Serikali yasema idadi ya magonjwa ya ngono imeongezeka pia watu 1,612,52 wanatumia ARV’s Nchini Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Watoto Milioni 1.5 wapatiwa chanjo
Wizara ya Afya imesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu jumla ya watoto 1,596,951 sawa na asilimia 98.6 walikuwa wamechanjwa chanjo ya Penta3 kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya Dondakoo, Kifaduro, Kupooza, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo, ambayo hutumika kama kipimo kikuu cha chanjo ikilinganishwa na asilimia 94.6 mwaka 2021/2022.

Watoto 24 kati ya 1000 hufariki Dunia
Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha huduma kwa Watoto wachanga ambapo matokeo ya utafiti wa viashiria vya Afya ya Uzazi na Mtoto ya mwaka 2022 "TDHS 2022” yameonesha kuwa vifo vya watoto wachanga ni 24 kwa kila vizazi hai elfu moja.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa matokeo hayo yanaonesha umuhimu wa Serikali kuongeza nguvu katika kupunguza vifo vya watoto wachanga ili kufikia lengo la Kimataifa la kupunguza vifo vya watoto wachanga hadi kufikia 12 kwa kila vizazi hai elfu moja ifikapo mwaka 2030.

Watu 1,612,52 wanatumia ARV’s
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu jumla ya wateja 1,632,328 sawa na asilimia 94.4 ya watu 1,729,408 wanaodhaniwa kuishi na virusi vya Ukimwi nchini walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi.

Waziri Ummy amesema, kati yao wateja 1,612,520 walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza Virusi hivyo ambapo watoto walikuwa ni 58,760.

Wanaotumia uzazi wa mpango wamepungua
Serikali imesema katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 hadi Machi mwaka huu Serikali kwa kushirikiana na Wadau imetoa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na kununua na kusambaza bidhaa za uzazi wa mpango ikiwemo vidonge vya uzazi wa mpango, sindano za uzazi wa mpango na vipandikizi ambapo katika kipindi cha taarifa hiyo jumla ya wateja 4,509,605 walitumia njia mbalimbali za kisasa za uzazi wa mpango ikilinganishwa na wateja 4,905,854 kipindi kama hicho mwaka 2021/2022.

Wagonjwa 812 kutoka Nchi 11 watibiwa Nchini
Serikali imesema katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 hadi mwezi Machi mwaka huu jumla ya wagonjwa 812 wamehudumiwa na hospitali za
Taifa, Maalum na Kanda ukilinganisha na wagonjwa 368 waliotibiwa kipindi kama hicho mwaka 2021/2022.

Akiwasilisha bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa wizara hiyo Ummy Mwalimu amesema, wagonjwa hao walikuwa wanatoka katika nchi za Kenya, Uganda, Congo, Comoro, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Sudan Kusini.

Malaria bado kinara
Serikali imesema katika kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi mwezi Machi 2023, magonjwa yaliyoongoza katika kuwaathiri zaidi wananchi na kuwasababishia kwenda katika vituo vya kutolea huduma kupata matibabu ni maambukizi katika mfumo wa hewa, maambukizi ya njia ya mkojo na Malaria.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema, magonjwa yaliyoongoza hadi mgonjwa kulazwa hospitalini ni Malaria, homa ya mapafu na Anemia.

Ameongeza kuwa, takwimu zinaonesha kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa ndani ya magonjwa kumi yanayoathiri zaidi wananchi.

Tsh. Bilioni 14.5 zanunua mashine za MRI
Serikali imeendelea kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo jumla ya mashine za MRI sita zimenunuliwa kwa gharama ya shilingi 14,534,624,000 ambapo kati ya mashine hizo nne zimeishasimikwa na kuanza kutoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali ya Taifa ya Saratani - Ocean Road, hospitali ya kanda - CHATO na hospitali ya kanda - MTWARA.

Idadi ya magonjwa ya ngoni imeongezeka
Serikali imesema idadi ya watu wanaougua magonjwa ya ngono imeongezeka kutoka wagonjwa 458,914 hadi wagonjwa 480,448 mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa rai kwa Watanzania kutumia kinga ili kujikinga na magonjwa ya ngono.
 
Idadi ya watu waliougua magonjwa ya ngono imeongezeka kutoka wagonjwa 458,61 katika kipindi cha kati ya Januari mwaka 2021/22 hadi 480,448 katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya mwaka 2023/24.

“Magonjwa ya ngono yaliyoongoza ni Klamidia (Chlamydia), Kaswende (Syphilis) Kisonono (Gonorrhea) na Herpes,”amesema Ummy.

