Serikali yashangaa gesi ya kupikia kupanda bei, yataka viwanda vieleze sababu ya ongezeko hilo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Serikali imesema viwanda vya gesi ya kupikia havijafata utaratibu katika kupandisha bei hivyo bei mpya hazitambuliki.

Afisa wa Ewura mr Kaguo amesema viwanda vya gesi vimetakiwa vipeleke vigezo vya kupandisha bei na serikali ama itavibariki na kukubali bei mpya ama itavikataa kama havijitoshelezi.

 
Maeneo mengine serikali wako makini, ila sehemu nyingine wanawaachia wananchi mizigo waibebe wenyewe, au kwasababu hili halijapitia bungeni ndio maana serikali imesimama na wananchi? Kwa sababu kama likipitia bungeni hata likiwa na maumivu kwa wananchi lazima lipitishwe.
 
Kwenye ishu za bei mara nyingi serikali ikiingilia ndo mambo huwa magumu, mfn: sukari na mafuta ya kupikia.

Kwenye hili la gesi waache maigizo na kushangaa wawe serious.
 
Inahitaji tone Moja tu la akili kutambua sababu za kupanda bei ya bidhaa. Tozo za kijinga Kila mahali zinapunguza mzunguko wa pesa. Kwa bahati mbaya tuliopo kitaa tuna mawazo mazuri ya maendeleo lakini walio na wadhifa na nafasi ya maamuzi, hawawazi lolote zaidi ya kulinda nafasi zao watawale milele
 
Mkuu hapo hakuna kitachobadilika, hao wenye viwanda watatoa pesa na mambo yataendelea
 
Haya yatafika mwisho siku tukiamua kutanguliza Nchi kwanza vyama baadae, Ila kwakua tumechagua vyama kwanza.... tuendelee hivi hivi, ni hakuna kupumua hadi siku ya kudanja
 

Ustake ncheke. Serikali hawa hawa wanashangaa?



Kwani hawa watalipa vipi tozo wanazo tozwa?

Na waongeze kama mara 10 hivi, itapendeza zaidi.
 

Futuhi, Mimi sijawahi fanya biashara ya gas ila naweza elezea!
 
Serikali ya Tz Bwanaaah! Vitukotuko tupu, Yan wanajitekenya wao kisha wanacheka, wanatengeneza tatizo zen wajishangaza afu wanaigiza kutatua ili kuhadaa wananchi!
 
Jamani 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…