Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine



WAZIRI WA ELIMU YA JUUU ANAVIMBA MASHAVU ITABID TUMUITE WAZIRI MASHAVU



HAWA SIDHANI KAMA WANA HATA HILO CHOZI LA KUILILIA NCHI YAO



JE KUNA HAJA YA KUWA NA HII PASSPORT???


TUKUBALI SERIKALI IMESHINDWA JE WAKO WAPI HAWA:

JAMAL MALINZI

REGINALD MENGI

FREEMAN MBOWE

HAWA NDIO TUNAAMBIWA NI WAFADHILI WAKUBWA KWETU KWA KUJITOLEA MBONA NAO WAKO KIMYA?
[/QUOTE]
 
Mwaka 2004 nilikuwa natoka Stuttgart Germany naelekea Brussels kwenye high way nchini ujerumani nikasimama kununua mafuta nikavamiwa na hawa sikin head ni wabaya . Kilicho niokoa ni kuongea Kiingereza kwa kasi ya ajabu na kusema nikiifikia gari yangu na kutoa bunduki nitawa shoot wote . Wakiwa wanashangaa nikatimka nakuingia kwenye gari na kuiwasha mmoja akaja mbele kuzuia gari nikamvunja mguu na kuondoka .Hatari naijua na nasema poleni sana vijana wa Ukraine
 
Aaaah we Lunyungu hebu acha hizo bwana. Eti uliongoea Kiingereza kwa kasi ya ajabu.....usikute wala hawakukuelewa ulichokuwa unazungumza kwa sababu ya accent nzito. Acha kuleta masihara bwana
 
Nyani Ngabu umenifanya nicheke ktk uchangiaji wako kwa Lunyungu...Let us do what we is best...najaribu kuwa-email watu wa aljazeera international tuona kama nawao wata-respond..au...maana naona sky news wapo kimya? Vipi Said Yakubu na BBC mie sijasikia hadi sasa?....
 
Chuma BBC niliwapa habari na contacts zote since last week!! VOA nimewapa habari jana na leo wamewaweka vijana hewani!!! now you tell me!!
 
Kuna mtu anayeweza kuwasiliana na Abubakar Lyongo wa Deutche Welle?
 
Kuna mtu anayeweza kuwasiliana na Abubakar Lyongo wa Deutche Welle?

Deutsche Welle
Kiswahili Redaktion
53110 Bonn
Deutschland

Tel. : +49 228 429-4148
Fax : +49 228 429-4915
E-Mail: kiswahili@dw-world.de

IPS-Inter Press Service International Association
Via Panisperna, 207
00184 Rome
Italy
Email: headquarters@ips.org
Tel: +3906 485692
Fax: +3906 4817877

Nimejaribu kutafuta NHK World Radio(swahili) contact zao lakini nimekosa Ila nimepata hii hapa I hope itasaidia

Fax: +81-3-3481-1350
Email: info@intl.nhk.or.jp
 
jamani wanaJF ebu naomba muelewe kitu kimoja, serikali hadi sasa imeshindwa kulipia wanafunzi wa UDSM, ikawa habari nzito kweli mpaka vyama vya upinzani vikaingilia, lakini hadi sasa serikali haijafanya chochote ndio kwanza ikachukua hatua ya kuwalipisha faini ili warudi madarasani, sasa mnaniambia serikali hiyo hiyo inaweza ikawalipia wanafunzi hao wa ukraine ? ebu niambie ikifanya hivyo, serikali itaeleweka vp ? naelewa sana matatizo wanayopata hawa wanafunzi, i understand that. lakini basi tusiangalie upande mmoja, lets look @ both ways !
that being said, sidhani na sina moyo kabisa kama serikali hii hii iliyoweza kukalia kimya kilio cha wanafunzi wa mlimani ikaweza kusikiliza kilio cha hawa wanafunzi wa ukraine. therefore, kilichobaki ni either warudi nyumbani AU mpitishe michango kwa wabongo wote walio ughaibuni ( it might OR might not work ) sidhani kama watu watakuwa na moyo huo wa kuchangia pesa zooote kwa ajili ya wanafunzi woote hao na kwa muda wote huo pamoja na pesa za chakula, malazi, hospitali, usafiri n.k !!
AU njia ya 3 kama hiyo ya kwanza haitafanya kazi ( yaani wanafunzi warudi nyumbani ) na ya pili haikufanya kazi, which am pretty sure it wont work ( hiyo ya fundraising ) basi tunaweza kuendelea na hiyo kampeni ya kusema huyo dk. msolla ( sijui kama ndiye yeye ) ajiuzulu !!

