Serikali yapoteza State attorneys kila mwaka

Binafsi naunga mkono hoja ya mueshimiwa hapo juu..brother amenena mengi yanayoikabili hii ofisi ya mwanasheria mkuu..Ofisi hii ni muhimu sanaa katika utoaji wa haki hapa nchini..mahakama,polis na ofisi hii ni ofisi zinazotegemeana sanaa..ili haki ipatikane inabdi hawa wadogozake na brother anaowaongelea apo juu waandae mashataka yenye ushaidi mzuri ambao utatoa haki ya mwananchi..bila ya hawa hizo aki tunazosema aziwezi kupatikana kabsaa..najua wananchi wengi awafahamu kazi za hii ofisi na nivigumu sana kwaho kutambua humuimu wa hii ofisi ndiyo maana wachangiaji wengi awajaweza kumuelewa mtoa mada hapo juu..binafsi changamoto ninazoziona katika ofisi hii na maslahi duni kwa wafanyakazi wote wa ofisi hii siongelei wanasheria pekee kama bro hapo juu alivyobagua wafanyakazi wengine wa ofisi hii naongela kwa ujumla wafanyakazi wa ofis hii wte wanansheria nawasio kuwa wanasheria amabo kwapamoja wanatengeneza ofisi hii,maslai yao yanaonekana kuendelea kuwa duni kwasababu kazi za ofisi hii azionekani kama zinamslai na mchango mkubwa katika utoaji wa haki hapa nchini.hii ni moja ya ofisi
kongwe hapa nchini ni ofisi iliyonyuma kimaendelea ukilinfanisha na ofisi nyingine zilizo changa kama PCCB na NAO

Nadhni mwarubaini wa changamoto za ofisi hii ..
. Mosi,ni kuundwa kwa cheo cha mtendaji katika ofisi hii ili kutenganisha masuala ya kitaaluma na kiutawala kwasababu muundo wa ofisi yenyewe bado unamgongano wa kiutendaji kati ya DPP na muajili DAG,lakn pia katika kushughulikia maendeleo ya ofis nadhni wanasheria wameprov failure kwenye ilo kwasababu wameitawala hii ofisi kwa mda mrefu lakn ofisi bado iko nyuma sanaa kimaendeleo ni bora Wakabakia na shughuli za kitaaluma yaani mf kuprosecute etc.
.Mwisho kama hilo likishindikana basi ninaona kiunit cha DPP kijitenge na kijitegemee chenyewe labda inaweza kusaidia kupunguza changamoto za kimuundo.
Ila kama changamoto hizo azitatatuliwa kwakweli maendeo ya ofisi hii
yatakua nyuma sanaa..kwasababu inaonekana wanaoendesha ofisi hii ni waafidhina kimaendelo kabsaa inaonekana ni watu wasioshaurika wanajifanya wajuaji wakila kitu na kibaya zaidi inasemekana watumishi wengine wasio kuwa wanasheria awapewe kipaumbele katika kutekeleza na kutoa ushauri wa taaluma zao kwasababu tu ujuaji wa wwnye ofisi yaani wanasheria ndiyo maana ofisi kwa mda mrefu aipigi atua kabsaa
 
Last edited:

