Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SERIKALI YATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA MIRADI KWA WAKATI
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Jackline Msongozi ameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati bila kusubiri misimu kwa kujenga vipande nusu nusu.
Ameyasema hayo wakati akichangia hotuba ya wizara ya ujenzi na uchukuzi iliyowasilishwa Mei 22 mwaka 2023 bungeni na Waziri wa wizara hiyo Prof. Makame Mbarawa.
“Barabara ya urefu wa kilomita 64 mkajenga kipande nusu halafu baadaye inasubiri tena miaka mitano hainogi, malizieni km124 zote ziwe na commitment ya serikali”
Aidha amesema kuwa uwepo wa utaratibu wa serikali kutolipa wakandarasi kwa wakati imekuwa hali inayopelekea barabara kutokamilika kwa wakati na kudumaza uchumi wa nchi.
“Magari yanayobeba makaa ya mawe ndiyo yanayopita kwenye barabara hiyo, pesa iharakishwe ili barabara iweze kujengwa kutokufanya hivyo maana yake ni kudumaza hali ya uchumi katika Mkoa wa Ruvuma na nchi yetu, kutangazwa ni jambo Moja na kupeleka fedha ni jambo lingine” Mhe. Msongozi
Aidha ametumia nafasi hiyo kutoa mchango wake katika miradi inayoendelea ikiwemo SGR huku akiipongeza serikali kwa kuendelea kukamilisha miradi ya Maendeleo iliyoanzishwa na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na kuwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao pasi na kujali changamoto zilizopo
“Kelele za Chura hazimzuii tembo kunywa Maji hizo ndo changamoto za kazi Fanya kazi, endelea kupambana” Mhe. Msongozi
Amehitimisha kwa kumtaka Waziri wa Wizara hiyo kukamilisha ujenzi wa reli kutoka Mtwara mpaka Mbambabei ili kurahisisha shughuli za usafirishaji wa mizigo (makaa ya mawe) kwani hali ya barabara hiyo ni mbovu.