Serikali yatenga bil 3/- kufadhili wanafunzi 500 masomo ya sayansi

Serikali yatenga bil 3/- kufadhili wanafunzi 500 masomo ya sayansi

Joined
Sep 16, 2021
Posts
4
Reaction score
10
Serikali ya Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi wa masomo ya Sayansi na Teknolojia hasa katika zama za wakati tulio nao, Rais Samia Suluhu kupita bajeti ya Serikali ya Wizara ya Elimu 2022/23 kiasi cha Sh. 3bn/- kimetengwa kwa ajili ya kufadhili wanafunzi 500 wa masomo ya Sayansi.

Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita watapata ufadhili wa masomo katika kada za udaktari na uhandisil.
 
Kuna wanafunzi chungumbovu waliosoma sayansi wako mitaani hawana pa kwenda . Mh. Raisi Kikwete alianzisha courses maalumu za sayansi vyuo vikuu,akaweka hadi upendeleo wa Mikopo elimu ya juu. Alipoondoka madaraka akaingia ambaye hana kazi nao,kaajiri zaidi mapolisi kumlinda.

Pale SUA, kuna kozi mpya alianzisha Mzee Kikwete,inaitwa Bioprossesing and Post harvesting Engineering na ililenga kuanzisha na kuendeleza Kilimo katika Value addition kwa kuprocess mazao ya Kilimo na Mifugo. Alipoondoka TU, end of story. Matokeo yake, sasa tunaita wawekezaji kufanya kazi Zile wangewezeshwa hao vijana wanaograduate kila mwaka.

Nashauri, hii fedha kiasi iende mikoani kuwezesha ambao tayari ni wanasayansi waliohitimu na tayari wana entrepreneural ideas waimplement. Wachina, Wakorea nk walifanya hivyo. Kiasi kiendeleze mpango huo wa serikali
 
Back
Top Bottom