Pre GE2025 Serikali yatoa kanuni zitakazotumika kwenye Uchaguzi mkuu wa 2025

Pre GE2025 Serikali yatoa kanuni zitakazotumika kwenye Uchaguzi mkuu wa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Wakati CHADEMA ikikoleza moto wa ajenda ya No Reforms No Elections, Serikali ya Tanzania imetoa kanuni za Uchaguzi ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

===========================================================

Serikali ya Tanzania imetangaza kanuni mpya za uchaguzi kwa mwaka 2024, ambazo zinahusisha mchakato mzima wa uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani.

Kanuni hii, inayojulikana kama Kanuni ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani (Na. 1 ya Mwaka 2024), inaelekeza kuhusu mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi, pamoja na mabadiliko yoyote ya mipaka ya maeneo hayo.

Soma pia: Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024

Aidha, kanuni hiyo inatoa mwongozo wa uteuzi wa watendaji wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na wasimamizi, wasaidizi wao, na makarani waongozaji, pamoja na kiapo cha kutunza siri.

Pia kuna taratibu zinazohusu mafunzo ya watendaji hao ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unatekelezwa kwa ufanisi na uadilifu.
 

Attachments

Kutunza siri kivipi yaani kufanya siri kinyume hata na haki
 
Hapo kwenye siri kuna mengi yaliyojificha, tupakazie jicho sana.
 
Back
Top Bottom