Serikali yatoa bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Chekereni - Kahe - Mabogini

MTANZANIA620

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
105
Reaction score
116
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohammed Omar Mchengerwa, akiwa ziarani mkoa wa Kilimanjaro ametangaza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa shilingi bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Chekereni - Kahe - Mabogini yenye urefu wa kilomita 31.25 kwa kiwango cha changarawe, pamoja na mitaro, madaraja na kuinua maeneo korofi.

Akizungumza akiwa ziarani katika mkoa huo, Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa serikali inatafuta shilingi bilioni 45 ili kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami, na amewapongeza wabunge wa eneo hilo—Mhe. Prof. Patrick Aloyce Ndakidemi na Mhe. Dkt. Charles Stephen Kimei—kwa juhudi zao za muda mrefu za kuibua changamoto hiyo bungeni kwa niaba ya wananchi.

Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia inaendelea kujidhihirisha kama serikali sikivu na tendaji, inayojibu kilio cha wananchi kwa vitendo.

Katika ziara hiyo, Waziri pia amejibu maombi ya ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Mwangaria kwa kutoa shilingi milioni 100, pamoja na shilingi milioni 120 kwa ukarabati wa shule za msingi za Mwangaria na Oria, kama alivyoombwa na Mhe. Dkt. Kimei.
 
Subirini muone mapovu toka kwa Nyumbu(CDM)
 
Back
Top Bottom