Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Tatizo la Mh. President kukaa kimya ni kwamba bajeti hairuhusu tena kutumia pesa zaidi..... mpk sasa serikari imeshatumia bajeti ya miaka miwili zaidi.....kwa kipindi kifupi sana.... hivyo wameamua kuwakopesha pesa za nauli na wakirudi warudishe!! swali je hizo hela za kuirudishia serikari watazitoa wapi wakati wo wenyewe bado wanafunzi na hata kujilipia ada tu wameshindwa????
 
Nyani Ngabu,

Wazo zuri sana. Mwanakijiji kama umekubaliana nalo nakuomba tazama PM yako!
 
Mkandara nalifanyia kazi. Hata hivyo kuna hoja kubwa mbili ambazo nimeziona zikitolewa kwenye forum nyingine kuhusu kutowachangia vijana hawa. Kuna wale wanaosema "tukiwachangia hawa basi tutafungua lango la gharika ya michango kwa maelfu ya Watanzania watakaodai kuwa "wametelekezwa" na pia "Kwanini tuwachangie wakati wengi wetu wenyewe tumehangaika kupata elimu na wengine hata hatukumaliza kupata elimu tuliyokuja kutafuta nje, kwanini tuwape kila ambacho sisi hatukupata"? Natumaini hapa JF hakuna watu wenye mawazo ya namna hiyo, hata hivyo ukiwa gwiji wa uchunguzi wa mambo you don't anything for granted.

Sasa, Mawazo ya kusema "mbona mimi sikupewe kwanini nimpe mtu mwingine" ni mawazo ambayo hayana nafasi na niya kibinafsi sana. Kwanini tusijifunze kutoka kwa watu ambao wanajua maana ya kuchangiana kweli kweli? Wamarekani walipokutana na majanga kula New Orleans, na hata yale ya Ughaidi ya Sept 11 na wakaitishana michango hawakuulizana "mbona mimi sina nyumba kwanini nichangie". Pia wakati wale watu wa New Orleans wanatapatapa na Katrina ni wazi watu walilaumu mioyoni mwao kwa kujenga walivyojenga na kuishi walipoishi, hata hivyo hiyo haikuwa sababu at least kwa watu waliochanga mabilioni ya dola kutotoa michango yao.

Hiyo yawezekana kuwa ni mifano ya extremes, lakini ukweli ni kuwa Wamarekani hata kwenye jumuiya zao ndogo ndogo huchangiana kwa karibu kila kitu ambacho mtu anahitaji msaada, si kwa sababu kila anayechangia ana hali nzuri zaidi ya kifedha au hana matatizo yake mwenyewe. Hili la kutaka kuchanga pale unapofaidika wewe mwenyewe ndio limeanza hata kugeuza michango yetu ya zamani kama ndoa n.k kuanza kuwa ya kualikana na usipochangia basi "hupati mnuso". Tumeanza kuchangia kwa masharti kuwa na sisi tufaidike siyo kuchangia kwa kuguswa moyo na kutaka kumsaidia mtu regardless.

Kama mtu anachangia atachangia kwa uzuri wa moyo wake na si kwa sababu nyingine yoyote ile. Kama vijana hawa kuchangiwa na kupata elimu kitawauma watu wengine ambao wameshindwa kupata elimu kwa sababu mbalimbali sijui kama inawezekana kuwasaidia watu hao.

Ndio maana waswahili walisema, kutoa ni moyo siyo utajiri!! Tunapojaribu kuwachangia vijana hawa ni lazima tushinde hisia zetu za wivu, kutohusika, lawama, n.k na kuinua ndani yetu hisia ya utu wetu na heshima yetu kama Watanzania. Nawaambia hakuna kituu kinachokufanya ujihisi vizuri kama kumsaidia mtu ambaye una uhakika kuwa kweli anahitaji msaada wako na unampa kumuondolea adha yake bila kufanya deni. Serikali inapotaka kuwanunulia tiketi kwa mkopo siyo msaada bali ni kuwadhalilisha. Sisi tunapochangia vijana hawa wasome, na siku ile mkisia wana graduate kwa michango yenu na kurudi nyumbani, mtajisikia fahari kama fahari ya mzazi kuona mwanawe amekua!

