Serikali yasema itawaondoa Watanzania waliopo Sudan kama itahitajika

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amesema imejiridhisha kuwa Watanzania 201 waliopo huko wapo salama ambapo kati yao 171 ni Wanafunzi na idadi nyingine ni raia na Maafisa wa Ubalozi.

Dkt. Tax amesema Serikali imesikitishwa na kuzorota kwa hali ya Usalama na imeunga mkono Tamko la Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika la kukemea Mapigano yanayoendelea Nchini humo kati ya Jeshi Tawala na Upinzani.

Tanzania imezitaka pande mbili zinazopigana Nchini humo kukaa na kujadili changamoto zilizojitokea pamoja na kuzitatua kwa kuhakikisha zinazingatia mahijtaji ya Binadamu na Usalama wa Raia wa Nchi nyingine.
 
Waziri mwenye dhamana una mpango gani na watanzania wenzetu walioko nchini sudan?
Ndugu zetu wapo hatarini
hawakai kwa amani
Hawajui hatma yao
 
Masaa 72 yametolewa kwa nchi kutoa watu wao.

Marekani kapeleka ndege 11 kuondoa kila kilicho chake.

Japan naye kafanya hivyo hivyo

Tanzania haitapeleka kitu
 
waliopo eneo la tukio wanasema hali si nzuri kwa sasa kiasi kwamba mpaka risasi zimeanza kuingia vyumbani kwao.
IMG-20230421-WA0035.jpg
 
Waziri mwenye dhamana una mpango gani na watanzania wenzetu walioko nchini sudan?
Ndugu zetu wapo hatarini
hawakai kwa amani
Hawajui hatma yao
Waziri yuko sahihi watanzania walioko Sudan wako salama wengi wanavyuo

Watanzania wengi walioko Sudan hiyo ya waarabu wengi wanasomea uislamu vyuo vya kiislamu vya hapo Sudan

Wanaopigana wote waislamu tena wamefunga Ramadhani.Na ikifika saa ya swala wote huswali

Na wote wakirushiana risasi na makombora utawasikia wakipiga kelele Allah Akbar kila upande

Misikiti na maeneo ya vyuo vya kiislamu wote pande zote wanayeheshimu sina hakuna upande ambao utashambulia hayo maeneo
Wako salama kwenye maeneo hayo
 
Masaa 72 yametolewa kwa nchi kutoa watu wao.

Marekani kapeleka ndege 11 kuondoa kila kilicho chake.

Japan naye kafanya hivyo hivyo

Tanzania haitapeleka kitu
Wale boda to boda

Ova
 
Waziri yuko sahihi watanzania walioko Sudan wako salama wengi wanavyuo

Watanzania wengi walioko Sudan hiyo ya waarabu wengi wanasomea uislamu vyuo vya kiislamu vya hapo Sudan

Wanaopigana wote waislamu tena wamefunga Ramadhani.Na ikifika saa ya swala wote huswali

Na wote wakirushiana risasi na makombora utawasikia wakipiga kelele Allah Akbar kila upande

Misikiti na maeneo ya vyuo vya kiislamu wote pande zote wanayeheshimu sina hakuna upande ambao utashambulia hayo maeneo
Wako salama kwenye maeneo hayo
Dah! Hivi tafsiri ya Allah Akbar kwa kiswahili ni ipi?
 
Mungu Mkubwa majeshi ya Sudan wanaopigana wote waislamu kila mmoja akilenga mwenzie na risasi ,bomu au kombora anaruka ruka na kusema Allah Akbar yaani Mungu mkubwa kaniwezesha kumtandika Risasi, bomu au kombora Muislamu mwenzie upande wa pili wanayepigana naye

Anamshukuru Allah kumuwrzesha kutwanga muislamu mwenzie
 
Kuwa na maarifa na akili,hawa hawapigani kwa ajili ya dini,hawa wanapigana kwa ajili ya siasa.
 
Mungu Mkubwa majeshi ya Sudan wanaopigana wote waislamu kila mmoja akilenga mwenzie na risasi ,bomu au kombora anaruka ruka na kusema Allah Akbar yaani Mungu mkubwa kaniwezesha kumtandika Risasi, bomu au kombora Muislamu mwenzie upande wa pili wanayepigana naye

Anamshukuru Allah kumuwrzesha kutwanga muislamu mwenzie
Kuwa na akili na maarifa,hivi ni vita vya kisiasa sio vyakidini.
Wataka kusema vita vya Kongo au Sudan kusini,au Urusi na Ukraine,wanasema Yesu wangu,wakati wakitwangana?
 
Nchi nyingine wameshaondoa watu wao.

yale masaa 72 waliotolewa yanakaribia kuisha.

watanzania wao wanapigwa kalenda kila leo

Hali hii mpaka lini au mpaka ghasia izidi ndio muone kama hawapo salama.
 
Tanzania haina nyenzo, nia ya kuwatoa.
Maana inabidi waongee na RSF na Sudan Army, wakubaliane afu ndo wapeleke helicopter
 
Back
Top Bottom