The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
"Mhe. Spika imeelezwa pia bei ya kuunganisha umeme vijijini na Mijini. Nieleze la kwanza kwamba bei ya kuunganisha umeme ni shilingi 27, 000 vijijini na kwenye Vijiji miji. Serikali inaendelea kuunganisha umeme kupitia mpango wa National energy Compact na kwa mwaka 2025/26 serikali kupitia REA imetenga shilingi Bilioni 40 ili kuanza kuunganisha umeme wananchi kwa shilingi 27,000 kwenye maeneo mbalimbali yenye sura ya Vijiji miji.
Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya wastani wa asilimia 58 za gharama ya kuunganisha umeme kwa wananchi lakini wananchi hulipia kiasi fulani ambacho bado wananchi wamesema ni kikubwa. Mhe. Spika baada ya kuwa tumejadili suala hili kwenye kamati, tuliamua kuunda kamati kwasababu Mhe. Spika hili ni jambo linalohusiana na uchumi, linahosiana na fedha, haliwezi kutamkwa bila uchambuzi."
Nawaomba waheshimiwa Wabunge kwa heshima na unyenyekevu, mtupe muda, kuna timu tumeunda ya kwenda kuangalia namna gani tutapunguza gharama ya kuwaunganisha wananchi vijijini kwaajili ya kuwapelekea umeme."
Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Dotto Biteko akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara ya nishati kwa mwaka 2025/26.