Shime ndugu zangu, sisi tulio nje tumepewa utangulizi kwa sababu tunaweza kufanya mambo mengi kwa mtandao na tunaelewa, kule nyumbani hadi kesi iwekwe vizuri mbele ya hadhara ndipo michango itaanza kukusanywa. Tuoneshe mfano na tuamke tutende.
 
Huu ni moyo mzuri umeonyeshwa na Watanzania wenye access na mtandao.Mimi,kabla sijatoa mchango wangu naomba kuuliza,kama nilivyosikia ni kwamba serikali, imesema kuwa itawarudisha hawa vijana kuja kuendelea na masomo hapahapa nchini,sasa kama hawa vijana kweli watarudi,hizi pesa zinazochangwa zitaenda kwa nani? Pia,inafahamika ni kiasi gani wanahitaji,au tunachanga tu? Na kama hakitoshi,then inakuwaje?
 
Domo Kaya.. mi naona kwa vile serikali washafanya makosa.. hizo hela za nauli wachangie tu kwenye hiyo akaunti yaishe.. kuwakopesha watu waliokwisha nyimwa mikopo ni kutafuta sababu ya kuwadhalilisha watu bure.
 
Zanaki, vijana hawarudi na hakuna ahadi ya vijana hao kurudi wataendelea na masomo nyumbani. Serikali haijatoa ahadi kuwa wakirudi watapewa mikopo yao waendelee na masomo bali wakirudi waanza upya kuomba tena mikopo!! Sasa kama wameshanyimwa mahali ambapo walikubaliwa na wameshamaliza muhula mzima wa masomo, kwanini warudi nyumbani na kuanza at zero?

Kwa muhula huu ambao wamesoma bure na kulala bure vyuoni wanadaiwa kila mmoja dola 1500 x 26 sawa na 39000/ Kama Watanzania 500 tu wakichangia angalau dola 100 kila mmoja dola 50,000 zinapatikana kwa urahisi! Hadi hivi sasa watanzania wanne tayari wamechangia dola 250 kila mmoja na akaunti tayari ina dola 1000! Sasa tukisema basi watanzania 260 wachangie dola 150 kila mmoja tutapata hivyo dola 39,000 mara moja.

Siku ya tarehe 20 mwezi Mei mwaka huu JF peke yake kwa wakati mmoja tulikuta na wageni 762 ambao walikuwa wanafuatilia habari hii na nyingine (hasa baada ya kuzungumza na Rais na Waziri Mkuu na Prof. Msolla). Tukisema kuwa kati ya hao 300 hawawezi au hawatachangia basi tunao 462 ambao tukisema tuchange dola 50000, basi kila mmoja atatakiwa kuchanga less than dola 110! na tukisema watu hao wachange dola 220 tu basi tutapa dola laki moja, !!! sawa na shilingi milioni mia moja hivi!!!

Je inawezekana? kwa wasio na imani hakuna jambo linalowezekana, kwa wale tunaoamini katika wema wa wato hakuna jambo linaloshindikana! yote yawezekana!.. sasa hapa JF tukubaliane sisi wana JF tukubaliane tutatoa kiasi gani kila mmoja na tuone sisi peke yetu tunaweza kukusanya kiasi gani. Kama umeshatuma kwa vile sasa sihitaji jina au kitu chochote cha kukutambulisha kwangu unaweza kuniandikia au kuandika tu umetuma kiasi gani ili tujumulishe..! angalau tukubaliane isiwe chini ya dola 100.
 
MKJ upo right, ila tukiweke watu watakachojaaliwa mifukoni kwao, kwani we unajua hali ya familia zetu...zilipo...sipendi ntete lkn tusiwabane watu na pia wenye fursa wachangie zaidi. nashuri iwe min $50.0 wengine mnajua kila mwezi lazim uwachangie zaidi $300 wale wanaokuzunguka...kidgokidogo hujaza kibaba.....MKJ nashauri ukiweza kuwapigia kuongea na watu wa Aljazeera International maana siku hizi naona wanachukua market share na CNN etc..hasa wao wanapogusa issue za Africa..its possible wakalaunched hii in their way..
 
Jamani msikose kusikiliza BBC.. na habari leo... kwani.. moto bado wawashwa...
 
