BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Your browser is not able to display this video.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amesema imejiridhisha kuwa Watanzania 201 waliopo huko wapo salama ambapo kati yao 171 ni Wanafunzi na idadi nyingine ni raia na Maafisa wa Ubalozi.
Dkt. Tax amesema Serikali imesikitishwa na kuzorota kwa hali ya Usalama na imeunga mkono Tamko la Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika la kukemea Mapigano yanayoendelea Nchini humo kati ya Jeshi Tawala na Upinzani.
Tanzania imezitaka pande mbili zinazopigana Nchini humo kukaa na kujadili changamoto zilizojitokea pamoja na kuzitatua kwa kuhakikisha zinazingatia mahijtaji ya Binadamu na Usalama wa Raia wa Nchi nyingine.