Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amezipa siku 30 taasisi za umma zinazodaiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) zilipe shilingi bilioni 30 ndani ya mwezi mmoja.
Dk Ndugulile alitoa agizo hilo jana alipotembelea TTCL na kuzungumza na wajumbe wa Bodi, menejimenti na wafanyakazi wa shirika hilo Dar es Salaam.
Alisema, zaidi ya taasisi 20 za Serikali zinadaiwa na TTCL zaidi ya shilingi bilioni 30, na kwamba, zipo taasisi zinazotumia huduma za shirika hilo na zinakusanya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwezi ila hazipo tayari kulipa huduma za TTCL. Dk Ndugulile pia alitoa onyo kali kwa kampuni zinazohujumu miundombinu ya TTCL ili ishindwe kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja wake.
Alisema, wanaoiba nyaya za shaba za TTCL na kuuza kama chuma chakavu nao waache mara moja kwa kuwa watahusishwa na uhujumu uchumi kwa kudhoofisha utendaji kazi wa TTCL.
Aliwataka watendaji wa Wizara kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufanya utafiti na tathmini ya kubaini mchango wa sekta ya mawasiliano aidha wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja katika kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew aliwataka watumishi wa TTCL kuwa wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wajenge utaratibu wa kufuata na kuwahudumia wateja waliko badala ya kuwasubiri ofisini.