Wapinzani wawaokoa wanafunzi wanaosoma Ukraine
Shadrack Sagati
HabariLeo; Saturday,June 02, 2007 @00:06

Waomba wananchi wawachangie

VYAMA vinne vya upinzani vimewadhamini wanafunzi 26 wa Tanzania wanaosoma katika vyuo vya Ukraine waweze kuendelea na masomo yao.

Viongozi wa vyama hivyo walisema Dar es Salaam jana kuwa vyuo wanavyosoma wanafunzi hao vimekubali dhamana yao na vimekubali kuwapokea tena wanafunzi hao kwa ahadi kuwa fedha zinazodaiwa zitakuwa zimelipwa kufikia Juni 10, mwaka huu.

"Kutokana na tamko letu na kwa kuwa tumeonyesha kwa vitendo, vyuo vyao vimekubali dhamana tuliyowapatia, hivyo wamekubali kuwarejesha mabwenini ili mradi wawe wamelipa ada na fedha za malazi kabla ya Juni 10," alisema Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Shaibu Akwilombe wakati akisoma tamko la vyama hivyo jana.

Wanafunzi hao walifukuzwa kutoka vyuoni baada ya kukosa ada pamoja na fedha ya malazi. Walilazimika kukimbilia katika ubalozi wa Uingereza nchini humo kwa ajili ya kupata hifadhi.

Walikuwa wanadai kuwa wana mkataba na Serikali ya kuwasomesha, lakini Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia iliwaruka na serikali ikatuma tiketi ili warejee nchini.

Viongozi hao katika tamko lao wametoa wito kwa Watanzania bila kujali itikadi zao, kuwachangia wanafunzi hao ili waendelee na masomo yao. Kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Sheria (TANLET) tayari akaunti kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao imefunguliwa.

Akaunti hiyo, namba 201660043, ambayo imefunguliwa katika Benki ya NMB tawi la Bank House Dar es Salaam ina jina la michango ya dharura ya elimu. Akaunti hiyo inasimamiwa na Tanlet ambayo imekuwa inashughulika na masuala ya elimu.

Akwilombe alisema Sh milioni 13.2 zinahitajika haraka kuhakikisha wanafunzi hao wanalipa malazi.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akitoa mchanganuo wa fedha zote zinazotakiwa kulipwa kwa ajili ya wanafunzi hao, alisema dola za Marekani 10,100 (Sh milioni 13.2) zinatakiwa haraka. "Hiki ndicho ambacho tunawaomba Watanzania wachange haraka ili wanafunzi hao wasifukuzwe tena."

Alisema licha ya fedha hizo za malazi pia zinahitajika dola za Marekani 39,000 kwa ajili ya ada kwa wanafunzi wote 26. Alisema kuwa jumla ya fedha zinazohitajika ni Sh milioni 63.830 kwa mwaka mzima.

Mbatia alisema Watanzania watambue kuwa viongozi wa vyama hivyo vya siasa wameweka dhamana hiyo siyo kwa manufaa ya siasa, bali kwa kuthamini mchango wa elimu katika maendeleo ya taifa.

Alisema suala la elimu ni la maendeleo halipaswi kutanguliza itikadi za vyama, hivyo akatoa wito kwa Watanzania wenye uchungu na nchi yao wachangie kiasi chochote cha fedha ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo yao badala ya kurudi nyumbani.

Viongozi hao wamedai kuwa pamoja na Serikali kuwakana wanafunzi hao, wanafunzi watatu kati ya hao wameanza kudhaminiwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

"Hizo fedha za kuwadhamini hao zimetoka wapi na hao watoto ni akina nani?" Alihoji Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema.

Alipoulizwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, George Nyatega alisema hafahamu chochote juu ya madai hayo ya wapinzani. "Kwa hilo mimi sina taarifa, kama wapinzani wana vielelezo wavitoe," alisema.

Hivi karibuni serikali iliwakana wanafunzi 29 ikidai kuwa waliondoka bila kukamilisha taratibu za kukopeshwa. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestine Gesimba alisema Serikali iliwakatalia wanafunzi hao na kuwashauri wasome kwenye vyuo vya ndani, lakini wao walikataa.
 
