Serikali yatoa wito kwa Madereva waliofungiwa Leseni zao kuzifuata

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Your browser is not able to display this video.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa wito kwa madereva kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani baada ya kushughulikia mashauri ya madereva waliowasilisha malalamiko yao wakati wa changamoto ya madereva wa mabasi iliyotokea Septemba 29, 2026, katika maeneo mbalimbali nchini.

Katambi amesema jumla ya madereva 65 waliwasilisha malalamiko kuhusu kufungiwa leseni zao kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani, yakiwemo mwendokasi, kuyapita magari mengine bila tahadhari na uendeshaji wa uzembe. Amesema madereva 13 wametakiwa kufika kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Oktoba 9, 2026, huku wengine wakipangiwa utaratibu wa kushughulikiwa kwa makundi.

Aidha, amesema madereva wanane wameelekezwa kufika katika ofisi za Kikosi cha Usalama Barabarani kwa taratibu za kurejeshewa leseni zao, huku madereva 52 wakitarajiwa kuitwa Novemba 1, 2026. Hata hivyo, amesisitiza kuwa Serikali haitakuwa na muhali kwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali, huku akibainisha kuwa mfumo wa nukta katika leseni za udereva bado uko katika kipindi cha majaribio na utoaji elimu.

Soma pia
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…