Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katambi amesema jumla ya madereva 65 waliwasilisha malalamiko kuhusu kufungiwa leseni zao kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani, yakiwemo mwendokasi, kuyapita magari mengine bila tahadhari na uendeshaji wa uzembe. Amesema madereva 13 wametakiwa kufika kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Oktoba 9, 2026, huku wengine wakipangiwa utaratibu wa kushughulikiwa kwa makundi.
Aidha, amesema madereva wanane wameelekezwa kufika katika ofisi za Kikosi cha Usalama Barabarani kwa taratibu za kurejeshewa leseni zao, huku madereva 52 wakitarajiwa kuitwa Novemba 1, 2026. Hata hivyo, amesisitiza kuwa Serikali haitakuwa na muhali kwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali, huku akibainisha kuwa mfumo wa nukta katika leseni za udereva bado uko katika kipindi cha majaribio na utoaji elimu.
Soma pia