Serikali yatoa mamilioni kwa vijana, wanawake na walemavu bila riba kujikwamua kiuchumi

Serikali yatoa mamilioni kwa vijana, wanawake na walemavu bila riba kujikwamua kiuchumi

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
Serikali yatoa mamilioni kwa vijana, wanawake na walemavu bila riba kujikwamua kiuchumi

SERIKALI wilayani Bunda mkoani Mara imetoa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali kiasi cha zaidi ya Tsh. milioni 600 zinazotokana na fedha za makusanyo ya mapato ya halmashauri na Serikali kuu.

Serikali imetoa mikopo hiyo kwa vikundi 223 vilivyowezeshwa kupitia makundi ya vijana, wanawake na walemavu katika halmashauri mbili za Bunda Mji na Bunda vijijini.

Fedha hizo zinatolewa kwa makundi hayo ya Wanawake, Vijana na Walemavu ili kuwanyanyua na kuwanufaisha kiuchumi kupitia asilimia 10 inayotolewa kila mwaka katika halmashauri mbalimbali nchini.

Kongamano hilo, lilihusisha shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake na wasichana la Kivulini lenye makao makuu yake Nyamhongoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza ambalo lilitoa mada kuhusu haki ya kupiga kura na rushwa ya ngono katika uchaguzi.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Lydia Bupilipili, amesema lengo la kukutana na vikundi hivyo ni kubadilishana nao mawazo na kujadilina namna shughuli zao za maendeleo zinavyokwenda katika vikundi vyao vya wajasiliamali.

Amesema wanakutana na makundi hayo, kuangalia changamoto zinazowakabili na kutathimini mwenendo mzima wa shughuli zao za kiuchumi walizonazo kwenye vikundi vyao.

Bupilipili amesema mwaka 2019, walikutana na vikundi vya wajaslimali na mwaka huu pia wamekutana nao kuangalia kwa mara nyingine kama kuna vikundi ambavyo vinakosa mikopo licha ya kukidhi vigezo na kuondoa urasimu uliopo wa baadhi ya vikundi kujirudia kupewa mikopo.

"Leo tumeona kuna vikundi 223 vimekopeshwa kiasi cha Tsh. Milioni 665 kwa miaka mitano haya ni mafanikio makubwa kwani kabla ya mwaka 2015 hakuna vikundi vya walemavu vilivyokuwa vinapata mikopo.

"Pamoja na vikundi vingine kueleza changamoto kwamba kuna vikundi havipata taarifa za mikopo, tunataka kufuatilia hao ambao hawapati taarifa wapate habari na wao waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali.

"Tunataka kuona watu wote wananufaika na serikali yao imeweza kukitoa na kukiweka utaratibu wa wao kunufaika nina imani wana shughuli zao kiuchumi lakini haviendani na kile walichonacho lazima iwanyanyue ikizingatia tupo uchumi wa kati," amesema Bupilipili.

Bupilipili amesema uchumi wa kati unahitaju watu kufanya kazi kwa bidii kwani uchumi wa kati hauhitaji uzembe hivyo unahitaji watu kuwezeshwa kama Serikali ya chama cha mapinduzi kinabyowawedhesha wananchi wake.

Hata hivyo katika kongamano hilo la vikundi vinavyonufaika na mikopo ya halmashauri hizo za Bunda Mji na Bunda vijijini, mkuu huyo hakusita kuwagusia na kuwakumbusha kuhusu uchaguzi mkuu wa 2020.

Bupilipili aliwashauri wanufaika hao wa mikopo, kuchagua viongozi bora na viongozi wenye Sera za kutoa mikopo kwa makundi hayo kwakuwa vipo vyama vingine ambavyo Sera zao hazionyeshi dira ya kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu.

Kwa upande wake, mdau wa maendeleo wilayani humo, ambaye alialikwa kutoa elimu ya rushwa ya ngono hususani kwa wanawake, Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Kivulini, Yasin ally alitaka kuchagua viongozi sahihi.

Yasin alieleza kuwa, wanapaswa kutumia haki ya msingi ya kupiga kura kuchagua viongozi sahihi kuanzia ngazi ya madiwani, wabunge na nafasi ya Urais ili kwenda kutatua kero mbalimbali za maendeleo.

Yasin aliwasisitiza wanawake kutumia fursa hiyo ya kupiga kura kutokana na wao ndio wahanga wakubwa na ambao ni wasimamizi wa familia zao na wasifanye kosa la kuacha kupiga kura kuchagua viongozi wanaofaa.

Afisa maendeleo ya Jamii Bunda Mji, Corman Moshi amesema katika kipindi cha miaka mitano wametoa kiasi cha Tsh. Milioni 315 kwa vikundi 126.

Amesema fedha hizo zimetolewa kwa vikundi vya wanawake 65, vijana 48 na walemavu 13 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015 - 2020.

Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Mary Chacha amesema fedha zilizotolewa na Serikali zimewasaidia kwa kiasi kikubwa kujikwamua kiuchumi huku akiiomba Serikali kuongeza kiwango cha mikopo kwani zinazotolewa kwa sasa ni kidogo ikilinganishwa na idadi ya watu waliopo kwenye kikundi.


Mwisho
IMG20200909112130.jpg
IMG20200909112216.jpg
IMG20200909112220.jpg
 
Tundu Lissu chaguo la Mungu!

Yaani kwa kampeni zake za wiki mbili tu ajira 13,000 zimetolewa! je akiwa rais ajira ngapi zitazalishwa?

Pia ni mtanzania wa kwanza ku survive baada ya kupigwa risasi 16!

Naamini kuna dhumuni la Mungu kumponya!!
 
Utaratibu ni very simple,

Mnasajili kikundi,

Mnaandika malengo ya kikundi.

Vijana tunapaswa kuchangamkia hii nafasi.

Wakuu wa Wilaya pia wanapaswa kuwataarifu wananchi juu ya upatikanaji wa hii fursa.
 
Back
Top Bottom