Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

I found this on Tanzania Daima for those who need updates:

TANLET yasaidia wanafunzi Ukraine​
na Mkolo Kimenya

KATIKA kuwasaidia wanafunzi walikokwama nchini Ukraine, Shirika la kuhudumia wanafunzi la Tanzania Legal Education Trust (TANLET), limekusanya sh milioni 3 ambazo zitasaidia kuwalipia sehemu ya ada wanazodaiwa wanafunzi hao.
Uchangishaji wa fedha hizo umekuja baada ya wanafunzi hao kukwama kujilipia ada na serikali kukataa kuwalipia kwa kile kinachodaiwa kuwa, hawapo katika mahesabu ya kulipiwa na serikali.

Hivi karibuni, viongozi kutoka vyama vya upinzani vinne walilitaka shirika hilo kufungua akaunti maalumu kwa ajili ya wahisani mbalimbali kuweza kuchangia ili wanafunzi hao waweze kulipiwa fedha hizo.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TANLET, Mwalimu Nderakindo Kesi, aliiambia Tanzania Daima kuwa, hadi sasa akaunti hiyo ina sh milioni 3 na jana waliweza kuwatumia dola 1,000.

Alisema kiasi hicho bado ni kidogo kutokana na mahitaji ya fedha zinazotakiwa, kinachohitajika ni kikubwa kulingana na ukubwa wa ada wanazotakiwa kulipa.

“Fedha hizi bado ni kidogo kutokana na ukweli kuwa wanadaiwa fedha nyingi na katika akaunti kuna sh milioni 3, lakini hii ni kwa sababu hapa katikati tulikwama kuendelea kuchangisha kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo,” alisema Kesi.

Alisema mbali ya kufungua akunti hiyo yenye namba 2016600043 katika benki ya NMB, pia wanachangisha kupitia kusaini katika makaratasi ambapo wafanyabiashara wengi wamejitokeza kuchangia.
 
ahsante seni hamsini, ningelipenda kujua hali zao zinaendeleaja? na jee wanaendelea na masomo au weshafukuzwa?
 
Hapa mimi nasikia kidhungudhungu, si tumeambiwa vijana wetu walioko Ukraine wanasomea mambo ya sayansi kwenye Chuo Kikuu kilichotoa washindi watatu wa Nobel? Sasa kama kweli tunataka wataalamu hivyo kwanini tunataka kuwarudisha nyumbani? au hao wanasayansi watashushwa kutoka Mbinguni?

ni swali tu,

asante.


JK wants science subjects be given priority
SUNDAY NEWS Reporter
Sunday News; Sunday,July 08, 2007 @00:04

PRESIDENT Jakaya Kikwete has said that the country's development would only be brought about by scientific and technological revolution, and called on higher learning institutions to give priorities to science subjects.

He gave the challenge on Friday night during a fund-raising dinner for the Sebastian Kolowa University run by the Lutheran Church North Eastern Diocese.

"Science subjects must be given priority as many of our youths are not interested in the subjects, and girl students shy away from subjects such as mathematics. But for our country to develop we must put emphasis on science subjects," he said.

Mr Kikwete told those in attendance that Tanzania ranks amongst the lowest countries to have students who are pursuing science subjects.
He said that statistics show that of all the students in secondary schools, less than 30 per cent are taking science subjects.

"If you compare with other universities and other higher learning institutions in the world, we are the last in terms of ranking when it comes to undertaking science subjects, it is imperative that we put more efforts in strengthening the education sector but science subjects should be given special attention," he said.

Besides calling on universities and higher learning institutions to give priority to subject studies, President Kikwete also challenged both private and public universities to expand their institutions so as to accommodate more students.


Meanwhile, President Kikwete has commended Celtel Tanzania Limited for introducing BlackBerry smartphones in the country that can make clients access office files while out of office.

Mr Kikwete hailed Celtel after launching the company's new product in Dar es Salaam on Thursday night. The new technology has only been launched in Kenya, making Tanzania the second country for the technology to be introduced in Africa.

BlackBerry is a sophisticated technology that allows users to get in touch with their office or home while away. With the BlackBerry technology, people can also communicate and access data, Internet, files and update their office calendars while on safari.
 
hakuna chochote kinachoendelea, naweza nikasema watu ni wavivu wa kufikiria, kulazimishia MONETARY CONTRIBUTIONS kusomesha watu huko kupitia watz wachache ambao "SIDHANI" kama wataweza kuchangia, lakini kama serikali tokea mwanzo iliposema ingewanunulia tiketi jamaa wakarudi, wangerudi mapema ! lakini tena wakachelewa, mpaka watu wakastukia ndio nimesema wakstukiwa kwamba wanadaiwa ndipo administration ilipotia ngumu kusema haondoki mtu mpaka kieleweke ! sasa mna plan yoyote ya kuwalipia vijana deni lililobakia au mtaacha waendelee kusoma huku deni likizidi mpaka wanamaliza kusoma, then hapo ndipo balaa litakapokuwa maji ya shingo ? tusiwe na mambo ya kuona mambo ya sasa hivi tu, tuoneni miaka 3-4-5 wakimaliza shuleni itakuwaje na deni hilo !
 