Aidha, Ummy amesema ili kuwakinga watoto wachanga kuzaliwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono ambapo wajawazito milioni 1.09 sawa na asilimia 65 walipimwa maambukizi ya Kaswende ikilinganishwa na wajawazito milioni moja sawa na asilimia 66 katika mwaka 2021/2022.
 
Hivi inakuwaje wale jamaa Telegram wanawababua wale makahaba kavu kabisa!? Nadhani chanzo kimeanzia huku
 
watu hawana kazi pesa wala michongo mambo yaliyobaki ni kuni tu kwa kwenda mbele tu
 
Watoto Milioni 1.5 wapatiwa chanjo
Wizara ya Afya imesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu jumla ya watoto 1,596,951 sawa na asilimia 98.6 walikuwa wamechanjwa chanjo ya Penta3 kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya Dondakoo, Kifaduro, Kupooza, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo, ambayo hutumika kama kipimo kikuu cha chanjo ikilinganishwa na asilimia 94.6 mwaka 2021/2022.

Watoto 24 kati ya 1000 hufariki Dunia
Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha huduma kwa Watoto wachanga ambapo matokeo ya utafiti wa viashiria vya Afya ya Uzazi na Mtoto ya mwaka 2022 "TDHS 2022” yameonesha kuwa vifo vya watoto wachanga ni 24 kwa kila vizazi hai elfu moja.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa matokeo hayo yanaonesha umuhimu wa Serikali kuongeza nguvu katika kupunguza vifo vya watoto wachanga ili kufikia lengo la Kimataifa la kupunguza vifo vya watoto wachanga hadi kufikia 12 kwa kila vizazi hai elfu moja ifikapo mwaka 2030.

Watu 1,612,52 wanatumia ARV’s
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu jumla ya wateja 1,632,328 sawa na asilimia 94.4 ya watu 1,729,408 wanaodhaniwa kuishi na virusi vya Ukimwi nchini walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi.

Waziri Ummy amesema, kati yao wateja 1,612,520 walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza Virusi hivyo ambapo watoto walikuwa ni 58,760.

Wanaotumia uzazi wa mpango wamepungua
Serikali imesema katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 hadi Machi mwaka huu Serikali kwa kushirikiana na Wadau imetoa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na kununua na kusambaza bidhaa za uzazi wa mpango ikiwemo vidonge vya uzazi wa mpango, sindano za uzazi wa mpango na vipandikizi ambapo katika kipindi cha taarifa hiyo jumla ya wateja 4,509,605 walitumia njia mbalimbali za kisasa za uzazi wa mpango ikilinganishwa na wateja 4,905,854 kipindi kama hicho mwaka 2021/2022.

Wagonjwa 812 kutoka Nchi 11 watibiwa Nchini
Serikali imesema katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 hadi mwezi Machi mwaka huu jumla ya wagonjwa 812 wamehudumiwa na hospitali za
Taifa, Maalum na Kanda ukilinganisha na wagonjwa 368 waliotibiwa kipindi kama hicho mwaka 2021/2022.

Akiwasilisha bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa wizara hiyo Ummy Mwalimu amesema, wagonjwa hao walikuwa wanatoka katika nchi za Kenya, Uganda, Congo, Comoro, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Sudan Kusini.

Malaria bado kinara
Serikali imesema katika kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi mwezi Machi 2023, magonjwa yaliyoongoza katika kuwaathiri zaidi wananchi na kuwasababishia kwenda katika vituo vya kutolea huduma kupata matibabu ni maambukizi katika mfumo wa hewa, maambukizi ya njia ya mkojo na Malaria.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema, magonjwa yaliyoongoza hadi mgonjwa kulazwa hospitalini ni Malaria, homa ya mapafu na Anemia.

Ameongeza kuwa, takwimu zinaonesha kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa ndani ya magonjwa kumi yanayoathiri zaidi wananchi.

Tsh. Bilioni 14.5 zanunua mashine za MRI
Serikali imeendelea kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo jumla ya mashine za MRI sita zimenunuliwa kwa gharama ya shilingi 14,534,624,000 ambapo kati ya mashine hizo nne zimeishasimikwa na kuanza kutoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali ya Taifa ya Saratani - Ocean Road, hospitali ya kanda - CHATO na hospitali ya kanda - MTWARA.

Idadi ya magonjwa ya ngoni imeongezeka
Serikali imesema idadi ya watu wanaougua magonjwa ya ngono imeongezeka kutoka wagonjwa 458,914 hadi wagonjwa 480,448 mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa rai kwa Watanzania kutumia kinga ili kujikinga na magonjwa ya ngono.

Mods unganisha huu uzi
 
Cc Juma1967 (joshua_ok)
 
Back
Top Bottom