Unajua wanafunzi wameshazoeshwa kwamba matatizo yao hayawezi kutatuliwa hadi wagome. Na ni kweli mara nyingi wakigoma hupata walichokuwa wakikitaka. So, it is the question of attitudes. Ndio yale yale tunayoongelea hapa kila siku: respect to the rule of law na ustaarabu. Ongeza na cha tatu sasa: ustahimilivu.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 101!
Jamii yetu imekuwa jamii isiyo na ustahimilivu. Hakuna patience kabisa. Wanafunzi wetu hawawezi kusibiri hata kidogo.
Kimsingi nakubaliana na wewe; lakini ningeweza kusema hivi: mtu huru anayo haki ya kukataa uovu na kutouvumilia hata kwa dakika moja ya ziada. Uovu ukivumiliwa huzaa uovu mkubwa. Ni jukumu la mtu huru kuupinga uovu (evil) na dhulma (injustice) wakati wowote utakapoonekana.
Lakini katika kupinga uovu huo, njia za kufanya hivyo ndizo zinaamua ni kwa mwendo gani uovu hupingwa. Uzito wa uovu pia huamua kama ni hatua gani zichukuliwe kwanza kupambana naye. Hivyo mtu anayekutukana akiwa ndani ya gari na wewe uko unatembea amekutendea uovu. Lakini kulikimbiza gari ili umchape vibao siyo njia sahihi. Hivyo unavuta subira. Lakini mtu akija nyumbani kwako na galoni la mafuta na kiberiti mkononi na anataka kuilipua nyumba yako, huyo anahitaji kupingwa mara moja na kuzuiliwa na siyo kuvutiwa subira.
Na kuna udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa wanafunzi. Kuna faslafa ya kijinga kwamba ukiwa kiongozi wa wanafunzi unafuata wanachosema wanafunzi. Hii ni weakness kubwa na sio maana ya uongozi. Ukiwa kiongozi unakuwa na taarifa nyingi zaidi kuliko unaowaongoza kwa hiyo lazima uonyeshe njia.
Mzee huu ni ukweli mkubwa sana ambao siyo tu kwenye serikali ya wanafunzi lakini unaweza kutolewa kwenye semina yoyote ya uongozi. Ndio maana mojawapo ya zile kanuni zangu za uongo inasema viongozi huongoza hawafuati.
Mimi nikakataa, nikawaambia sipo tayari kuongoza mgomo kwa sababu hatuwezi kuvumilia siku tatu wakati kuna watanzania wanashinda njaa kila siku. Nikawaambia wakati sisi tukisema hatuwezi kusubiri siku tatu, kuna watanzania walikuwa wamekufa na njaa kule Gairo. Nikawaambia wanafunzi wenzangu kuwa watanzania wangetudharau kwa kushindwa kuvumilia siku tatu tena tukisubiri utaratibu wa kawaida wa kibenki. Tukalumbana sana na mwisho nikwaambia kama mnaona ni lazima tuandame twende wizarani saa hiyohiyo, basi sikuwa tayari kuongoza huo mgomo na kwamba ningejiuzulu ili wachague kiongozi mwingine.
Hongera kwa hili, kwani ulifanya kitu kinachoitwa kuchukua msimamo badala ya kukubali kuyumbishwa na sauti mbalimbali na ulikuwa tayari ulipie gharama ya msimamo huo.
Baada ya hapo wanafunzi wakapoa, wakatawanyika wakabaki wachache kama 20. Nikawaambia wanafunzi walio wengi wameshanielewa. Ilipofika Jumanne wanafunzi wakapapata pesa zao na mambo yakaendelea kama mdundo. Ndio walinidharau sana siku hiyo Nkrumah na kuniona mimi ni traitor, lakini wengi walinishukuru baada ya siku tatu baada ya kutulia na ku-reflect.
veri veri gud!
Katika pointi zako za mwisho naweza kusema hivi; ni lazima tuwe na utaratibu wa kuwasaidia hawa vijana wanaoingia katika uongozi katika ngazi hizi. Wengine wana kipaji ya kuongoza lakini kipaji hicho hakijanolewa vizuri. Sijui ni lini mara ya mwisho kwa hawa vijana kupata semina ya viongozi au hata kupelekwa "ngurdoto" ya viongozi wa chuo.
Kuchaguliwa tu kwa sababu mtu anaweza kusema na anajenga hoja au kuahidi kutetea wanafunzi hakumfanyi awe kiongozi mzuri. Kujifunza tu mbele ya safari pia ni hatari na ndio maana unaoenekana huo udhaifu. Sijafuatilia profile yako, lakini naweza kusema (nisahihishe) kuwa uongozi wako pale Chuo Kikuu haikuwa mara ya kwanza watu kukudhamini nafasi ya uongozi. Na siwezi kushangaa uamuzi wako ule haikuwa mara ya kwanza kujikuta unalazimika kufanya maamuzi magumu lakini kwa watu wengi lakini ukatumia principles ulizokwisha jifunza kwenye uongozi mdogo au katika mambo yako binafsi.
Ndio maana naamini njia mojawapo ya kuwasaidia hawa vijana ni kuwaandalia vitu kama "semina ya uongozi" au semina ya "utatuzi wa migogoro" n.k Kuwaacha waende hivi na upofu kwa hakika watafanya makosa yasiyo ya lazima.