bulama
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 561
- 135
Katika hali ya kusikitisha serikali imewatelekeza walimu wanafunzi wa vyuo vya ualimu vya CHETI pamoja na Stashada ambao wapo kwenye mazoezi ya Muda mrefu ya kufundisha (BTP). Tarehe 3 mwezi huu wizara ya elimu iliruhusu hao wanafunzi kwenda mazoezi kwa kuwalipa posho ya siku 15 tu kwa ahadi ya kuongeza fedha hiyo kabla tarehe 15, Cha kusikitisha mapaka leo hii naonngea hapa hakuna hela iliyoongezwa wala tetesi kwamba hiyo hela inakuja lini. Watoto wawatu wameanza kuonja joto ya jiwe ukizingatia maisha yalivyo huko katika vijiji vyetu waliko pangwa.
Naomba mweshimiwa Waziri wa fedha na wasaidizi wako mlione hili ili muweze kuwasaidia hawa watoto wa wakulima na walala hoi.
Naomba mweshimiwa Waziri wa fedha na wasaidizi wako mlione hili ili muweze kuwasaidia hawa watoto wa wakulima na walala hoi.