Serikali yapiga marufuku mazao ya uhandisijeni(GMOs) nchini


Let me ask you this, which one you would rather choose, Saving the World or Destroying it?

You really typing BS you know? have you imagined how it will be if we depend on these seeds rather than what the nature has to offer? and let me ask you one thing, why GMO and not natural ones? give me a good reason if you make sense
 
All said, all written and all researched, ni ukweli kwamba matumizi ya mbegu za aina hii ya GMO, ndiyo mwanzo wa kuua kilimo asilia na mwanzo mpya wa UKOLONI MAMBO LEO katika KILIMO. Ukisha ingizwa kwenye ukoloni mambo leo katika kilimo chako unadhani ni nini kitafuata, kama siyo kuwa TEGEMEZI KWA WAKOLONI katika mahitaji yako yote ikiwa ni pamoja na CHAKULA? Ukitegemea hata chakula kutoka kwa mtu mwingine, basi ujue wewe na familia yako MMEKWISHA! Ndicho wanachotaka kutufanyia hawa WAKOLONI kwa kutumia mlango wa sayansi na teknolojia na utafiti uchwara through watafiti na "wasomi" wachache wenye uchu wa fedha na "njaa kali". Hii hoja ilikwisha kataliwa na serikali miaka mingi na ikasahaurika, mara ghafla inazushwa na hawa "wasomi na watafiti uchwara" kwa kushirikiana wabunge na viongozi wachache kwa maslahi yao wenyewe.

Hiyo hoja ya kuwa wabunge walishangilia si hoja, jiulize na fanya utafiti kidogo, utaona composition ya hao wabunge walioshangilia na kupiga makofi on this GMO issue. Kwa kweli ni WALE WALE TU! Kwa ufupi, matumizi na utegemezi wa hizi mbegu zinazotokana na GMO teknolojia, ndiyo mwanzo wa kufa kwa njaa kwani wenye mbegu zao wanaweza kuamua wasikuuzie aidha hizo mbegu au hiyo teknolojia! Under such a SITUATION, UNAFANYAJE KUTOKA? Nimalizie kwa kusema kuwa uamuzi huu wa Serikali hii ni wa ujasiri na wenye lengo la kuinusuru nchi yetu na hili JANGA LA UKOLONI MAMBO LEO NA NJAA YA KUDUMU. Mbinu hizo ZISHINDWE NA MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
labda tafsiri ya gmo watu hwajailelewa vizuri , mbegu organic ni zile za kienyeji tuu. Hizi zote zinazozalishwa na zilizopo madukani na tunazohamasishwa tulime kisasa na nyingi zipo kwa majina ya F.1 zote ni geneticaly modfined ( G.M.O) I stand to be corrected
 
Unaweza kuwa sahihi kidogo, lakini hizi za GENETICALLY MODIFIED ORGANISMS AU GMO ni kama jina lilivyo ni mbegu zinazotokana na ufundi wa kitaalamu na kimaabra kisayansi zaidi kutokana na "genes" mbalimbali kisayansi na kisha zinakuwa "modified" kadri wapendavyo hao wataalamu ili to fit their needs and requirements. Wanaweza kuchukua genes za kuku na kuzi modify wapendavyo na kutoa kuku "mwenye ubora zaidi"! Lakini wewe uliye mnunua huyo modified kuku huwezi kumuendeleza zaidi ya labda kumla tu, kwani huwezi kupata muendelezo wa huyo "kuku mwenye bora zaidi" bila kununua hiyo GMO ya huyo kuku kutoka kwao! Hayo ndiyo mambo ya GMO! Yanafanyika hivyo hadi kwenye mazoa! Hapa ndipo utegemezi na hatari inapo anzia.

Hizi za madukani ni nzuri sana ndizo hizo wanataka kuziondoa katika maisha na kilimo chetu. Kwa mfano mbegu zote zinazouzwa madukani zimezalishwa kutokana na utafiti wa kawaida tu , siyo wa kutumia GENES na kisha kuzi MODIFY, mbegu hizi ni zile zile zetu za miaka yote ila sasa zinaboreshwa kisayansi bila kutumia genes. Kwa mfano mahindi yanayotoa magunia 40 au zaidi kwa ekari ni yale yale ya miaka yote ila yamefanyiwa UTAFITI na kuboresha uzaaji wake. Hiyo ni kweli pia kwa mazao yote kama matikiti maji, mapapai n.k. Mbegu za GMO zitatufanya tuwe tegemezi kwa wenye mbegu zao na hivyo kutuingiza kwenye utegemezi hatarishi. Kongole kwa Serikali yetu kwa uamuzi huu wa ujasiri wa kupiga marufuku utafiti wake. Hongera sana Wizara ya Kilimo kwa kutunusuru na janga hilo.
 
