Serikali yavunja mabanda ya wafanyabiashara stendi ya Kawe usiku

Serikali yavunja mabanda ya wafanyabiashara stendi ya Kawe usiku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali imevunja vibanda vya wafanyabiashara wadogo waliokuwa wanafanya biashara hizo katika stendi ya Kawe. Hali ya kushangaza mabanda hayo yamevunjwa usiku na kwa sasa polisi wanaranda kuona kama kuna ghasia yoyote kutokana na tukio hilo

Japo kuna raia walioathiriwa na tukio hilo kwa vitu vyao kupotea, kuharibiwa au kuibwa, wananchi wamesema walipewa tangazo la kuhama siku tatu zilizopita lakini wamedai hawakuoneshwa sehemu ya kwenda kufanya biashara.

Ni wangapi wanarudi kwenye umasikini
1644384310414.png

1644384335776.png
 
Mbeya hawakuvunja.

Walihamisha mabanda yote usiku. Asubuhi watu wanafika kijiweni hawakuti mabanda.

Wakagewa tangazo kila mmoja afuate mali zake jiji.

Kwanini approach kama hii haikutumiwa?
 
Kumbe bado inaendelea! TTCL wakaweke nguzo yao sawa naona imelala hapo..
 
Mbeya hawakuvunja.

Walihamisha mabanda yote usiku. Asubuhi watu wanafika kijiweni hawakuti mabanda.

Wakagewa tangazo kila mmoja afuate mali zake jiji.

Kwanini approach kama hii haikutumiwa?
Kwahiyo walipofuata kila mmoja alipata mali zake?
 
Back
Top Bottom