Serikali yaunda Tume kuchunguza Ufisadi Tanesco

Serikali yaunda Tume kuchunguza Ufisadi Tanesco

tume inayochunguza 1.4bil inaweza yenyewe ikala 600m! second hatujashuhudia kazi ya tume ikifanyiwa kazi unless kuwe hakuna maslahi ya wakubwa. eg ya kina mwakyembe jamaa aliiunda maksudi kuwafisha upande wa pili, sio kuwa imezaa matunda,why mambo muhimu km tume ya warioba, nyalali, kisanga hazijafanyiwa kazi? migodini etc! ni kudanganyana km watoto, hapa onatakiwa umekwenda kinyume na maadili out na kufilisiwa, kwani watz kibao kutake over, next yrs tunachapa risasi km china!!
 
Na Kizitto Noya, Dodoma

SIKU moja baada ya Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa kuibua ufisadi wa Sh1.4 bilioni ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), serikali imeunda tume kuchunguza tuhuma hizo.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliliambia gazeti hili jana kuwa tuhuma hizo ni nzito na hawezi kuacha zikapita bila kuzifanyia kazi.

"Mimi ndiyo kwanza nilizisikia bungeni na kimsingi nilipigwa butwaa, lakini sasa nimeanza kulishughulikia suala hilo kwa kuunda kamati ya uchunguzi," alisema Ngeleja na kuongeza;

"Ninaamini kazi kubwa, lakini haitakuwa nzito sana kwani mheshimiwa mbunge ametusaidia kwa kutaja namba za nyumba zinazohusika".

Ngeleja ambaye hakutaja idadi ya wajumbe wanaounda kamati hiyo wala muda watakaotumia kukamilisha kazi hiyo, alisema anaamini uchunguzi huo hautachukua muda mrefu.

Alisema kwa kuwa suala hilo limeibuliwa bungeni, ataweka matokeo ya uchunguzi huo hadharani ili wananchi wajue ukweli wake.

"Of Course (kwa ujumla) tuhuma hizo ni nzito, lakini siwezi kusema lolote zaidi ya kueleza kuwa ninazifanyia uchunguzi. Kazi imeanza leo (jana) na kwa sababu suala hilo limeibuliwa bungeni, tukimaliza kazi tutaijulisha jamii," alisema Ngeleja.

Juzi jioni wakati akihitimisha mjadala wa wizara yake ya Nishati na Madini, Waziri Ngeleja aliliambia Bunge kuwa tuhuma hizo ni changamoto kwake na kwamba anajipanga kuishughulikia mara moja.

Aliliambia Bunge kuwa anathamini mchango wa mbunge huyo na kwamba isingekuwa rahisi kwake kufahamu jambo hilo kwa kuwa kinachoiunganisha wizara yake na Tanesco ni Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

Juzi mbunge wa Sumve Richard Ndassa aliibua ufisadi katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kulieleza Bunge kuwa shirika hilo liko katika harakati ya kuiuza kwa Sh60 milioni nyumba namba 13 iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam, mtaa wa Toure/Chaza line baada ya kuikarabati kwa Sh 600 milioni.

Sambamba na ufisadi huo, pia Shirika hilo linatuhumiwa kutumia Sh1.4 bilioni kukarabati nyumba sita za wakurugenzi kinyume na taratibu.

Ndasa alitoa tuhuma hizo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa Jumamosi iliyopita na waziri wake William Ngeleja.

More : www.mwananchi.co.tz

BJ: Tume, Tume, Tume kila mara bila matokeo ya hizo tume!.Inakera
Aliliambia Bunge kuwa anathamini mchango wa mbunge huyo na kwamba isingekuwa rahisi kwake kufahamu jambo hilo kwa kuwa kinachoiunganisha wizara yake na Tanesco ni Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.


Hapa Waziri najua unapendekeza wajumbe wa bodi. pia kamishna wa nishati lazima awe kwenye hiyo bodi. Ina maana hukuambiwa hili na bodi au halikupata baraka za bodi?
 
Dada Belinda, kwa maoni yangu tume ya nini?. Hayo matumizi ya Tanesco yanatawaliwa na sheria, taratibu na kanuni. Kama sheria zilifuatwa tatizo liko wapi?. Kama zilikiukwa ni suala la uwajibikaji, kuna mahali Tanesco inawajibika, wahusika wawajibishwe. Tume ya nini hapa?/
Kama sheria zimefutwa, hakuna cha ajabu kukakarabati nyumba kwa milioni 600 na kitoa sadaka kwa boss kwa kifuta jasho cha milioni 60.
Mbona zile nyumba za oysterbay walizojiuuzia wakubwa, wameuziwa kwa milioni 2-4. ofisi zao zikawakarabatia kwa mamilioni. Thamani ya viwanja vywenyewe tuu ni zaidi ya bilioni, cha muhimu ni jee sheria taratibu na kanuni zilifuatwa?. Hivi kweli tunaunda tume kuchunguza the obvious!? its a waste of time and money.
 
Yaani huko Tanesco kuna uozo kweli kweli wa ufisadi, naomba tu hiyo tume iundwe ili angalau ufisadi upungue.
Pretty,
Tume ngapi zimeundwa na bado zikatetea ufisadi? Siamini kama tume zinasaidia kupunguza ufisadi, badala yake ni ufisadi juu ya ufisadi.
 
Rev, Ngeleja, Management yote ya ya juu ya TANESCO na Bodi ya Wakurugenzi wote hawa wanastahili kufukuzwa kazi mara moja kutokana na uozo uliojaa pale TANESCO, lakini tuna Rais ambaye ni muoga anaogopa kufanya maamuzi mazito ambayo yataungwa mkono na Watanzania walio wengi.

Halafu mwenyewe haoni kama kazi imemshinda ili akae pembeni katika kinyang'anyiro cha 2010 na wako wasioitakia mema nchi yetu wameshaanza kumpigia debe pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha jamaa kazi imemshinda kabisa.
Mnanichekesha kweli mnapomuita ni rais mwoga kuchukua hatua.
Ukweli ni kwamba si mwoga bali ni rais mshiriki kwa asilimia mia moja katika ufisadi huu. Sasa atajisurubu mwenyewe?
Mbona hamuelewi?
 
Ni kupoteza fedha za walipa kodi kuunda tume juu ya tume zilizokwisha maliza kazi na kutoa ushauri ambao mpaka leo haujatekelezeka.
Kuna Mkuu ameuliza hivi huko majuu wanafanyaje? Swali zuri sana. Nchi zenye utawala unaofuata sheria sawasawa haihitaji kuunda tume kwa mambo kama haya, Taasisi mfano kamaTakukuru ilitakiwa iwajibishwe mara moja, ndiyo maana ya kuwepo hiyo taasisi, sasa tume za nini tena? hizi tume nyingine huongeza hata muda wa kazi kuendeleza ulaji. Bongolalalaaaaa!!
 
Back
Top Bottom