Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Serikali tayari imetenga eneo jipya la ujenzi wa soko la mpito, kwa ajili ya Wafanyabiashara waathirika wa janga la moto, lililotokea usiku wa kumakia September 15 mwaka huu katika soko kuu la Kawe.
Haya yameelezwa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe: Suleimani Jafo, alipotembelea soko hilo liloteketea kwa moto na Kuzungumza na Wafanyabiashara na waathirika, pia kukagua hatua zinzoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Wilaya na Mkoa za kurejesha hali kuwa safi kama hapo mwanzo.
Waziri Jafo amesisitiza kuwa, ujenzi wa soko hilo la mpito linalotarajiwa kuanza kujengwa kuanzia sasa, katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, uende na ukamilike kwa haraka ili shughuli za kibiashara ziendelee kama kawaida, huku ujenzi wa soko kuu la Kawe ukiwa unaendelea katika viwango vya kisasa, na pindi utakapomalizika basi Wafanyabiashara hao watarejeshwa katika maeneo yao ya awali yaliyoboreshwa zaidi