SI KWELI Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Baada ya Kushindwana na Mwekezaji

SI KWELI Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Baada ya Kushindwana na Mwekezaji

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
1660131135961.png

Kumekuwepo na madai kuwa Serikali imesitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo baada ya Kushindwana na mwekezaji.

Hapo awali Serikali ilifufua mazungumzo na mwekezaji kuhusu ujenzi wa Bandari hiyo ila mazungumzo hayakwenda sawa.

Hayo yamesemwa na Waziri Prof. Makame Mbarawa

NB. Kwenye suala na negotiation timu ya mama Samia ipo vizuri sana na ipo kwa maslahi ya watanzania wote.
 
Tunachokijua
Serikali ilianza kuhakiki mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwezi wa kwanza 2022. Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema Serikali inapitia mkataba wa mradi wa uwekezaji wa ukanda maalumu wa Bagamoyo, ili kuhakikisha unakuwa na tija kwa masilahi ya Taifa.

Juni 24 mwaka 2022, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Hata hivyo, Rais wa tano, Hayati John Magufuli aliwahi kukaririwa akisema ujenzi wa mradi wa Bagamoyo una masharti magumu ya mwekezaji ndio sababu ya kusuasua kutekelezwa. Miongoni mwa masharti yaliyowekwa na wawekezaji ni kutaka kumilikishwa Eneo la Mradi kwa Miaka 99, Serikali kutochukua kodi yoyote kwa kipindi hicho, Nchi kugharamia utekelezaji wake sambamba na kutoendelezwa kwa bandari nyingine yoyote.

Katika mwaka wa fedha 2021/2022, wizara ilifufua majadiliano na wawekezaji wa Kampuni ya China, Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) na Oman Investment Authority (OIA) ambayo awali ilikuwa inaitwa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (SGRF).

Juni 26, Rais Samia Suluhu Hassan alisema wameanza mazungumzo ya kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ule wa chuma na makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga.

“Nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika wanaendelea na mazungumzo na wawekezaji wa Mchuchuma na Liganga kuona tatizo ni nini hasa. Serikali inaweza kujitoa hadi wapi na mwekezaji anaweza kujitoa hadi wapi ili mradi ufanye kazi.”


Taarifa zilizopo duniani chuma kimepanda bei ni wakati mzuri wa kuharakisha kuufanya mradi huu. Bagamoyo tunakwenda kuanza mazungumzo na taasisi iliyokuja kwa ajili ya mradi huu ili tuifungue na tuende nao kwa faida yetu,” alesema Rais Samia.

Rais Samia alitoa kauli hiyo wakati kukiwa kumeibuka mjadala bungeni kuhusu bandari hiyo, ambapo aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai aliitaka Serikali kuangalia upya mradi wa bandari hiyo mkoani Pwani na iwapo ni jambo jema waendelee nao.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi kama makala ilivyochapishwa Juni 10, 2019, Ndugai alinukuliwa akisema;

“Sisi hatukuwa na taarifa ya masharti ya nyongeza ambayo mheshimiwa Rais ameyaeleza. Katika majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji, wakati mwingine siyo kwamba tunaangalia mambo yote, huwa tunaangalia faida za mradi,”

Lakini Rais ameeleza masharti kwa mfano kuzuia bandari zote kuanzia Tanga hadi Mtwara zisifanye kazi. Sasa masharti kama hayo ni ya kipumbavu sana, ya kijinga, sijui hata. Haiwezekani kutekeleza huo mradi kwa masharti hayo.”

Kwamba sisi tusikusanye kodi kwa miaka 100 ni vitu vya ajabu sana. Rais akishasema basi. Kwa masharti yake hayo, haufai kabisa. Lakini kwa zile faida tulikuwa tunaangalia, kumbe kuna masharti hasi ambayo wabunge hawakuyajua,”
aliongeza Ndugai.

Hadi sasa, JamiiForums haijapata taarifa yoyote iliyotolewa kuoneshwa kusitishwa kwa mazungumzo ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo
Mwindaji aliposema hawa jamaa ni wahuni hawatoi 21 trill
Kwa kuwachekea chekea tu mezani,bali wanataka bandari iwe yao na waiendeshe miaka kadhaa,wahuni wakazusha kwamba amekaza sababu hajapewa mgao[emoji16][emoji16][emoji16].

By the way hizi ni habari njema kwa mstakabali wa taifa.
 
Back
Top Bottom