Remaining option kubwa ni wao kurudi nyumbani tu !!
 
Hebu tujiulize maswali manne tu:

(a) Bajeti ya elimu ya juu kwa mwaka huu wa fedha ikikuwa ni kiasi gani?
(b) Bajeti ya Ikulu nayo kwa mwaka huu pia ilikuwa ni kiasi gani.
(c) Hadi sasa Elimu ya juu imeshatumia kiasi gani na kubakiwa na kiasi gani?
(d) Ikulu imehstumia kiasi gani na kubakiwa na kiasi gani?
 
tetesi zinazonifikia ni kuwa serikali ina ukata mkubwa...! why? I don't even want to guess
 
tetesi zinazonifikia ni kuwa serikali ina ukata mkubwa...! why? I don't even want to guess

Matumizi ni makubwa na yasiyo na mpangilio. Kwa kifupi, kama hamjashtuka ni kwamba, tumerudi kwenye enzi za RUKSA! Kama serikali imejaa mawaziri na watendaji ambao wote wamewekwa kwa sababu ni washkaji au tu walikuwa wapiga debe wazuri kipindi cha kampeni, unategemea nini?

Hawawezi hata kukemewa na aliyewateua! Inasikitisha sana, na mbaya zaidi, inakatisha tamaa!
 
Suala la wanafunzi wa Ukraine, leo limeanza kuchukua sura mpya kabisa. Kwanza kabisa, hali ya wanafunzi bado haijatengemaa na familia zimeshajulishwa.

Baada ya kufanya uchunguzi wa kina. Tunaweza kuripoti kwa mamlaka kuwa serikali ya Tanzania ina kigeugeu na yenye kuonesha upendeleo mkubwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao wana uwezo wa "kupenyeza rupia". Mara nyingi mmesikia tukisema ni wanafunzi 29 walio matatani. Leo naweza kuthibitisha pasipo shaka kuwa tangu sakata hili lianze vijana wetu walijitahidi mara nyingi kuwasiliana na wizara, bodi na viongozi mbalimbali. Vifuatavyo ni baadhi ya vielelezo na vingine vinazidi kumiminika kuthibitisha kuwa vijana hawa wamebaguliwa kwa sababu moja tu, WAZAZI WAO HAWAKUWA NA UWEZO WA KUPENYEZA RUPIA!

A: Barua ya kuthibitishwa kupokelewa na mamlaka huko Ukraine na barua hii inaeleza wazi kuwa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kuingia 2005/2006 zinashikiliwa hadi 2006/2007



 
B:Baada ya kufika kule Ukraine, vijana hawa wakaandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kuulizia mikopo yao. Kama unavyoweza kuona nakala ya barua hii ilitumwa kwa Rais, Waziri, na Balozi Chokala



 
C: Barua kwa Mkurugenzi bodi ya Mikopo. Barua inaelekezwa kwenye bodi kuwapatia maelezo kuhusu baadhi ya wanafunzi wote 65 ambao walisaidiwa kupata nafasi hizo za vyuo na Ukraine Educational Fund.



 
Tafadhali endelea kufuatilia thread hii.. kwani ushahidi zaidi unazidi kumiminika..!! KLH News Exclusive, bring you news when no one else dares!! because we care!!
 
Kwa mtindo huu tutafika? kama baba yako hana rupia za kupenyeza ndio basi tena. Tena vijana wanasoma kozi ambazo zitakuwa na manufaa sana kwa taifa letu. Duh hii kali.
 
Kweli thats a reality check kwa wale wote ambao ni watoto wa wakulima (wapiga kura!) Its sad kweli kuona umaskini ndo unakuhukumu! Yet hata juhudi za kujikwamua wachache wanazididimiza! Ohhh....Good work mwanakijiji..tenda wema...usisubiri shukrani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…