Hii ishu ya hao vijana huko Ukraine naona watu wanazidisha siasa. Hata huku Tz wako wanafunzi wengi tu wanaojilipia masomo kwa asilimia 100 kwenye private universities, na inapotokea wamekosa ada serikali huwa haiingilii kati kuwalipia, badala yake ni sisi ndugu na jamaa tunaombwa michango kujazia palipopungua. Kwa taarifa yenu mlioko nje ya nchi, sasa hivi Tanzania ziko universities za binafsi zaidi ya 20 na zote zina wanafunzi. Sijawahi kusikia chama chochote cha siasa ama taasisi kama hii inayojiita TANLET ikijitolea kulipia ada wanafunzi wanaoshindwa kujilipia hapa nchini. Hata miaka kadhaa nyuma ilipotokea migomo UDSM na wanafunzi kadhaa wakafutiwa ufadhili wa serikali sikuona yeyote aliyejitokeza kuwalipia.

Hii tabia ya kutaka kukuza mambo itatupeleka pabaya. Hao kama walitaka msaada wa serikali wakaambiwa wangesaidiwa kurudi nyumbani, wangeukubali huo. Lau kama hawautaki, basi watafute wenyewe njia zao zingine na kusiwepo lawama zisizo na msingi.
 
Kithuku, inawezekana hujui jambo hili lilikoanzia. Hivi unafikiri watu wote hawajui maana ya kuchangia elimu? Kama hawa vijana wangejua hawatalipiwa si wasingeondoka nyumbani. Hebu soma toka mwanzo unaweza kuelewa ni nini kinachoendelea, siyo suala la ku"kujilipia masomo". Unajua wakati mwingine jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
 

Hiki ni kichekesho. Kijana atavutiwa vipi kusoma sayansi wakati:
1. Hao wenyewe waliosoma sayansi (madaktari, wataalamu wa kilimo na mifugo, wanamisitu, wahandisi, nk) hapa Tanzania hali zao ni "choka mbaya", wamegaragazwa vibaya kiuchumi hadi wanajuta kwa nini walisoma fani hizo. Wakiajiriwa serikalini wanalipwa "kiduchu", hakikidhi mahitaji. Wakijaribu biashara za fani zao wanapigwa kikumbo vibaya katika ushindani na makampuni ya kigeni ambayo yana msamaha wa kodi na yamewezeshwa na serikali hii hii kuhodhi soko la ndani katika kile kinachodaiwa ni "kuvutia wawekezaji!" Wakiajiriwa katika makampuni hayo ya kigeni wanapuuzwa na kubaguliwa ili wakate tamaa, wawapishe wataalamu wa kigeni waendelee "kupeta". Nafasi pekee anayopewa mzawa katika haya makampuni ya kigeni na haya yanayonunua mashirika yetu yaliyobinafsishwa ni "Public Realations Officer/Manager" (hii haihitaji masomo ya sayansi). Ndio, meneja uhusiano, ili aweze kudumisha uhusiano mzuri kati ya mnyonyaji na wanyonywaji. Na njaa ilivyo mbaya, wanakubali "kumtumikia kafiri wapate mradi wao".
2. Shule wanazosoma hazina chochote kinachofanana na sayansi. Hakuna maabara, vitabu, matukio au shughuli zinazohimiza sayansi.
3. Walimu wanaofundisha sayansi wanakatisha tamaa kwa hali zao. Walimu wako frustrated,malipo madogo hadi wanalazimika kufanya biashara ya kufuga bata na nguruwe (ndio wanaoweza kula mabaki ya ukoko wa ugali wa boarding schools), hata akimwambia mwanafunzi asome hiyo biology au chemistry mwanafunzi anawaza "kama nikiisoma hiyo nitaishia kuwa kama huyu mwalimu, basi hiyo sayansi ndio adui wa maendeleo". Walimu wa masomo ya lugha na michezo ndio angalao wana vipindi vichache (kwa hiyo wana muda wa kufuatilia "dili" za maana) na wanapata nafasi za kutoka na wanafunzi kwenda kwenye mashindano, wanapatako angalao "extra duty allowances" zinaongezea pale kwenye mshahara.
4. Mafanikio ambayo vijana wetu wanatangaziwa kila siku na vyombo vya habari ni ya wasanii, wanamichezo, wanamuziki (hii wanaita siku hizi "hip hop"), hakuna kinachooneshwa au kutangazwa kuhusu mafanikio anayopata mwanasayansi wa kitanzania. Sasa hapa utashangaa nini kusikia vijana wetu hawana "personal heroes" wenye mrengo wa sayansi? Ukimwuliza mvulana anavutiwa na mafanikio ya nani utatajiwa Tupac, Evander, Pete Samprass, etc. Msichana atataja sijui Tyra Banks, Mariah Carey, sijui hao kina miss Tanzania, ati ndio "heroes" wake. ndicho wanachoona na kusikia kikivuma kila kukicha. Hiyo sayansi wataipenda kivipi?
5. Hata hao wanaosifiwa ni mashujaa wa nchi hakuna aliyepata sifa hiyo kutokana na kuwa mwanasayansi. Wanaenziwa wanasiasa tu, na ndio wanaoandikwa kwenye vitabu vyetu vya historia, kiasi cha kujenga hisia kwamba historia ni somo la siasa za kale. Kumbe kila fani inahusika katika historia, lakini huku kwetu historia ni siasa tu. University zetu zina majina ya wanasiasa. Barabara zote zina majina ya wanasiasa. Hospitali pia majina ya wanasiasa. Shule za msingi na sekondari pia wanasiasa. Hakuna jitihada zozote za kuenzi mchango wa wanasayansi wachache tulionao. Nani asome sayansi?
6. Wanasayansi waliobobea wa kitanzania wamegundua (quite late of course, wengi ni baada ya kupata PhD) kwamba walikosea kusoma masomo hayo, kwani "wanalosti". Haraka wakabadili mbinu wakakimbilia kwenye siasa, ndiko kuna unafuu. Dr Mohamed Bilal alikuwa anafundisha Nuclear Physics pale UDSM. Profesa Juma Kapuya ni mtaalamu wa botany. Profesa Philemon Sarungi ni daktari bingwa wa mifupa. Prof Mark Mwandosya ni electrical engineer. Dr Alli Mohamed Shein ni bingwa wa biochemistry. Ritha Mlaki ana M.Sc ya chemistry (synthetics, hasa plastics). Hata huyu waziri machachari John Pombe Maghufuli alikuwa mwalimu katika shule ya sekondari wa masomo ya sayansi, baadaye akafanya M.Sc ya Chemistry. Hawa wote ni miongoni mwa wanasayansi waliogundua kwamba kusoma sayansi hakumfanikishi mtu katika mazingira ya kitanzania, wakageukia kwenye siasa. Na huko wamefanikiwa. Nina uhakika wakiwatazama wenzao waliobaki kwenye fani wanawasikitikia! Nani asome sayansi?
7. Wachuuzi (including hata machinga, madalali, mapromota uchwara n.k) ndio wenye nafuu mara nyingi kuliko hao waliosoma hizo sayansi. Nani asome sayansi?

