Kama mawazo ya Watanzania ni haya basi inatisha, si ajabu tukawaita wawekezaji waje kutuendeshea mambo ndani ya familia zetu. Tatizo letu ni kwamba watanzania tumekuwa wavivu wa kufikiri, tunapenda majibu rahisi rahisi, tunapenda kulaumu wengine na kukwepa wajibu wetu. Hivi kuna yeyote aliyejiuliza mchango wa wanafunzi katika sakata hili? Haya huyo aliyekuwa akilia Hall & analilia nini?ni yale yale ya utawala wa Msolla! hivi kweli Tanzania hatuna watu wenye akili timamu ambao wanaweza kukaa chini na kutatua matatizo ya Mlimani? Tuombe wawekezaji waje kutuonesha jinsi ya kuendesha Chuo Kikuu cha Taifa...?
Sisi wenyewe si wastaarabu, tunajifanya tunajua sana. Huko Ulaya umesikia lini ati Chuo kimefungwa kwa sababu ya siagi, mkate, nyama au wali? Ina maana hakuna masikini? Au Masikini wa huko hawaendi shule? Tumezidi kujiendekeza na kuiga mambo tusiyoyaweza.
Mjukuu wangu yupo mwaka wa tatu na yeye kanieleza yafuatayo:-
1. Kuna wanafunzi ambao hawataki kusoma wapo Chuoni kwa shinikizo la wazazi wao.
2. Wamefeli koziweki na wanadhani vurugu zikipelekea kufunga chuo watasalimika na kufukuzwa.
3. Wapo waliomaliza boom, hawana kitu mifukoni, wanaona wiki nne zilizobaki wataumbuka, chuo kikifungwa wakirudi nyumbani wanaweza kupata chochote kutoka kwa wazazi wao.
Na wengi katika makundi haya ni mwaka wa 1 na wa 2
Mwaka wa 3 na wa 4 kama wamo basi ni wachache sana.
Bahati njema kwangu mjukuu wangu Aggy si mmoja kati ya makundi hayo. Nashukuru Mungu. Naomba Mungu pia amalize mtihani wake.