Wapinzani wawaokoa wanafunzi wanaosoma Ukraine

Shadrack Sagati

HabariLeo; Saturday,June 02, 2007 @00:06


Waomba wananchi wawachangie

VYAMA vinne vya upinzani vimewadhamini wanafunzi 26 wa Tanzania wanaosoma katika vyuo vya Ukraine waweze kuendelea na masomo yao.

Viongozi wa vyama hivyo walisema Dar es Salaam jana kuwa vyuo wanavyosoma wanafunzi hao vimekubali dhamana yao na vimekubali kuwapokea tena wanafunzi hao kwa ahadi kuwa fedha zinazodaiwa zitakuwa zimelipwa kufikia Juni 10, mwaka huu.

“Kutokana na tamko letu na kwa kuwa tumeonyesha kwa vitendo, vyuo vyao vimekubali dhamana tuliyowapatia, hivyo wamekubali kuwarejesha mabwenini ili mradi wawe wamelipa ada na fedha za malazi kabla ya Juni 10,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Shaibu Akwilombe wakati akisoma tamko la vyama hivyo jana.

Wanafunzi hao walifukuzwa kutoka vyuoni baada ya kukosa ada pamoja na fedha ya malazi. Walilazimika kukimbilia katika ubalozi wa Uingereza nchini humo kwa ajili ya kupata hifadhi.

Walikuwa wanadai kuwa wana mkataba na Serikali ya kuwasomesha, lakini Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia iliwaruka na serikali ikatuma tiketi ili warejee nchini.

Viongozi hao katika tamko lao wametoa wito kwa Watanzania bila kujali itikadi zao, kuwachangia wanafunzi hao ili waendelee na masomo yao. Kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Sheria (TANLET) tayari akaunti kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao imefunguliwa.

Akaunti hiyo, namba 201660043, ambayo imefunguliwa katika Benki ya NMB tawi la Bank House Dar es Salaam ina jina la michango ya dharura ya elimu. Akaunti hiyo inasimamiwa na Tanlet ambayo imekuwa inashughulika na masuala ya elimu.

Akwilombe alisema Sh milioni 13.2 zinahitajika haraka kuhakikisha wanafunzi hao wanalipa malazi.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akitoa mchanganuo wa fedha zote zinazotakiwa kulipwa kwa ajili ya wanafunzi hao, alisema dola za Marekani 10,100 (Sh milioni 13.2) zinatakiwa haraka. “Hiki ndicho ambacho tunawaomba Watanzania wachange haraka ili wanafunzi hao wasifukuzwe tena.”

Alisema licha ya fedha hizo za malazi pia zinahitajika dola za Marekani 39,000 kwa ajili ya ada kwa wanafunzi wote 26. Alisema kuwa jumla ya fedha zinazohitajika ni Sh milioni 63.830 kwa mwaka mzima.

Mbatia alisema Watanzania watambue kuwa viongozi wa vyama hivyo vya siasa wameweka dhamana hiyo siyo kwa manufaa ya siasa, bali kwa kuthamini mchango wa elimu katika maendeleo ya taifa.

Alisema suala la elimu ni la maendeleo halipaswi kutanguliza itikadi za vyama, hivyo akatoa wito kwa Watanzania wenye uchungu na nchi yao wachangie kiasi chochote cha fedha ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo yao badala ya kurudi nyumbani.

Viongozi hao wamedai kuwa pamoja na Serikali kuwakana wanafunzi hao, wanafunzi watatu kati ya hao wameanza kudhaminiwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

“Hizo fedha za kuwadhamini hao zimetoka wapi na hao watoto ni akina nani?” Alihoji Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema.

Alipoulizwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, George Nyatega alisema hafahamu chochote juu ya madai hayo ya wapinzani. “Kwa hilo mimi sina taarifa, kama wapinzani wana vielelezo wavitoe,” alisema.

Hivi karibuni serikali iliwakana wanafunzi 29 ikidai kuwa waliondoka bila kukamilisha taratibu za kukopeshwa. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestine Gesimba alisema Serikali iliwakatalia wanafunzi hao na kuwashauri wasome kwenye vyuo vya ndani, lakini wao walikataa.
 
Hawa jamaa wanataka kulitumia hili kama mtaji wa kutokea kisiasa; wengi wao ni opportunists tumewazoea.
 