Hakuna mtu au mtumishi yo yote wa umma ambaye anaweza kujidai eti yeye ni mhimu au wa maana zaidi ya mwingine. This is principle number one in any system.
Chukulia mfano huu: Kulikuwa na mabishano makali baina ya viungo vya mwanadamu. Kila kiungo kikijigamba kuwa ni cha mhimu kuliko wengine: mkono, mguu, jicho, sikio, mdomo, pua, mapafu, moyo, ubongo, utumbo, maini, figo, nyeti na kadhalika. Kila kimoja kikijigamba kuwa kazi yake ni mhimu kuliko kingine na kwamba kikiacha kufanya kazi yake wengine wote watapata tabu. Moyo alijigamba kuwa akiacha kusukuma damu ambayo wote wanaihitaji watakufa wote, Figo akajigamba akiacha kusafisha hiyo damu watakufa wote, Pafu akajigamba akiacha kuwaingizia hewa safi na kutoa ile chafu watakipata n.k. Bwana Mkundu ndiye kiungo aliyekuwa anadharauliwa kuliko wote - yaani kazi yake kunya mavi tu! Alijaribu kujieleza kwa wenzake kwamba kazi yake ni mhimu kuliko wengine lakini aliishia kuzomewa! Basi Bwana Mkundu akaamua kugoma kufanya kazi yake: haikupita hata siku tano kila kiungo kikawa hoi, binadamu akawa taabani. Viungo vyote vikambebeleza ayatoe hayo mavi, na alipoyatoa kila mtu alifurahi na kurudia afya yake. Tangia hapo hata Bw. Anus naye alipata heshima yake katika jamii.

Hivyo vigezo vya mishahara vinazingatia kuwa kazi zote zina umuhimu sawa. Tofauti ya mshahara huzingatia mambo mengine hususani: kiwango cha elimu, muda unaotumika kupata elimu hiyo (eg miaka 6 hadi 7 kupata shahada ya kwanza ya udaktari na miaka 4 hadi 5 kupata shahada ya uzamifu ya udaktari), ugumu wa masomo aliyosomea (eg arts versus science), mahitaji/ vipaumbele vya kitaifa, uwezo wa kiuchumi kitaifa wakulipa hiyo mishahara.

Hadi sasa mishahara ya watumishi wa serikali imeboreka zaidi ikiwamo hiyo ya mawakili wa serikali. Sasa hivi mishahara yao ni mikubwa kuliko ilivyo kwenye nyingi ya sekta binafsi. Ni ukweli kuwa sasa hivi output ya wanasheria (LLB) toka vyuo vikuu vyetu nchini ni zaidi ya elfu ishirini kwa mwaka, na wengi wao hawana ajira wako mitaani maana soko lao la ajira limejaa. Wewe inaelekea ulisoma zamani ambapo soko lilikuwa juu, sasa si hivyo. Huu ndiyo ukweli. Kigezo hakiwezi kamwe kuwa eti nchi jirani wanalipa zaidi. Hakuna anayekatazwa kwenda kuajiriwa nchi jirani au yo yote ile. Si rahisi, ndiyo maana wengi tuu wako mitaani. Wahamasishe watoto wako wasome masomo ya sayansi maana ndiyo yenye soko la ajira kwa sasa. Tanzania ya sasa na ijayo ni ya viwanda na teknolojia. Hata hayo majambazi yatadhibitiwa kisayansi na technologia. Unafanya ujambazi unanaswa na makamera, ushahidi tayari na wakili kazi yake inakuwa ndogo tu, na huyo jambazi atalaumu kamera, hata akitoa rushwa kwa wakili haitasaidia.

Ningekuunga mkono kama ungezungumzia tofauti kubwa ya mishahara kati ya wanasiasa na watalaamu katika utumishi wa serikali, si haya mambo ya eti mwanasheria ni muhimu kuliko mwalimu, polisi, mhasibu, mhandisi nk! Tofauti ya mishahara ya wanasiasa na wanataaluma ni janga na tishio la mstakabali wa Taifa (timing bomb). Utakuta hata kijana wa miaka 20 akishakuwa mbunge (hata wa viti maalum) mshahara na marupurupu yake hayapungui Shs million 15 kwa mwezi! Yaani zaidi ya mara 30 ya mshahara wa mhitimu wa shahada ya kwanza!
 
