Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Serikali yapitia sheria ya kemikali kudhibiti matumizi mabaya ya tindikali.
Kufuatia matukio ya matumizi mabaya ya kemikali ikiwemo tindikali kushamiri hapa nchini serikali imesema inafanya mapitio ya sheria ya matumizi ya kemikali ili kudhibiti hali hiyo na kuongeza kuwa changamoto kubwa inayozikabili kesi za tindikali ni wananchi kutokutoa ushirikiano ili kupata ushahidi unaojitosheleza.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP Bw Eliezer Feleshi kwenye kikao cha pamoja na mkuu wa jeshi la polisi, waandishi wa habari na mkemia mkuu
wa serikali kilichofanyika jijini Dar es Salaam kikiwa na lengo la kuangalia namna vyombo hivyo vitaweza kushirikiana katika kukabiliana na tatizo hilo ambapo wakati
akielezea mabadiliko hayo ya sheria ametoa mifano ya nchi mbalimbali ambazo mtu akibainika kutumia tindikali kinyume na taratibu hukumu yake ni kifo.
Akizungumza katika kikao hicho mkemia mkuu wa serikali Prof Samweli Manyele mbali na kufafanua sheria mbalimbali zinazoruhusu matumizi ya kemikali ametoa
miezi mitatu kwa wafanyabiashara wa kemikali kwenda kujisajili na baada ya hapo kama hawakufanya hivyo hawataruhusiwa kuendelea na biashara hiyo na kuongeza
kuwa ambao tayari wamesajiliwa ni lazima wawe na kumbukumbu sahihi za wateja wao na matumizi yake na waziwasilishe kwake kila mwezi.
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Saidi Mwema amesema tatizo la watu kumwagiwa tindikali hapa nchini ni aina mpya ya uhalifu
iliyojitokeza na kudai kuwa kazi ya upelelezi wakati mwingine inakuwa ngumu kutokana na ushirikiano mdogo wa wananchi huku akiwataka wananchi kuhakikisha
wanatoa ushirikiano wa karibu ili kubaini wanaojihusisha na uhalifu na kwamba taarifa za upelelezi wa matukio ya tindikali zitatolewa na jeshi hilo mara tu zitakapokamilika.
Hata hivyo kikao hicho kimefanyika siku chache tu baada ya raia wawili wa nchini wingereza kumwagiwa tindikali huko visiwani Zanzibar huku kukiwa na mlolongo wa
Watanzania waliofanyiwa vitendo hivyo na hadi sasa hakuna taarifa zozote za watu
waliochukuliwa hatua kuhusiana na matukio hayo.
chanzo. Serikali Yapitia Sheria Ya Kemikali Kudhibiti Matumizi Mabaya Ya Tindikali