Serikali yatoa ukomo kukaimu nafasi kwa watumishi

Serikali yatoa ukomo kukaimu nafasi kwa watumishi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
1578468366656.png

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwajelwa, alisema Serikali baada ya kugundua kuwapo kwa uozo kwa watumishi mbalimbali wanaokaimishwa nafasi waliamua kuja na waraka unaoelekeza kikomo cha mtumishi kukaimu katika nafasi husika.

Dk. Mwanjelwa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

“Suala la kukaimu kwa muda mrefu ndiko kuna sababisha kuwepo na uozo mkubwa katika sehemu zetu za kazi kutokana na watendaji hao kutokuwajibika kwa ufanisi,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Aliwataka watumishi wote wa halmashauri, hususani mkurugenzi na wakuu wa idara kufanya kazi kwa ushirikiano, ikiwa ni pamoja na kupokea ushauri wa kitaalamu unaotolewa na alisisitiza suala la mafunzo katika kazi ili kuwaongezea ujuzi watumishi hao.

Katika ziara hiyo mbali na kukutana na kutatua kero mbalimbali za watumishi katika halmashauri za Mkoa wa Singida, pia anapitia kuangalia utekelezaji wa Mpago wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf).


Chanzo: Mtanzania
 
Mbona hatuoni ukomo katika bandiko lako??, Uandishi nusu nusu unatunyima taarifa muhimu maana hapa nilipo nimekaimu mwaka wa pili sasa
 
Back
Top Bottom