Last edited:
Wamewezaje kuwa waendesha mashtaka au mapolisi bora bila kupitia MIKONO BORA YA MWALIMU!? RISK zipo na tunatambua ugumu wa kazi hizo na hata wakilipwa mamilioni bado ukweli unabaki ubinadamu wao ktk kazi hizo utakuwa hatarini wakati wote na ndio maana pamoja na risk zote hizo na malipo finyu bado Kuna watu wanajiunga na hizo kazi. Kwa hiyo tuboreshe kada zote kimaslahi maana kada hizi zinategemeana!!
 
umeongea jambo la maana sana, mawakili wa serikali kusema kweli wanatakiwa kuboreshewa maslahi, ulinzi etc. vilevile, hatuwezi kuwaacha waalimu ambao ndio wanasaidia nchi hii iwe na wasomi au la, tukiwa na waalimu wanaolipwa vizuri kuanzia watoto wetu hadi watu wazima watakuwa na uelewa mzuri na tukakuwa na kizazi cha kisomi. hakuna mbadala hapa, lazima waalimu wafikiriwe. hata hivyo hii haiondoi ukweli kwamba mawakili wa serikali pia wanahitaji kukumbukwa, wapo katika risk nyingi sana ndio maana wakafika wakati wanaamua tu kujiunga na wahalifu wanatoa siri za kuwasaidia wahalifu ili wahalifu wasifungwe kwasababu hakuna jinsi. hata ningekuwa mimi, maisha yangu yako hatarini lakini serikali hainijali na jambazi anaonekana atanipa interest fulani, sisemi kwamba nitajiunga na jambazi lakini nasema kwa mwanadamu wa kawaida lazima utakuwa kwenye cross-road fulani hivi. no wonder tunaona majambazi na wauaji wanakamatwa na kuachiwa muda si mrefu mahakamani...wanarudi mtaani wanaendelea kuua.
 
nakubaliana na mtoa mada, umuhimu wa hawa jamaa utakuja kuuona siku ukivamiwa na majambazi wamekufanyia umafia wa aibu mbele za watoto wako, majambazi wakakamatwa wewe ukaendelea kuwa home na wao wakawa wanaendelea kupambana na jambazi huyo mahakamani. bila shaka utahitaji jambazi afungwe ili walau asirudi mtaani akufanyie umafia tena...wakati huohuo utakuwa na kihori kwamba sijui jambazi huyo atatoa rushwa kwa hawa jamaa akaachiwa akarudi tena mtaani na akirudi wewe uliyeripoti tukio polisi yaani mtendewa ndio adui namba one jambazi kukushugulikia, na alishaijua nyumba yako yote, si aliingia humo? anaweza kuja. hapo ndio utajua kuwa hawa jamaa wanaopambana na majambazi mahakamani, magaidi na mafisadi wa aina zote, wako katika risk sana ndio maana huwa inafikia kipindi wakiona maisha yao yako hatarini wanasalenda kwa wahalifu wanashirikiana nao kwa kula rushwa na wanaharibu kesi.

jambo la msingi lililoongelewa na mdai ni kwamba, serikali ina train hawa jamaa kila mwaka kwa seminars nyingi sana za garama lakini kwasababu hakuna maslahi, mawakili wa serikali waliopikwa vizuri wanaondoka kwenda kufungua ofisi za kujitegemea na kuwa mawakili wa kujitegemea, jua hawa jamaa pamoja na kwamba wamekuwa mawakili wa serikali, walipita mtihani wa uwakili na kupata cheti cha uwakili lakini jaji mkuu amewazuilia walipokee kazi binafsi kwasababu ya interest kugongana, hivyo anaweza kuacha kazi leo na mwezi huohuo akaanza uwakili wa kujitegemea na serikali hapo inakuwa haijafaidika naye. ni hasara kwa serikali, serikali yeyote au kampuni yeyote huwa na akili ya ku retain wafanyakazi, ukiwa retain ndio kampuni yako inaendelea, wakiwa wanaondoka ni dosari na hasara. tunatakiwa kuweka mbinu za kuwa retain hawa jamaa wanaacha kazi kila mwaka na wanarudi kuwategea wale wahalifu ambao wao wenyewe walikuwa wanawaprosecute. i think this is the point.
 
