Serikali yatoa siku 7 ipatikane suluhu bei ya Saruji (Cement)

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Serikali imewapa siku saba wazalishaji wa saruji nchini kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto ya kupanda kwa bei na upatikanaji wa bidhaa hiyo katika soko.

1787073009945.png

Magizo hayo yametolewa na ayo yametolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, alipokutana na wamiliki wa viwanda vya saruji kujadili sababu za upungufu wa bidhaa hiyo na kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini.

Soma: Nasikia Cement imepanda hadi kuuzwa Sh 22,000 kwa mfuko. Mtaani kwenu mnanunua kwa bei gani?

Balozi Salum amesema Serikali inataka wazalishaji kufanya tathmini ya kina kuhusu changamoto zinazoathiri uzalishaji, usambazaji na bei ya saruji, kisha kuwasilisha mapendekezo yatakayosaidia kupata suluhisho la kudumu.

“Tunataka kupata suluhisho litakalowezesha saruji kupatikana kwa wakati na kwa bei inayozingatia maslahi ya wazalishaji, wafanyabiashara na wananchi. Siku hizi saba zitumike kufanya tathmini ya kina na kuwasilisha mapendekezo yenye utekelezaji,” amesema Balozi Salum.

Kikao hicho kimewakutanisha pia wadau muhimu katika mnyororo wa saruji, wakiwemo Tume ya Ushindani (FCC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), TanTrade pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Hatua hiyo inakuja wakati saruji ikiwa miongoni mwa bidhaa muhimu katika sekta ya ujenzi, huku mabadiliko ya bei na upatikanaji wake yakigusa gharama za miradi ya ujenzi kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji.
 
Huwezi mbana mfadhili wako maishani.
 
Back
Top Bottom