Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Soda na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.
===
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mh. Ashatu Kijaji ametoa siku tatu kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji baridi nchini ambapo pia ametoa siku saba kwa Tume hiyo kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na hatua ambayo Tume hiyo imechukua kuhusiana na kupanda kwa bei hizo.

Chanzo: ITV habari
View attachment 2085855
Ha ha ha siku zooote hizo wamekaa kimya. Wameona hali mtaani si hali approval ratings zimeshuka sana wanaanza kujikosha!
 
Tatizo ni mfumo wa siasa unatumika kwetu ni wa kizamani .mtu kutoa ahadi za uongo na kutotekeleza Kama ilani za vyama vyao umekuwa Jambo la kawaida .. na wengi wanaoingia kwenye siasa bado Wana upeo huo. Inahitajika external force kuvunja hiyo kitu
 
Back
Top Bottom