Serikali yatimua wanafunzi UDSM


Hili ndilo tatizo kubwa la nchi yetu. Kila kizazi kinataka kusukumizia matatizo kizazi kijacho. Mwisho wa mambo ndiyo yale ya COngo na Rwanda yanatokea bila watu kujua.
 

Wakifanya hivi watakuwa tu wanaahirisha matatizo kabla wananchi wote hawajaungana na wale wa Buzwagi kupinga uonevu huu.

Dikiteta, fisadi na muuaji Rwekaza Mukandala uko kwenye notice!
 

Nimeandika kimakosa hapo juu. Sio bungeni Dodoma, ripoti hiyo iliwasilishwa kwenye kikao cha NEC Butiama

Mawazo yangu yote yalikuwa Dodoma wakati naandika

PM
 
Nimeandika kimakosa hapo juu. Sio bungeni Dodoma, ripoti hiyo iliwasilishwa kwenye kikao cha NEC Butiama

Mawazo yangu yote yalikuwa Dodoma wakati naandika

PM

Kwi kwi kwi,

Punguza kutoa siri za vikao vya ccm na wabunge wake mkuu na pia upunguze chuki zako dhidi ya CHADEMA na mnyika na utaishi maisha safi yasio na waaaaa .... lol
 
Ni kweli tupuNilitembelea hapo mlimani mwaka 2006..na pia niligundua mambo mengi tu!Maprofessa wenyewe kazi yao kunywa pombe kuanzia asubuhi hadi jioni huku wakishinda na mabaamedi na kuwa wabishi tu by nature!..nenda groceries zote kuwanzia maeneo ya mwenge..utawakuta wakati waliotakiwa kulecture wao wanayachapa maji..they dont care coz nobody cares anyways!Mambo ni mbaya kwa sana!Na pia narudia kuwa mabadiliko yanayohitajika ni makubwa sana na sio haya mabishano ya hapa na pale kuona nani atashinda..we've got to be true and tell the truth only..KATIBA NI LAZIMA IBADILISHWE!
 

Ni ukweli mtupu ulioundika. Kwasababu hawa jamaa hawatakawia kusema kuwa wanafunzi wameharibu mali zenye thamani ya kiasi fulani, lakini kiasi hicho wala si 0.05% ya visenti au milions za waheshimiwa. Hawa wanafunzi mara moja wamewafikisha mahakamani, je vijisenti vitapelekwa lini mahakamani??
 

Kitila,
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa mgomo wa wanafunzi haueleweki kabisaa. Mambo mengine ni ya kitoto kiasi cha kujiuliza nini kimekisibu UDSM? Migomo sasa imekuwa na mfumo wa kisekondari, maana inashangaza kuwa, eti wanafunzi wamegoma na kufikia kuvunja sheria kwa vile tu hakuna maji au kwa vile a 'Ugandan' student amekataliwa kuwa kiongozi wao, how stupid is this. Are these reasons worth sucrificing their entire future? What would have happened if they had elected a different candidate? What if they had continued to register their water shortage grievances with the VC, Minister etc? Hawa wanafunzi inaonekana kabisa walikuwa na nia ya kugoma na walichokuwa wanatafuta tu ni sababu tu ya kugomea tu. This insanity has to stop. Other universities, Tumaini, Nyegezi etc., will soon outshine UDSM because of these never ending foolishness.

