armanisankara
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 283
- 49
Serikali imetishia kuwatimua wawekezaji wa kampuni ya madini ya Tanzanite one iliyopo Mererani wilayani Simanjiro iwapo watashindwa kulipa deni la zaidi ya Dola za kimarekani milioni 2.2 zilizotokana na ukwepaji kodi.
Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alitangaza msimamo wa serikali wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini baada ya kugundulika kuwa yapo makampuni kadhaa yamekuwa yakiendesha shughuli zake za madini bila kulipa ushuru wa serikali kinyume cha sheria.
Akizungumza na Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini nchini (Tamida), jijini Arusha jana, Maswi alisema kuwa kampuni ya Tanzanite one imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya mrahaba wa madini tangu mwaka 2004 hadi 2008 na kufikia kiasi cha Sh. bilioni 3.4.
Alisema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitumia ujanja wa kukwepa kulipa mrabaha wa mauzo pale inapokuta soko la madini nje ya nchi limeongezeka na kwamba serikali kupitia kitengo cha ukaguzi wa madini ilibaini ukwepaji huo wa kodi na kuiamuru kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha au ifungashe virago.
''Tulibaini ukwepaji wa ulipaji kodi kwa kampuni ya Tanzanite one baada ya kuanzisha kitengo maalumu cha ukaguzi wa migodi hapa nchini na tulipoifikia kampuni hiyo ndipo tulipobaini imekwepa kulipa kodi kiasi hicho, na hivi sasa tunaanza kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini,'' alisema Maswi.
Alifafanua kuwa kampuni hiyo iligoma kulipa deni hilo ikidai ni kubwa sana, ndipo serikali ilipotaka kufanya ukaguzi upya lakini kampuni hiyo iligoma na kudai kuwa ipo tayari kulipa deni hilo.
Aliongeza kuwa iwapo kampuni hiyo ingegoma kulipa deni hilo serikali ilikuwa tayari kuwatimua na kuwamilikisha wazawa mgodi huo.
Kwa mujibu wa Kamishina wa madini kanda ya kaskazini, Benjamin Mchwampaka, alisema kuwa tayari kampuni hiyo imeshaanza kulipa deni hilo na kwamba hadi sasa imeshatoa malipo ya dola 200,000 zaidi ya fedha za kitanzania milioni 310, huku serikali ikiitaka kuhakikisha inamaliza kulipa deni hilo hadi kufikia jamuari mwaka 2013.
CHANZO: NIPASHE
mimi naona kama serikali inadai fedha ndogo sana [deni la dola mil. 2] kampuni kama tanzania one inaingiza millions. sasa why serikali inadai kiasi kidogo?