Serikali yapunguza riba ya mikopo

Serikali yapunguza riba ya mikopo

Benki Kuu inapaswa kufanya "auditing" taasisi zote za fedha ambazo zipo chini yake. Katika taasisi za fedha ambazo zipo katika "Tiers 2, 3 " 4 kutokana na MFI Act ya 2018 itakutana na "lending rate" za ajabu sana. Pamoja na uwepo wa ""loan sharkrs" lakini kitu cha ajabu ni kwamba watu wanazidi kukopa tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo imetumika tu lugha ya jumla kuhusu kushushwa kwa riba pengine kwa malengo fulani ya kiki za kisiasa. Benki Kuu pamoja na kuwa yeye ni "regulator" lakini kamwe haiwezi kukurupuka na kuagiza mara moja kuanza kutumika kwa 'price ceiling' mpya kwa taasisi za kifedha ndani ya soko la fedha.

Riba huwalilisha bei ya bidhaa za kifedha iliyopo sokoni, ambapo hutegemea nguvu utashi kwa wanunuzi, na pia nguvu za ugavi kwa watoa huduma za kifedha. Taasisi mbalimbali za kifedha huweka viwango vya riba kwa kutegemea vigezo vya kiuwiano katika kutaka kuiendeleza taasisi husika kifaida, na kama ni ya wanahisa, basi lengo kubwa likiwa ni kurudisha faida kwao.

Bajeti, mipango na mikakati ya taasisi yoyote ile ya kifedha, hutegemea uwiano wa namba za kiakaunti na kifedha, "the bottomline being Return on Equity (ROE)" Ndiyo maana viwango vya riba vilivyopo sokoni vya kibenki, ni si chini ya 16% kwa zile bidhaa ambazo hazina ruzuku kutoka serikalini. Na kwa taasisi zingine za kifedha ambazo si za kibenki utakuta riba zake ni kati ya 48% mpaka kufikia 96%.

Na hapo kinachokokotolewa na kuwekwa nisu bayana kwa wateja ni "normal interest rate" na wala siyo 'effective interest rate". Nikisema nusu bayana namaanisha mteja humbiwa tu kuhusu riba ya mkopo kwa mwezi na wala si kwa muda wote wa kipindi cha mkopo, ama njia ambayo inatumika kukokotoa riba husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sentensi za paragraph ya mwisho ni muhimu sana kwa watanzania wa kawaida...Wengi wamejikuta kwenye madeni yasiyolipika
 
Rais Samia Suluhu anaendelea kuteka mioyo ya watanzania walio wengi kwa jitihada hizi za kuinua uchumia wa mtanzania kwa maendeleo haya 2025 Rais Samia Suluhu atashinda kwa kishindo
Mkuu Nyabukika, hili ni jambo jema, kwa maendeleo ya taifa na litasaidia sana wananchi, ila sasa naomba usilete siasa za uchawa katika hili kuwa 2025 atashinda kwa kishindo, huu uchawa uta waterdown nia njema na nia nzuri ya Mama kwenye hili la kushusha riba likaonekana ni kwa ajili 2025
P
 
Hivi raia tu mpambanaji kitaa mwenye ghetto lenye sufuria mbili na ndoo saba na (sabufa)na tv chogo 18" anawezaje kupata mkopo Bank?hili ni swali gumu nililowahi kuulizwa
Na hata ukiwa na dhamana ya nyumba au gari,na biashara lazima utaletewa vikwazo kwa mtanzania halisi ila wa Asia fasta wanapewa mikopo.
 
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu iliahidi kumuinua mwananchi kiuchumi na sasa imekuja na punguza ya riba ya mikopo ya mtu binafsi

Benki Kuu ya Tanzania imetangaza kushusha riba ya mikopo binafsi kutoka asilimia kati ya 11 na 13 hadi asilimia 9.

Hatua hii inafuatia mwongozo wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuongeza upatikanaji wa mitaji ya biashara kwa riba nafuu kwa kila mtu mwenye sifa.

Rais Samia Suluhu anaendelea kuteka mioyo ya watanzania walio wengi kwa jitihada hizi za kuinua uchumia wa mtanzania kwa maendeleo haya 2025 Rais Samia Suluhu atashinda kwa kishindo
Hata riba ikiwa asililimia 2 inakusaidia nini wakati bei ya mchele, unga na mafuta ya kupikia ambavyo ni vitu vya kila siku bei zake zinapaaa?? Unafikiri huo mkopo atapata kila mtu...ukikopa ujue utalipa
 
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu iliahidi kumuinua mwananchi kiuchumi na sasa imekuja na punguza ya riba ya mikopo ya mtu binafsi

Benki Kuu ya Tanzania imetangaza kushusha riba ya mikopo binafsi kutoka asilimia kati ya 11 na 13 hadi asilimia 9.

Hatua hii inafuatia mwongozo wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuongeza upatikanaji wa mitaji ya biashara kwa riba nafuu kwa kila mtu mwenye sifa.

Rais Samia Suluhu anaendelea kuteka mioyo ya watanzania walio wengi kwa jitihada hizi za kuinua uchumia wa mtanzania kwa maendeleo haya 2025 Rais Samia Suluhu atashinda kwa kishindo
Wallahi naenda benki sasa hivi.
 
Mimi ni mkopo NMB nakatwa asilimia 18% Acheni uongo kama Wa Magufuli
 
Tukisema ana upiga mwingi, wengine wanaumia. Hakika kupunguza riba ni jambo jema
Rais Samia Suluhu alisema lengo lake ni kuwainua watanzania kiuchumi ndio maana unaona kila siku anakuja na njia mpya za kuwainua watanzania kwa haya anayoyafanya tuna kila sababu ya kusema anaupiga mwingi
 
Back
Top Bottom