Kitila makes some good points but fails to conclude. Here are my takes;
  1. Wale wote walioleta vurugu wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
  2. Kutolewe elimu kwa wanafunzi, e.g. seminars, letters, n.k., kuwaelimisha nini faida na hasara za migomo, with concrete examples of those affected in the past. Waelimishwe juu ya haki ya kila mtu kugoma au kutogoma without intimidation.
  3. Intimidators wa wanafunzi wanaopingana na migomo wachunguzwe na kupewa adhabu kali ikiwemo hata kufunguliwa mashitaka. Ni muhimu kwa wanafunzi kuelewa kuwa intimidation sio demokrasia. Kama wao wanapinga serikali kutumia nguvu kuzima matakwa yao, hawana budi na wao kuacha vitendo vya vitisho kwa wanafunzi na waalimu wao wasiokubaliana nao.
  4. Chuo kisisimamishe masomo wala kubadilisha ratiba yake wakati wanafunzi wanapogoma au kusababisha chuo kufungwa. Hili liwe wazi wakati wanafunzi wanapojiunga ili waelewe consequences za kugoma.
  5. Kunapokuwepo dalili za migomo, ni muhimu kwa uongozi wa chuo kuimarisha ulinzi kwa kuongeza polisi wa doria kwenye maeneo yote ili anayetaka kugoma awe salama na yule asiyetaka naye pia usalama wake uhakikishwe. Hii itazuia tabia ya kuleta FFU baadaye wakati furugu zinapoanza au munkari wa wanafunzi unapokuwa umepanda.
  6. Mwisho ni ushauri wangu kwa wanafunzi waliomo humu mtandaoni ni kuwa, ni vizuri sana kushiriki katika siasa iwe ni CCM au upinzani. Lakini jihadhari sana kutumia imani zako za kisiasa kwenye mambo ambayo yataingiliana na ulichofuata hapo chuoni, kwani unaweza ukakosa vyote.
 

Halafu nikisema naanza kuambiwa eti nina low self esteem....inseciruty...na mambo mengine lukuki. Hivi inachukua muda gani kutatua haya matatizo ya wanafunzi...karne?
 

Mkuu, I beg to differ... Kama utawala pale UDSM ungekuwa kweli unafuata strict academic interest za chuo, kuhakikisha masomo yanafanyika vizuri, matatizo yanatatuliwa na pia kuna feedback zinazoeleweka, hakuna haja kabisa ya kuwa na migomo. kuna wakati pale UDSM migomo ilikuwa wanafunzi vs. serikali. sasa hivi imekuwa tena wanafunzi vs. uongozi wa chuo.

haya matatizo ni systemic, inabidi kuzama kwa undani kuwezakupata ufumbuzi halisi. ukiangalia mfumo pale UDSM sasa hivi ni tofauti kabisa na zamani enzi za mzee Punch. kwa hiyo ni rahisi mno kuwalaumu wanafunzi ambao wako katika mazingira tofauti na ya wakati ule, na wao pia profile yao ni tofauti.

kazi ngumu zaidi ni kuchambua vyanzo halisi vya matatizo na kuvipatia ufumbuzi. mabavu bila busara hayatasaidia kitu. Tukumbuke pia kwamba matatizo kama haya ni hasara kwa walimu, wafanyakazi, na taifa zima, sio tu kwa wanafunzi.
 
Kitila,

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa mgomo wa wanafunzi haueleweki kabisaa.

Mtu kama wewe huwezi kuelewa mambo kama haya maana una chuki kibao za kidini na kikabila


Yaani swala la kukosa maji huoni kama ni tatizo? au swala la kuingiliwa uchaguzi wao si tatizo kwako? no wonder unataka kiongozi wa ccm ndiye tu agombee uraisi.


Kwani kuna mashindano ya vyuo hapa, tatizo lako huwezi kuchukua maamuzi magumu na mtu kama wewe ukipewa nchi kuongoza unaweza kuwapa wairani na wakoloni wengine kila wanachotaka


Naona kuna mtu anaongea hapa kama president wa North Korea Kim Ill
 
Halafu nikisema naanza kuambiwa eti nina low self esteem....inseciruty...na mambo mengine lukuki. Hivi inachukua muda gani kutatua haya matatizo ya wanafunzi...karne?