Binafsi siukubali uhandisijeni. Nawapongeza wanasayansi wanaosimama kupinga uhandisijeni.

Uhandisijeni unaweza kuwa part and parcel ya conspiracy theory ye new world order...kwa maana kwamba watu wanatumia sayansi kwa malengo yao mabaya, hasa ktk kutaka kuitawala dunia kiuchumi na kisiasa, na kikubwa wao wanaona dunia imezidiwa na wingi wa watu hivyo kuna nia ya kupunguza idadi ya watu. Ni kama ilivyo kwa UKIMWI, EBOLA, SARS, saratani...ILA kubwa ni mabeberu kuuteka uchumi wa dunia kwa kumfanya mtu wa tabaka la chini kuwa mtumwa wa watu wa tabaka la juu.

Nashukuru serikali kufutilia mbali GMOs, warudi kwenye sheria na kurudisha kipengele cha awali kinachomtaka mtu aliyeingiza au kuleta GMOs kuwajibika kwa athari zote zitakazojitokeza.
 
We kamtu mbona umejaa pumba kiasi hicho? Watu wanazungumzia sayansi wewe unaleta siasa na mambo ya kusema wengine, wengine... Wengine wanatuhusu nini? Ukiletewa GMO unadhani umependwa? Mbona mambo tunayohitaji hayaletwi kwa mshawasha kama hiyo GMO.

Kuna mtu pale Mwenge kakazana saana akiamini yeye gwiji wa sayansi, swa lakini hatuihitaji sasa hivi. Utapewa sifa na pesa kibao za utafiti lakini ibaki huko huko! Hatuhitaji promosheni na kampeni za GMO.
 
Unayoitaja kwamba ni serikali, ni watalaamu wanaodhani wanatufundisha ujanja wa GMO. Tamaa ya pesa kujikimu kama ilivyokuwa tawala za nyuma, inawafanya baadhi yao vichwa vichemke.

Jamaa wanahangaika kupitia kila njia. Akila Bill Gates wanajidai kuja na kusifu watu ili tutamani kufanya wanayotaka. Wanaojiita wanasayansi wanafanya kama ya wale waliowasaidia wazungu ktk biashara ya utumwa. Wanajua upuunzi ndani ya GMO lakini hawajali kwa kuwa tu, wanapewa pesa za kununua VX.
 

Hivi do you know utofauti kati ya GMO ukiliganisha na madawa ya kupulizia mimea ili kuikinga dhidi ya wadudu waharibifu - hill LA kwanza.

La pili: Nchi zipi za Ulaya au Majimbo ya Marekani ulizo wahi kutembelea, ukabahatika kuingia kwenye aidha Super,Hypermarket au soko la kawaida ukakuta shelves za vyakula zimejazwa vyakula vya GMO?

Unayo yasema hapa yana ukweli gani? Au tuseme yanarandana vipi na masuala ya GMO?
 

Well said mkuu,jamaa hawa nilikwisha washtukia siku nyingi - wala sitashangaa kama hizi mbegu wanapewa na Monsanto halafu wanazuga Watanzania kwamba wamefanya tafiti wao!!

Yaani shinikizo lililokuwa linatumiwa na baadhi ya wabunge kupigia debe mbegu za GMO halikuwa la kawaida hata kidogo - miaka kama minne/mitano iliyo pita niliwahi kuzungumzia kwa kirefu kuhusu ubaya wa kula Frankstein food (GMO),kwa bahati mbaya bandiko langu lilidumu kwa siku moja tu baadae likaondolewa fasta, nafikiri walifabya hivyo kutokana na shinikizo la watu wanao pigia debe GMO nk - kumbuka Kampuni hizo zina fedha lukuki consequently are capable of doing anything under the SUN mradi malengo yao yanafikiwe

Mataifa mengi ya Dunia ya tatu Govt officials wanaongwa na jamaa hawa ili washinikize Serikali zao - kama huna Uzalendo unaweza kujikuta unawaingiza Watanzania wenzako kwenye matatizo ya kiafya pamoja na utegemezi wa mbegu zinazo zalishwa na makampuni ya kibepari, mbegu za asili zinakuwa cross pollinated na za GMO kwa njia ya pollen kupeperushwa na upepo, mwisho was siku mbegu asili zinakuwa extinct - watu wengi hawajui tu, mambo haya ni hatari sana sio ya kuchukuliwa poa hata kidogo. Mbinu za Bill Gates na wenzake zinajulikana zipo mpaka kwenye chanjo....
 
