Kuna wanafunzi chungumbovu waliosoma sayansi wako mitaani hawana pa kwenda . Mh. Raisi Kikwete alianzisha courses maalumu za sayansi vyuo vikuu,akaweka hadi upendeleo wa Mikopo elimu ya juu. Alipoondoka madaraka akaingia ambaye hana kazi nao,kaajiri zaidi mapolisi kumlinda.
Pale SUA, kuna kozi mpya alianzisha Mzee Kikwete,inaitwa Bioprossesing and Post harvesting Engineering na ililenga kuanzisha na kuendeleza Kilimo katika Value addition kwa kuprocess mazao ya Kilimo na Mifugo. Alipoondoka TU, end of story. Matokeo yake, sasa tunaita wawekezaji kufanya kazi Zile wangewezeshwa hao vijana wanaograduate kila mwaka.
Nashauri, hii fedha kiasi iende mikoani kuwezesha ambao tayari ni wanasayansi waliohitimu na tayari wana entrepreneural ideas waimplement. Wachina, Wakorea nk walifanya hivyo. Kiasi kiendeleze mpango huo wa serikali