetaka ufafanuzi wa waraka uliotolewa na kamishina kutoka wizara ya Elimu uliotaka shule zote zifungwe wakati wa likizo.

Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya shule za Serikali zinazalazimisha wanafunzi na wazazi kuchangia gharama kwa kipindi chote cha likizo ambacho wao wanatumia kufundishwa.
Naunga mkono hoja
 
Serikali inajifanya kama inawahurumia sana wazazi, ila mimi naona ni baadhi ya viongozi wao watoto wao wanasoma international Schools, katazo hili la masomo ya ziada haliwahusu, zipo shule zinazo somwa na watoto wa walala hoi ili wazidi kudidimia kielimu, international Schools(walipo watoto wao)watazidi kupeta tu na kuja kufaulu vizuri.
Sasa kama ni kweli serikali inawaonea huruma wazazi, kwanini wanawalipisha wazazi wajawazito ada ya kujifungua sh 80,000 na operesheni ya uzazi 300,000?
 
Back
Top Bottom