Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Soda na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.
===
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mh. Ashatu Kijaji ametoa siku tatu kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji baridi nchini ambapo pia ametoa siku saba kwa Tume hiyo kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na hatua ambayo Tume hiyo imechukua kuhusiana na kupanda kwa bei hizo.

Chanzo: ITV habari
 
Waziri wa Viwanda ameagiza Tume ya Ushindani wa Biashara, katika siku 3, wampe taarifa ya upungufu wa vinywaji baridi (TV habari leo). Najiuliza kama inawezekana katika siku 3 kufanikisha hilo.

Serikali ina vyombo vingi ambavyo ingevitumia iwapo kweli ingekuwa na nia ya dhati ya kushughulikia upungufu huo. Kwa mfano ingeweza kutumia Maafisa Biashara na kupata taarifa iliyo sahihi na kamili za kuiwezesha kuchukua hatua.
 
FRY.jpg
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Sida na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.

Source: ITV habari
What is INSANITY?
 
Haya maagizo huwa ni ya kijinga hata kama yana Nia njema kwa sababu vyote hivyo havijapanda kwa sababu za ndani bali ni sababu za kushuka kwa uzalishaji wa malighafi Duniani,ushindani na mambo freight charges..

So hao fcc ndio watafanya nini sasa ?
 
Soda ni anasa hata kujenga nyumba ni anasa pia...acheni bei ipande tu ! 🐒
 
Back
Top Bottom