Naungana na wewe mkuu katika kujali maslahi ya mawakili hao wa serikali kwa ujumla, yaani wake waliopo ofisi ya AG, DPP au TAMISEMI. Kote huko treatment yao si ya kurudhisha, huko TAMISEMI ndio kabisa mpaka sare za mahakamani(suti) wanajinunulia kwa mishahara yao ingawa kazi wanayofanya inawalazimu wavae hayo mavazi ambapo mahakimu au madaktari na manesi wanagharamiwa na serikali mavazi hayo ya kazi.
Hawa jamaa wanakaa mitaani na wanaowashtaki, kiukweli ni hatari sana kwa maana ya urahisi wa kuweza kudhuriwa au hata kushawishiwa rushwa.
Ila napingana na wewe kuhusu serikali kushindwa kesi kwa sababu ya ujunia wa mawakili wa serikali, hii si kweli. Nadhani hapa tunaongelea kesi nyingi za madai ambazo serikali mara nyingi ndio huwa inashindwa. Sababu ni ndogo tu, serikali huwa inaharibu yenyewe kwa kuwapa watu kazi, mfano makandarasi ambao wanafanya kazi halafu haiwalipi kwa wakati kitu kinachopelekea makandarasi hao kufungua kesi za madai mahakamani ambapo hata wakili wa
Serikali awe Malaika bado watashindwa tu sababu mlalamikaji anakua na kesi nyeupe yenye facts za kutosha kumsaidia, anashinda kirahisi tu. Au serikali inapovunja mkataba kienyeji mfano ule wa Dowans lazima itashindwa tu. Kesi za madai karibu zote zinazohusu serikali huwa ni nyeupe sana hivyo sio suala la ujunia au usinia wa mawakili unaopelekea serikali kushindwa bali facts za kesi.
Madaktari walipogoma mwaka 2005/2006 waliongezwa mishahara na allowances nyingine (mshahara wa wakili mwenye degree wakati wa kuajiriwa ni sawa na wa Assistance Medical Officer ambae ni diploma holder anapoajiriwa), sasa basi hali ikiwa mbaya sana wao wenyewe wapigane kupitia vyama na club zao kuhusu kuangaliwa kwa maslahi yao maana kusubiri AG au DPP awapiganie, wataishia kuisoma namba.
 
Nawashauri mtengeneze proposal ya kuomba kuongezewa maslahi, vinginevyo kama haina maslahi acheni kazi hizo njooni tulime mihogo
 


Umeongea nini sasa ndio hao tu umeona wanamaisha mabaya
Hawa polisi walimu manesi
 
hiyo ofisi tangu wamemwondoa feleshi imekuwa takataka. nafikiri kuta tatizo na utawala mpya. feleshi nasikia alishafanya utaratibu hadi wa kuanzisha chuo cha kutrain state attorneys kama kilivyo kwa mahakama kile cha rushoto. sijui kitakuwa wapi, lakini tangu hosea na watu wake wafanye umafia kumwondoa feleshi kwa maslahi ya mafisadi, ofisi hiyo huwa naionea huruma. najua feleshi hawezi kurudishwa na hata akiombwa hatakubali, lakini atafutwe mtu mwingine mwenye akili na maono kama feleshi ili ofisi hii iende mbele. kwenda mbele kwa hii ofisi maana yake ni kusababisha haki zitendeke. ninyi wananchi mkipata tatizo tu mnakimbilia polisi, hizo kesi mnazopeleka polisi hawa mawakili wa serikali ndio wanaoziendesha na ndio wanaweza kupambana hadi wahalifu wenu wakafungwa au kulipa faini. ukiona hauna macho mema kwa hawa jamaa basi ukipata tatizo usiende kuripoti polisi na ukiripoti ujue kesi yako itaendeshwa na watu ambao ni rejects na ambao wanaweza kuwa compromised na wahalifu wakapewa rushwa na kesi yako ikapotea.
 