Kama mhe Rais anamaanisha kweli anachokisema kuhusu kuhimiza watu wasome sayansi, ayaangalie kwanza mambo yanayopingana na himizo hilo, na makubwa kati ya hayo ndiyo niliyoyataja juu.
 
Duuu! Kithuku, umeniua kabisaaaaa!!
Yaani mwenzio ndo kwanza niko nakesha ilinipate udakitali wa sayansi, kwa mwendo huu naona mbele giza, inabidi nichaprishe niende nikatafute digrii ya uchitarilo ya kwenye mtandao nibadilishe fani mara moja.YAANI UMESEMA KWELI TUPU!

Ili sayansi ikubalike inabidi kufanya mageuzi katika hayo ulo yataja.
 

I definitely CO-SIGN on this one...
 
Niliposoma jina nikadhani ni Mkenya hivi; lakini kiswahili safi hicho.

Lo, umenena hasa. Hali ilivyo leo hapa Tanzania kwa kweli sayansi haimpeleki popote mtu.
Lakini kama ulivyosema, panahitajika juhudi kubwa kabisa za kisera ili kubadili huu mwelekeo. Kimaendeleo hatutafika mbali kama msingi wetu kielimu utaendelea kupuuza sayansi.

Mimi ninalichukulia tamko hili la Rais Kikwete kuwa serikali yake imeuona udhaifu huu, na kwamba hatua za haraka sana zitachukuliwa ili hali ibadilishwe.
Maendeleo ya nchi yetu na kwa uchumi kwa ujumla utahitaji msingi imara katika mihimiri ya Information Tecnology; Biotechnology, na Nanotechnology. Hii sio ndoto, na wala hatujachelewa kama tukianza mara moja kutoa kipaumbele maeneo haya. Waheshimiwa akina Msolwa wakisema tuanze, nina hakika tutafanikiwa.
 
Wadau hii issue ya Hawa vijana iliishia wapi? Mwkjj tupe update naona siku nyingi sijasikia. Balozi alienda huko sijui ilikuwa je. Tu update.
 
mkjj hii ndio keshaiweka kapuni, sasa katoka na ya kisungura. si unamjua kaka yetu yuko busy na kutetea wanyonge!!! bravo mwanakjj
 
Naona rais alikuwa anatania. Nadhani mimi nikiwa na mtoto ntamshawishi asomee mambo ya politix na sio science. Angalia kiinua mgongo anachopata mbunge baada ya service ya miaka mitano, na anachopata "mwanasayansi" wa Tanzania, au mwalimu na mwingine aliyesoma masomo hayo. Sasa hapo ukweli uko wapi, wasomi wengi Tanzania wamekimbia taaluma zao na kujiingiza kwenye politics per se, wao si wajinga.
 
jamani, hii issue ilishatolewa update sasa kama kuna mtu alimiss unaweza kusearch "nawahabarisha"...
 
Mwanakijiji what happened then? where are the kids, walipata pesa au ilikuwaje?? At least now we know Msolla went to Kilimo...So any progress let us know bana...Lol!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…