Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Serikali imesema inatarajia kutumia shilingi bilioni 730 na chenji katika maandalizi na kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za vuli zinazotarajiwa kuambatana na hali ya El Niño, kuanzia Oktoba 2026.
Kwa mujibu wa mpango huo, sehemu ya fedha hizo zitatumika katika maandalizi yanayoanza Agosti hadi Oktoba 2026, ikiwa ni pamoja na tathmini za hatari, maandalizi ya sekta ya afya na uimarishaji wa miundombinu.
Katika eneo la tathmini ya hatari mikoani, Serikali imetenga shilingi milioni 780 kwa ajili ya kutathmini uwezekano wa kuathirika na uwezo wa kukabiliana na majanga katika mikoa 11 iliyoainishwa kuwa katika hatari ya El Niño.
Aidha, shilingi milioni 240 zitatumika kufanya tathmini ya utayari wa huduma za afya katika mikoa hiyo, huku shilingi milioni 50 zikitengwa kwa ajili ya tathmini na uchoraji wa ramani za hatari za magonjwa ya mlipuko, ikiwemo kipindupindu, dengue, chikungunya na homa ya Bonde la Ufa.
Soma Pia: TMA: October kuna mvua za El Nino zinakuja
Katika upande wa miundombinu, Serikali inatarajia kutumia shilingi bilioni 143.01 kwa ajili ya ukarabati na uimarishaji wa mifereji, reli, madaraja, njia za maji, miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme, mabwawa na majengo ya umma, pamoja na kuongeza vina vya mito.
Vilevile, shilingi bilioni 15 zimetengwa kwa ajili ya ukaguzi, matengenezo na ukarabati wa barabara, madaraja na mifereji, pamoja na miundombinu ya huduma za watalii katika hifadhi za taifa, misitu ya hifadhi na maeneo ya usimamizi wa wanyamapori.
Serikali pia imetenga shilingi bilioni 1.63 kwa ajili ya kutambua maeneo yenye hatari ya mafuriko katika mabonde tisa ya mito, hatua inayolenga kuimarisha maandalizi na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Ikumbukwe, 2024 Serikali ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 830 kwa ajili ya kujenga upya na kwa ubora barabara na madaraja yalioathiriwa na mvua za El -Nino na kimbunga Hidaya nchini kote.