Ngabu maneno hapa naona yanamgusa kabisa dikiteta, fisadi na muuaji Rwekaza Mukandala na hiyo taasisi yake ya demokrasia feki kumbe yeye mwenyewe anakandamiza demokrasia
 
wanafunzi wa UDSM wanamakosa yao mengi kama kufanya migomo kila kukicha, lakini hakumpi Mkandala haki ya kwenda kuwaachilia FFU kwao.
nimetumia neno KUWAACHILIA FFU kwa kuwa hawa FFU ni kama wale mbwa wa polisi, hawana kipimo wala hawajui kusoma picha.
ingelikuwa FFU ni watu na hawafanani na mbwa wa polisi wasingeenda kumpiga mtu mjamzito.

haya narudia tena, tume ya haki za binaadamu iliyofunguliwa kwa pozi nyingi, na vicheko tele baina ya rais na akina mama warembo waliomzunguka itachukuwa hatua gani?
au ipo kula pesa za walipa kodi tu?

na ichukuwe hatua juu ya buzwagi, UDSM ......and the list continues
 
wanashida gani wakati watoto wao wamejaa huku UK na US wanasoma colleges wakitoka huku wanawekwa bank kuu, kwanza nataka kujua watoto wa magembe wanasoma wapi,mwenye taarifa zao azilete hapa

south africa
 
Serikali ya CCM bwana, hamna wanachoweza. Matatizo UD yataisha lini, au mpaka msaada wa wataalam toka ughaibuni pia. Uzoefu wa miaka hamsini bado tu hawawezi endesha chuo.
Wanachuo kugomea kwa ajili ya tatizo sugu la maji ama kuingiliwa ktk uchaguzi wao ni sawa kabisa hasa kwa serikali isiyowajibika km CCM. Serikali ya CCM wanashindwaje kujua kua mashangingi yao, off shore accounts zao, nk, si muhimu kuliko huduma ya maji kwa binadamu, hasa kwenye mkusanyiko wa watu kama chuoni. Hamna afya bila maji.
CCM ni sumu mbaya, wanafunzi wanajua hilo lakini bado tu wataendelea kuipa kura hata 2010. CCM ndio mchawi.
 

Mimi nadhani tatizo lilianzia na Nyerere, msingi mbovu husababisha nyumba mbovu. Nyerere asingekifungua hicho chuo kabisa. Hawa viongozi wa sasa wanatelekeza lile lililoanzishwa na marehemu; hawawajibika hata kidogo kwa matatizo yanayoendelea hapo chuoni. Nyerere na yeye si aliwatimuaga wanafunzi pale, hawa wanafuata nyayo tu hawana utashi wao binafsi.
 
Kumbumkumbu zangu kuhusu mlimani, 1998 waligoma kisa posho walitaka posho ziongezwe. 2000's tumeona migomo ya kumwaga kuanzia Calculator kwa wale wa Engineering depertment, mpaka serikali itupe free money mpaka maji hayatoki so tunagoma.

Mimi nimekulia mliamani i know lini migomo hutokea, soma migomo yote utaona inatokea April to May, Jee unajua why? Because the final exam inakuja and walikuwa behind kwenye kusoma ndio wanaanzisha mgomo, wanajua watasimamishwa, then they can study. Hii plan imekuwa kwa miaka nenda rudi, kuna watu ambao wanachaguliwa special kuengineer hii migomo. That is how the system works.

Serikali imesha try strategy million of strategies lakini zimefail.

Unajua kama watu wana abuse opportunity dawa ni kutake it away from them. That is the way it works all over the world. I feel sorry kwa wale wote waliofukuzwa, i know kwamba matatizo ya wachache always yanasababisha madhara kwa wengi. That is how it works

Mimi nailaumu serikali kwa kutoweka strong rules kuhusu swala zima la kugoma. I am expect strong rules will be implimented to stop this slow bleeding. UDSM students think they're like Einsten or Newtown. They're far way from truth and reality. Life doesnt promise you anything.

That is how it works, life has never been fair.
 

