Serikali yaunda timu kufanya tathmini bei kubwa uunganishaji umeme

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
"Mhe. Spika imeelezwa pia bei ya kuunganisha umeme vijijini na Mijini. Nieleze la kwanza kwamba bei ya kuunganisha umeme ni shilingi 27, 000 vijijini na kwenye Vijiji miji. Serikali inaendelea kuunganisha umeme kupitia mpango wa National energy Compact na kwa mwaka 2025/26 serikali kupitia REA imetenga shilingi Bilioni 40 ili kuanza kuunganisha umeme wananchi kwa shilingi 27,000 kwenye maeneo mbalimbali yenye sura ya Vijiji miji.

Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya wastani wa asilimia 58 za gharama ya kuunganisha umeme kwa wananchi lakini wananchi hulipia kiasi fulani ambacho bado wananchi wamesema ni kikubwa. Mhe. Spika baada ya kuwa tumejadili suala hili kwenye kamati, tuliamua kuunda kamati kwasababu Mhe. Spika hili ni jambo linalohusiana na uchumi, linahosiana na fedha, haliwezi kutamkwa bila uchambuzi."

Nawaomba waheshimiwa Wabunge kwa heshima na unyenyekevu, mtupe muda, kuna timu tumeunda ya kwenda kuangalia namna gani tutapunguza gharama ya kuwaunganisha wananchi vijijini kwaajili ya kuwapelekea umeme."

Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Dotto Biteko akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara ya nishati kwa mwaka 2025/26.

 

Attachments

  • 1746001143440.png
    566.3 KB · Views: 35
Ing
Ingependeza ipungue,iwekwe kwenye service charges ili wengi wafungue viwanda vya kati na vya juu kwa gharama nafuu na kuongeza ajira nakulipa kodi.
 
Nchi imekaa matapeli yaani unaunda tume ya kujadiri kwanini gharama ni juu? Huu ni uhuni
 
Daah!!
 
Sijaona popote ulipozungumzia habari ya kupungua bei ya kuunganisha umeme mjini!

Sasa hao wa vijijini si tayari washapunguziwa, bado gharama hiyo ni kubwa au?

Sisi wa mjini kipindi cha mwaka wa mwisho wa Magufuli walitushushia hadi 27 kama wenzetu wa vijijini.

Mwamba alivyokufa tu, kwanza wakatumbua Kalemani aliyeibeba sera hiyo ili wanapoua nyani wasimwangalie usoni wakajisikia vibaya!
 
Kuna vitu vinatia kinyaa
 
Hadi bungeni wanaleta siasa za majukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…