M
Mbaya zaidi sheria ya kazi imeweka ugumu kwa mawakili wa serikali na mahakimu kufanya migomo ya kudai maslahi bora. Yaani kuwa na chama chao cha kutetea haki zao ni ngumu kama ilivyo jeshi lolote.
 
M

Mbaya zaidi sheria ya kazi imeweka ugumu kwa mawakili wa serikali na mahakimu kufanya migomo ya kudai maslahi bora. Yaani kuwa na chama chao cha kutetea haki zao ni ngumu kama ilivyo jeshi lolote.
wamewakataza hata kuwa washabiki wa chama chochote cha siasa. hilo ni ok, basi wangeboresha maslahi yao basi kwasababu wamewafunga mikono na miguu kilichobaki ni wao kula rushwa au kukimbia ofisi.
 
wamewakataza hata kuwa washabiki wa chama chochote cha siasa. hilo ni ok, basi wangeboresha maslahi yao basi kwasababu wamewafunga mikono na miguu kilichobaki ni wao kula rushwa au kukimbia ofisi.
Si huwa wanasema mlango huu ukifungwa basi mlango mwingine hufunguliwa, basi ndio hivyo kwa state attorney walio wengi huwa hawajali sana serikali kupoteza kesi maadamu wahalifu/mafisadi wametoa kitu kidogo pesa kwao.
 
MwanawaMung leo ndio mnajua fani ya sheria ina risk ?

Askari nao wasemeje. ...usiwaharibu wadogo zako waache watumikie wananchi usipandikize moyo wa tamaa. ..ulitaka walipweje kwa mfano
Kuanzia uchaguzi askari wana posho ya laki 3 kila mwezi
 
Mtoa mada hajui anachokiongea binafsi hakuna kada ambayo ni zaidi ya nyingine pili Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali haitoi ushauri bure kwa wananchi ambao ndio wanafanya wanalipwa mshahara ofisi hii imejaa rushwa ndio maana serikali haishindi kesi ata mtu akija kucertify vyeti lazima atoe pesa kiufupi hakuna kitu cha bure ndani ya ofisi hii ambayo wananchi wana amini hii ndio sehemu ambayo wangeweza kupata huduma ya kisheria bure mimi nadhani ili ni jipu linalo subiri kutumbuliwa baada ya pccb so mtoa mada anajaribu kuvutia upande wake lkn hajui kuwa ofisi hii imeoza kabisa wanakaa pamoja na mawakili wa kujitegemea na mahakimu wanamaliza kesi juu kwa juu na kuiingizia serikali hasara kubwa mno alafu hawa wala rushwa ndo waongezewe mishahara sidhani kama tuna serikali ya kipuuzi kiasi hicho ndo maana serikali inapokuwa na kesi za maana inawaalika mawakili toka nje ya nchi inajua kinacho endelea ndani ya ofisi hii.
 
Kila kada ina umuhimu wake na huo umuhimu unatofautiana, hivi kwa mfano unalinganisha vipi daktari bingwa aliyetoka kufunya upasuaji wa masaa 8 na Mwalimu aliyekuwa anafundisha vita vya maji maji? Tofauti ziko wazi ndio maana baadhi ya kazi watu hulipwa kwa masaa
 
Duh nipo mwaka wa pil naweza kubadisha maana kama ndo ivyo nisipoteze mda kumeza vifungu tu
 
Labda mtoa mada hapo juu angetuambia ni kada hipi hisiyo kuwa na umuhimu katika kutekeleza majukumu ya kitaifa
 
Visingizio tu kila siku, nani alikwambia mishahara mizuri inazuia rushwa, hizo rushwa za TRA na Bandari huzisikii nini ilihali wana mishahara ya maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…