Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakulima wa zao la Vanilla Mkoani Kagera wameendelea kuiomba Serikali kuingilia kati kuwasaidia kupata malipo yao ya zao hilo walilouza kwa Kampuni ya Sosaka Limited.
Imeelezwa kuwa Kampuni hiyo ilifuata taratibu zote na kupata vibali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, ikanunua Vanilla kutoka kwa Wakulima zaidi ya 800 ambapo ilinunua zaidi ya Tani 80 na Wanadai zaidi ya Tsh. Bilioni 1.
Mauzo ya zao hilo yalifanyika Julai 19 hadi 23, 2023 kwa ahadi kuwa malipo yatafanyika siku chache baada ya Mnunuaji kukamilisha manunuzi, akaanza kulipa wachache baadaye akasitisha zoezi kwa ahadi kuwa malipo yatafanyika siku chache baadaye.
Malalamiko ya awali kuhusu kilichotokea soma hapa - Wakulima wa vanilla Kagera kutapeliwa na kampuni ya SOSAKA
Ufafanuzi wa Serikali
Akizungumzia changamoto hiyo, Toba Alnason Nguvila ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Kagera anasema:
"Kwanza bei ya Vanilla imeshuka Duniani kote, sio Tanzania pekee hata katika Nchi nyingine, ilizoeleka kununua Tsh. 10,000 hadi 15,000 kwa Kilo moja, huyo wanayemsema (Kampuni ya Sosaka Limited) Wakulima ameshindwa kupata soko mpaka sasa na ndio maana amekwama kupata fedha ya kuwalipa Wakulima.
"Serikali imechukua hatua, Mkuu wa Mkoa alimuweka ndani mhusika na baadaye Jeshi la Polisi likaendelea na uchunguzi, tunachukua kama utapeli kwa kuwa umefanya kazi na Wakulima kisha ukashindwa kuwalipa fedha.
"Taratibu za kwenda Mahakamani zinaendelea wakati huohuo Vanilla zenyewe zimeshikiliwa, zimehifadhiwa sehemu salama, hazijatoka nje ya Mkoa.
"Hakuna Mkulima ambaye Vanilla zake zimeuzwa au kupotea, zipo isipokuwa fedha ndio changamoto, akitokea mwingine mnunuzi aje atanunua ili kuokoa changamoto hiyo inayoendelea.
"Vanilla ni zao jipya ndio maana linaendana na changamoto kadhaa."