Awali ya yote, nipende kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa usikivu wake na kuchukua hatua stahiki kuhusiana na sakata la mimea na mbegu Zilizobadilishwa Vinasaba (GMO) nchini. Kama mtafiti wa Uhuru wa Chakula, napenda kuihakikishia Serikali kuwa, wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, walaji, wazalishaji wa mbegu wa ndani, watafiti katika taasisi zetu za Kilimo (mbali na wale waliokuwa wakinufaika na mradi wa WEMA), na wauzaji wa vyakula nje na ndani ya nchi wamefarijika sana na hatua hii. Namshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, lakini pia natambua suala hili ni la kisera hivyo kwa namna yeyote linamhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Natoa pongezi za dhati kabisa kwa Serikali, na katika makala hii fupi nitaeleza kwa nini uamuzi huu ni wa kupongezwa.
 

Attachments

  • GMO.jpg
    9.3 KB · Views: 32
SERIKALI YA MHESHIMIWA RAIS DOCTOR JP. MAGUFULI NINAIPONGEZA KWA KUONA UMUHIMU WA AFYA ZA BINADAMU KWA KUPIGA MARUFUKU UTENGENEZAJI WA MBEGU ZA VYAKULA FEKI VYENYE SUMU VYAKULA VYA KUTENGENEZWA MAVIWANDANI AKA VYAKULA VYA GMO HONGERA SANA RAISI WETU MUNGU MLINDE DOCTOR MAGUFULI AMIN.

Zijue faida na hasara za mbegu za kisasa za GMO zilizopigwa marufuku Tanzania chanzo.https://www.bbc.com/swahili/habari-46313408

 
1. Wakuu hebu tuelimishane kidogo, hizo mbegu za gmo zinazoongelewa hapa ni zipi?

2. Nachojua mbegu zooote zinazotumiwa na wakulima wetu kwa sasa ni hizo ambazo ukivuna huwezi kutumia mazao yake kama mbegu kwa zao la mwaka unaofata.

3. Sasa hivi ili uweze kupata mazao ya uhakika ni lazima kwanza ununue mbegu mpya dukani ndo uipande. Hapo mavuno yanakuwa ni uhakika. Na hii unafanyika kila mwaka.

4. Hii haijaanza juzi wala jana, ni miaka mingi sasa.

Je mbegu hizi zina utofauti na hizo za gmo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari nzuri sana, hizi mbegu za GMOs ni mpango wa wazungu wa kuzifanya nchi za Dunia ya Tatu ziwategee wao,..

Ukianza kutumia hizi mbegu basi inabidi uagize kutoka kwao, kila unapozihitaji..
 
Naona Waziri Mkenda Katoa tena tamko kulikoni ina maana hili agizo toka 2018 halikufanyiwa kazi?
 
Sasa mbona na huyu leo anapiga tena marufuku, ina maana serikali ilidharauliwa marufuku ya kwanza?
 
Tofautisha Hybridization na Genetic modification, sawa? Mzungu akizaa na muAfrika hiyo ni hybridization, ila ukichukua vinasaba vya mbwa na kuviingiza kwenye yai la binadamu ili azaliwe binadamu mwenye uwezo wa kunusa kama mbwa hiyo ni genetic modification, tumeelewana?
 
Kama ni hivyo usemavyo, basi, tumeshamalizwa !!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Natural hybridization kama hiyo ya mzungu na mwafrika na artificial hybridization inayofanywa na gene technologists .Kwenye suala la mimea wanabadilisha mpangilio halisi wa gene ,wanaondoa zile bad traits zote kama magonjwa, kuchelewa kukua, ukame na udogo na ku replace na traits bora kitu ambacho hakifanyiki baina ya binaadamu
 
Hybridization (natural/artificial) imekuwepo tangu karne na karne, ambapo genes ambazo zipo tayari ina nature zinakuwa cross bred kama zilivyo Kwenye organism of origin ili kupata desirable traits, kinachokatazwa hapa ni Genetic modification (modification at the genetic level)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…