I strong disagree na matamshi yako. Kama umepitia UDSM utafahamu what is inside Mlimani. Daruso students believe they're on top of everything. I know kwamba maproffesor wana matatizo yao, kuanzia maswali magumu mpaka kulikisha madesa kwa wanawake.

Chuo hakina anystrategy ya kuwaadhibisha hawa waandamanaji, the only way ni kuwatimu chuo. UDSM wame jaribu kuimpliment njia mbali mbali za kureduce migomo, lakini wanafanzi are out of touch.

Mwalim aliwatimuwa wanafunzi sababu ya migomo yao hii hii ya kipuuzi, na dharau zao za kuamini kwamba sababu wanaweza kusolve maswali ya Static then wao ni smart people on earth.

Jee unge suggest nini kama wanafunzi washawai kugoma kisa hawana calculator? Serikali ina spend million of shilling kuwafund hawa vijana, then payback yao ni kugoma. Do you know how many students wish wangepata chance ya kwenda pale mlimani? What the point ya kuwa na wanafunzi walevi, wavuta bangi, malaya, na washenzi?
If they think their grown and smart than every Tanzanian then how about paying their own school fees? Na kuachia wale wenye shida ya loan and grant.

I know serikali yetu ina matatizo, lakini kwa hili i think mchawi wetu ni hawa wanafunzi and not serikali.
 
serikali iliyoshindwa kutatua matatizo ya watoto 29 Ukraine, imeshindwa kutatua matatizo ya watoto 15 mlimani, na sasa karibu watoto 300, na by extension wasomi wapatao 10,000; yaani wanapelekana nao kila kukicha, hivi kweli tutategemea wataweza kutafuta suluhisho la madini, ufisadi n.k

Mimi naona Mlimani ndio pilot project... wahakikishe hapo kuna maji, umeme, halafu ndio tuone kama wataweza kudili na watu wengine. Serikali haiwezi kukwepa kushindwa kutatua matatizo ya Mlimani. Yaani unashindwa kumsaidia mtoto wako mwenyewe halafu unabakia kumfukuza tu kwa vile anakukera.

Hata mtoto anapokuwa mtukutu namna gani, jukumu la mzazi ni kujaribu kumpatia kila aina ya msaada wa ushauri na vinginevyo. Mara ya mwisho Mlimani kufanya semina ya ushauri, migogoro, mahusiano n.k hapo chuoni ilikuwa lini? Hivi hapo mlimani kuna projects gani za kuwasaidia vijana wanaoingia hapo kukomaa kihisia, kivionjo na kiakili? Je wanafunzi wa UDSM wanawashauri wa maisha yao na masomo?
 
Mkulu Nyani ngabu, unapoint hapa, sio kuwa tunashangilia wanafunzi kupigwa lakini matatizo ya mlimani yanachangiwa na wanafunzi wasiokuwa serious katika kufanya kilichowapeleka pale, labda other mnaweza kutupa analysis ya kujua kwanini migomo utokea wakati mitihani inakalibia, je kwa strategy hii hawaoni kuwa wanawaumiza mwaka wa mwisho ambao wanakuwa wamebakiza wiki chache kumaliza chuo.

Pamoja na hayo nalaumu nguvu kubwa iliyotuimika kuwaadabisha wanafunzi, kiasi cha kusababisha vifo, why those were unarmed kwanini kutumia nguvu kubwa namna hiyo, kwanini kuwafukuza wakati wangeweza kujadiliana nao na kumaliza hilo tatizo.

Pro. Mkandala ndo ulikuwa wakati wa kuwaonyesha watu kuwa umekomaa kiasi gani katika demokrasia kwani ungeweza kujadiliana nao na mgemaliza matatizo yenu. Kwa namna hii nahisi kusema kuwa hata watu wa CUF wakizuiwa kuandama wakaandamana utamshauri Raisi kutumia asikari kuwapiga kwa risasi za moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…