Editorial: Stranded students: Send fees, not cover up errors




HIGHER learning loans authorities have another embarrassing encounter in a short while after the stiff neck face off about the University of Dar es Salaam and its several affiliate colleges.

This time the cry is coming from afar, in the former Soviet republic of the Ukraine, with Tanzanian students said to be camped, or rather in refuge, at the UK High Commission. Not surprisingly the local scene has been ignited by the situation, with the opposition parties? leaders, practicing their newfound unity, addressing the issue together.

What seems to be the case is surprisingly clear enough for anyone to see through except the responsible ministry, either having erred in the first place to send students for studies, or erring now in backtracking on a promise.

Chances that 29 students or so would out of nowhere find themselves in such a distant place as the Ukraine, having identical promises of obtaining loans from the ministry (or rather the loans board) means their cases are the same. There would be variations in the failure to pay if they were private, not all of them.

Additionally, the Ukraine is so far away from this country, and scarcely a zone of likely emigration objective for someone to suspect that personal initiative outside official say on fees occurred. No one can take risks of traveling to such a far away place without actual assurance of fees arriving at a later date, and presume he would burden the government with his fees once his parent fails to pay. If anyone now says this was the case, one has to look twice in his eyes, to see if he perhaps has a reason not to be telling the whole truth.

That is why it is surprising that a few people, perhaps used to the ’Bongo’ method of living by cheating, are seeking to leaving about two dozen students high and dry to cover up for their own mistakes. Seeming to be harsh is a schoolmasterly habit that is often handy to cover up one’s own failures, in the absence of contingences within the ministry to respond to the problem. It is a way of trapping public authorities to come to the rescue, and then use informal channels within the ministry to clear out the blaming that surfaced.

NCCR Mageuzi chairman James Mbatia even suggested that three of the students had their fees cleared in the past few days, or obtained cheques for the same, after ’kitu kidogo’ was paid back home, though naturally he did not have to substantiate. Assuming that he was in a position to verify his statement, or at least cause enough to cite it as an example ? since the government didn’t say there are three genuine cases of late sending of payments ? it might make sense. It would amplify the picture of incompetence arising.

In the final analysis the ministry or its higher learning loans instrument needs to know that those whose welfare is more affected by a ruling on an unclear engagement on any issue are supposed to be given the benefit of doubt. The ministry or the board might insist that there was something conditional to sending the loans, or as it was the case with the recent stand off, how assured it was that it would cover all their needs. Since the students are far away from here, a certain amount of indulgence is acceptable in how the ministry moves to interpret their demands, as the ministry facilitated their taking the risk for good cause.

It is unfair to act as if the students were right here, penalizing them the return ticket, etc, as the right and proper thing to do is to facilitate their studies, on the basis of what they comprehended to be the case. As they did not arrange for the journey themselves but were in actual fact sent, it is pointless for the loans board or the ministry to renegotiate with them the terms of their going there. If there were any conditions they were required to fulfill, these would have been done before their visas were processed, without ifs or buts.
 
Majibu ya Rais kwa waandishi wa habari kuhusu wanafunzi hawa yalikuwa ya kukariri; sikuona na wala sikutegemea jipya.
 
kichuguu... hivi anapomuuliza Msolla, Mbegu na Nyatega kuhusu hawa wanafunzi anategemea jibu gani? I might be stupid.. but not that dumb
 
Mzee wa kijiji mimi nipo njia panda, Nadhani watanzania wote jana wamemsikia Mh. Raisi kuhusu hao wanafunzi wa Ukraine..... Kwa mdomo wake mwenyewe mbele ya runinga zetu amesema ya kwamba Wanafunzi hao walijipeleka wenyewe na wala serikali haihusiki kabisa na kupeleka wanafunzi huko (Hao 26) na serikari haiwezi kuwalipia wanafunzi wote ada kwa sababu kumsomesha mwanafunzi mmoja nje ya nchi ni sawa na kusomesha wanafunzi nane hapa nchini...... Swali kwako MWANAKIJIJI je hii hoja ya kwamba serikali imewatelekeza hao wanafunzi wewe umeipata wapi????????? Maana wengi tupo njia panda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…